Wanaharakati
wanaopinga Sheria ya Huduma za Habari iliyopitishwa hivi karibuni wamepata pigo
baada ya mmoja ya wakili Bw. Francis Stolla kujitoa katika utetezi.
Akiongea leo Jijini
Dar es Salaam Wakili nguli wa Kujitegemea Bw. Stolla alisema kuwa ameamua
kujitoa katika kesi hiyo iliyofunguliwa na wanaharakati dhidi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali kutokana na kukabiliwa na majukumu mengine.
“Wakati Shauri
linafunguliwa Arusha sikuwepo kwa sababu ya majukumu mengine, pia
lilivyofunguliwa Mwanza sikuwepo hivyo kutokana na hilo nimeamua kuwaachia
mawakili wengine waendelee na shauri hilo na mimi niendelee na majukumu
mengine” alisisitiza Wakili Stolla.
Alisema kuwa madai
makubwa ya mawakili hao ni kwamba Sheria ya Huduma za habari inakiuka mkataba
wa Afrika Mashariki, na kusema kuwa kesi iliyofunguliwa Mwanza inaitaka
Mahakama itamke kwamba kuna baadhi ya vifungu vilivyotajwa kwenye Sheria ya
Huduma Habari inakiuka Katiba ya nchi.
Akiongea kuhusu dalili
za kushindwa kwa kesi hiyo iliyofunguliwa na wanaharakati dhidi ya Mwanasheria
Mkuu wa Serikali katika mahakama ya haki ya Afrika Mashariki na Mahakama kuu
Mwanza Bw. Francis Stolla alisema suala hilo anaiachia mahakama kwani ni
kinyume kutoa mapendekezo wa kesi kushindwa au kushinda.
“Mara nyingi huwa tunaiachia
Mahakama na mashauri hayo yote mawili yapo Mahakamani huwezi sema shauri hili
litashinda ama kushindwa kwa sababu mashauri yakiwa mahakamani haturuhusiwi
kusema shauri hili litashinda ama kushindwa ili Mahakama ibakie kuwa huru”
alisema Wakili Stolla.
Kesi hiyo ilifunguliwa
na wanaharakati katika mahakama ya haki ya Afrika Mashariki mkoani Arusha na
Mahakama kuu ya Tanzania Mkoani Mwanza.
No comments:
Post a Comment