Thursday 31 March 2016

HIFADHI YA SAADANI YATEMBELEWA NA WAJUMBE WA KAMATI YA MALIASILI NA UTALII.


1.     Mkuu wa Hifadhi ya Saadani Bw. Hassan Nguluma akiwaonesha Wajumbe wa Kamati ya Maliasili, Utalii na Ardhi ramani ya Hifadhi hiyo wakati kamati hiyo ilipoitembelea Hifadhi ya Saadani pamoja na kukutana na Menejimenti ya TANAPA. Wengine katika picha ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani (mweye miwani) na Kulia kwake ni Mwenyekiti wa Kamati hiyo Mhe Atashasta Nditiye.

2.  Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii Mhe Atashasta Nditiye akizungumza na Menejimenti ya TANAPA wakati kamati hiyo iliopotembelea Hifadhi ya Saadani. Kulia kwake ni Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani

3.   Mkurugenzi wa Masoko na Utalii wa TANAPA Bw. Ibrahim Musa akitoa ufafanuzi wa masuala mbalimbali wakati akizungumza na Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.

4.    Naibu Waziri wa Utalii na Maliasili Mhandisi Ramo Makani akifafanua jambo kwa Wajumbe wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii. Kamati hiyo ilikutana na TANAPA katika Hifadhi ya Saadani.



No comments:

Post a Comment