Wakurugenzi na wenyeviti wa halmashauri mbili ya mji na wilaya ya Geita wakisaini makubaliano.(katikati) Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw. Richard Jordinso. |
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi aweka saini kwenye hati ya makubaliano ya miradi kwenye halmashauri mbili ya mji na wilaya. |
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akimkabidhi hati ya makubaliano mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola. |
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi ,akimkabidhi hati ya makubaliano mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Elisha Lupuga. |
Saini ya Makubaliano hayo inafuatia kutokana na marekebisho ya Sheria
Mpya ya Madini iliyopitishwa na Serikali ya Tanzania kwa lengo la kufanya
mageuzi kwenye utekelezaji wa Fedha za Miradi ya Huduma za Jamii baina ya
Kampuni za Uchimbaji Madini na Jamii kwenye eneo husika.
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi alisema Serikali mkoani
humo imekusudia kuanzisha miradi mipya ikiwemo kiwanda cha sukari kutokana na
mapato yanayotolewa na mgodi wa dhahabu wa GGM baada ya kuingia mkataba upya na
halmashauri ya mji na wilaya ya Geita.
Aliongeza kuwa fedha zilizokwisha kutolewa na GGM kwa mwaka huu ni
Bilioni tisa pointi mbili (B 9.2) ambapo fedha hizo zitatumika kuanzisha miradi
mbalimbali itakayo wawezesha wananchi kujikwamua na umasikini, ikiwemo kiwanda
cha sukari ,afya elimu na mazingira.
“Kifungu cha 105 (01) cha Sheria Mpya ya Madini kinazielekeza Kampuni
zote za Uchimbaji Madini kuandaa Mpango wa matumizi ya Fedha za Huduma ya Jamii
kwa kushirikiana na Halmashauri husika kabla ya kuanzisha Miradi yoyote ya
Maendeleo,na hiyo ndiyo sababu leo hii makubaliano hayo ya nafanywa,” alisema
Luhumbi.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mgodi wa Dhahabu Geita(GGM) Bw. Richard Jordinso
alisema kuwa wanajivunia mafanikio hayo na kwamba wanaamini kufanya kazi na
jamii inayowazunguka ili kuweza kuleta chachu ya maendeleo kwenye jamii
inayouzunguka mgodi huo.
Makubaliano hayo ambayo yamefikiwa jana yatatarajia
kutekeleza miradi mipya ya maendeleo kwa mwaka 2018 katika sekta ya afya
,miundo mbinu,mjai,elimu,sanaa na utamaduni pamoja na kuwajenhea uwezo
wajasiriamali wadogo na wakati.
No comments:
Post a Comment