Serikali
imewataka walimu wa shule za msingi na sekondari nchini kuwasilisha madai yao
yasiyo kuwa ya Mishahara ikiwemo stahili za likizo ili waweze kulipwa madai
hayo kwa wakati.
Hayo yamesemwa jana na Waziri wa Elimu, Sayansi na
Teknolojia Profesa Joyce Ndalichako wakati wa mahojiano ya kipindi maalum cha
TUNATEKELEZA kinachorushwa na kituo cha Televisheni cha Taifa (TBC1).
Profesa Ndalichako alisema kuwa Madeni ya Walimu
yamegawanyika katika sehemu mbili ambazo ni madai yatokanayo na mishahara na
yasiyokuwa ya mishahara ambayo yamekuwa yakilipwa na Serikali kupitia Wizara
yake ambapo hadi hivi sasa hakuna mtumishi ambaye hajalipwa.
“Hakuna jalada la madai ya walimu yasiyokuwa ya
mishahara na kama yapo madai walete ili walipwe kwani fedha zipo”. Alisema
Profesa Ndalichako na kuongeza kuwa madai ya mishahara yamekuwa
yakishughulikiwa na Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma ambapo nayo
yamekuwa yakifanyika.
Kwa mujibu wa Profesa ndalichako alisema Serikali
imekuwa ikipata ufadhili kutoka Serikali ya Sweden kwa ajili ya kusaidia katika
kulipa stahili mbalimbali za walimu ili kuboresha weledi wa taaluma yao.
Kwa upande wa ubora wa Elimu, Ndalichako alisema
kuwa pamoja na changamoto zilizopo katika sekta elimu, ubora wa Elimu ya
Tanzania umekuwa ukifanyiwa kazi kupitia program mbalimbali zikiwemo za mpango
wa Kusoma, Kuandika na Kuhesabu (KKK).
Akitolea mfano Waziri Ndalichako alisema kuwa
kumekuwapo na maboresho makubwa tokea enzi za mpango wa UPE miaka ya 1970 ambao
lengo lake lilikuwa kuwawezesha wanafunzi wengi zaidi kujiunga na elimu ya
msingi.
Waziri Ndalichako mwaka 2013 Serikali iliendelea
kufanya maboresho kwa kuongeza sifa za kujiunga na vyuo vya ualimu ili kupata
walimu wenye ubora ndipo udahili wa ikiwemo ufaulu wa daraja la tatu kwa
wahitimu wa kidato cha nne na ufaulu wa masomo mawili katika kidato cha sita.
“Serikali ilianzisha Sera ya Elimu na Mafunzo ya
mwaka 2014 ambayo ilibainisha kuwa elimu ya msingi na mafunzo mwanafunzi atatakiwa
atasoma darasa la kwanza hadi la 6 kwa msingi na mafunzo ni kuanzia darasa la 7
hadi la 12”.
No comments:
Post a Comment