Zaidi ya kaya 139 katika kijiji cha mkuyuni kata ya chato wilayani chato mkoani Geita zimekumbwa na mafuriko ya maji kufuatia mvua zinazo endelea kunyesha huku kaya 24 kati ya hizo zikikosa mahala pakuishi baada ya nyumba zao kubomoka.
Baadhi ya wahanga wa tukio hilo
wameimbia storm habari kuwa kadhia hiyo imetokana na mvua kubwa iliyo nyesha
March 26 mwaka huu nakusababisha maji kuzingira na kujaa ndani na nje ya makazi
yao hali iliyo pelekea baadhi ya nyumba hizo kubomoka likiwemo kanisa la EAGT
lililo kuwa limejengwa kwa thamani ya shilingi milioni hamsini.
Mwenyekiti wa kijiji hicho Bw. Anaclet
Frances amesema licha ya madhara yaliyo jitokeza hakuna vifo wala majeruhi kwa
kuwa walichukuwa tahadhari mapema baada ya kuona dalili za mafuriko hayo
nakuiomba serikali kuchimba mtalo mkubwa utakao saidia kusafirisha maji hayo kueleakea
ziwa Victoria.
Akizungumzia tukio hilo kwenye
kikao cha baraza la madiwani mkuu wa wilaya hiyo Bw Shaban ntarambe
amewahakikishia wananchi hao kuwa atalifanyia kazi suala hilo kwa kujenga mtalo
mkubwa utakao saidia kutiririsha maji hayo.
Sanjari na hayo amewataka
wananchi wanao ishi mabondeni na kwenye mikondo ya maji kuhakikisha wanahana
kwa hiyari ili kuepuka madhara makubwa zaidi yanayoweza kujitokeza.
No comments:
Post a Comment