Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndasa
Sekta ya Kilimo
inachangia ajira takribani asilimia 70 ya Watanzania ambapo imekuwa ikitegemewa
kusaidia kufanikisha juhudi za kupunguza umaskini hasa Vijijini na kuchochea
mapinduzi ya Viwanda. Kwa mwaka 2015 ukuaji wa sekta hiyo ulikuwa ni
Makamu Mwenyekiti wa
Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Josephat Kandege ameyasema hayo leo
Bungeni, Mjini Dodoma alipokuwa akisoma taarifa ya utekelezaji ya kamati hiyo
kwa kipindi cha mwezi Januari 2016 hadi Januari 2017.
Kandege amesema kuwa
sekta hiyo imekuwa ikitegemewa na watanzania wengi katika kuwaingizia kipato na
hata kuinua uchumi wa Nchi, lakini wakulima wamekuwa wakipata changamoto
mbalimbali katika Sekta hiyo kama vile gharama kubwa ya pembejeo, ukosefu wa
masoko ya uhakika na idadi ndogo ya wataalamu wa Kilimo.
“Kamati inaishauri
Serikali kuanza kutekeleza mikakati madhubuti ya kuinua sekta hii kwa kuboresha
kilimo cha umwagiliaji, kuboresha teknolojia ya Kilimo, kuwezesha
uanzishwaji wa viwanda vingi vya usindikaji wa mazao ya kilimo na kusambaza
maafisa ugani wa kutosha katika maeneo yote ya nchi,” alisema Kandege.
Kwa upande wake,
Mbunge wa Jimbo la Sumve, Richard Ndasa amesema kuwa Kilimo kinahitaji
uwekezaji mkubwa hivyo ni vyema Serikali ikawekeza katika sekta hiyo kikamilifu
ili kuinua uchumi wa Nchi na mtu mmoja mmoja.
Akijibu hoja hizo,
Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi Ole Nasha amesema kuwa Wizara hiyo
imejipanga kupambana na changamato za pembejeo ambazo zimekuwa zikipatikana kwa
gharama ya juu maeneo mengi nchini.
Hata hivyo amesema
kuwa wizara hiyo iko katika mkakati wa kuanza kuzalisha mbolea ndani ya nchi
ili kupunguza gharama ya mbolea na ili iweze kuuzwa kwa bei moja nchi nzima.
No comments:
Post a Comment