Friday 29 September 2017

PICHA: UTIAJI SAINI MRADI WA UJENZI WA RELI YA KISASA NCHINI


    Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi  kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakisaini Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.


 Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi  kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakibadilishana Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa (kulia) na pamoja na Mjumbe wa Bodi  kutoka Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakionyesha kwa waandishi wa habari  Mkataba wa ujenzi wa mradi wa Reli ya Kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.


Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) Masanja Kadogosa akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.


Mwenyekiti wa Kamati ya Bajeti ya Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Hawa Ghasia akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.


      Baadhi ya Wahandisi kutoka kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki wakifuatilia hafla ya utiaji saini saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.


Baadhi ya Wafanyakazi kutoka shirika la Reli Nchini (TRL) na kampuni hodhi ya Rasilimali za Reli (RAHCO) wakifuatilia hafla ya utiaji saini saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.



  Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano (Uchukuzi) Dkt. Leonard Chamuriho akizungumza akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.


1  Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akibadilishana mawazo na Mjumbe wa Bodi ya Kampuni ya Ukandarasi ya Yapi Merkezi Insaat ya nchini Uturuki, Erdem Ariogl  pamoja na Kaimu Balozi wa nchini hiyo Yunus Belet wakati wa utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.


Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano, Profesa Makame Mbarawa akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa mkataba wa mradi wa ujenzi wa reli ya kisasa kutoka Morogoro- Makutopora (Dodoma). Halfa hiyo ilifanyika leo Septemba 29, 2017.




TANZANIA YAKABIDHIWA MASHINE YA KUTOA DAWA YA USINGIZI WAKATI WA UPASUAJI


Pichani ni muonekano wa mashine ya kutolea dawa za usingizi, ambayo imetolewa msaada na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. 



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisisitiza jambo wakati wa hafla ya kupokea msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi zilizotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ). Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Idara kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya na  Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ) Rose  Mlay.

 

Mratibu wa Taifa wa Muungano wa Utepe Mweupe wa Uzazi Salama (WRATZ) Rose  Mlay akielezea jambo wakati wa hafla ya kukabidhi msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ). Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Waziri wa Afya, Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akisalimiana na Mkurugenzi wa Kampuni ya Kas Medics Limited Nishitha Kulshreshtha  mara baada ya kukabidhiwa kukabidhiwa msaada wa mashine ya kutoa dawa za usingizi iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) kufuatia udhamini wa kampuni hiyo leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu wa Wizara hiyo (Idara kuu ya Afya) Dkt. Mpoki Ulisubisya.



Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii , Jinsia, Wazee na Watoto Ummy Mwalimu akipata maelezo kuhusu namna mashine ya kutolea dawa za usingizi inavyofanya kazi wakati wa hafla ya kukabidhiwa msaada wa mashine hiyo iliyotolewa na Muungano wa Utepe Mweupe Tanzania (WRATZ) leo Jijini Dar es Salaam. Mashine hiyo yenye thamani ya Sh. Mil.55 imetolewa na Kampuni ya Kas Medics Limited ikiwa ni matokeo ya uhamasishaji wa kupunguza vifo vya wakina mama na watoto leo Jijini Dar es Salaam.

SERIKALI KUZICHUKULIA HATUA TAASISI ZILIZOKIUKA TARATIBU ZA MANUNUZI 2016/2017


Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga (kushoto) akiongea wakati wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma,  Kulia ni Mjumbe wa Bodi hiyo Prof. Sufian Bukurura.


Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akimsikiliza Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga wakati wa makabidhiano ya Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.




Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga akimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akikata utembe baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.



Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akionesha kwa wanahabari na wajumbe wengine wa Bodi(hawapo pichani) kitabu cha Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma, , Kulia ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Balozi Dkt. Matern Lumbanga.





Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiongea na wajumbe wa Bodi ya ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) baada ya kupokea Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma ambapo ameahidi kuzichukulia hatua taasisi zote zilizokiuka taratibu za manunuzi zilizoainishwa kwenye Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017.



Mtendaji Mkuu wa Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA) Dkt. Laurent Shirima akiongea, wakati wakimkabidhi Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango Ripoti ya Tathmini ya Utendaji kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 Leo Mjini Dodoma.



Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwa katika picha ya pamoja na wajumbe wa Bodi ya ya Mamlaka ya Udhibiti wa Manunuzi  ya  Umma (PPRA).

WAZIRI MWAKYEMBE APIGA MARUFUKU MATUMIZI YA TAKWIMU ZA KAMPUNI YA GEOPOLL



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akizungumza wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa na kulia ni Mjumbe kutoka Mamlaka ya Mawasiliano Tanzania (TCRA) Dkt. Raynold Mfungahema



Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa (kushoto) akifafanua jambo wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam. Kulia ni Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe



Mwakilishi kutoka kampuni ya IPSOS inayokusanya takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji Bw. Samuel Muthoka akiwasilisha taarifa ya namna kampuni hiyo inavyofanya kazi wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam.



Mwakilishi kutoka African Swahili  Televisheni akichangia mada wakati wa kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam.



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (waliokaa watatu kulia) katika picha ya pamoja na wadau walioshiriki kikao cha wadau wa ukusanyaji na usambazaji wa takwimu zinazohusu sekta ya utangazaji jana Jijini Dar es Salaam. Watatu kushoto waliokaa ni Mkurugenzi Mkuu Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS) Bibi. Albinus Chuwa

BENKI YA NMB YAZUNGUMZA NA WALIMU MKOANI GEITA



 Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga  Akizungumza na walimu wakati wa Kongamano ambalo limeandaliwa na NMB Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita. 




 Baadhi ya walimu ambao wanatoka kwenye halmashauri zilizopo Mkoani Geita wakifuatilia Hotuba ya Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga. 



 Meneja wa Benki  ya NMB  Mkoani Geita Mathias Nkuliwa akizungumza wenye Kongamano hilo ambapo alisema lengo la kungamano hilo ni kutambua mchango wa walimu katika Benki ya NMB. 



 Meneja  wa NMB Kanda ya ziwa Abraham Augustino  akizungumza na walimu wakati wa 
Kongamano. 





 Meza Kuu ikiongozwa na Mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Mkoa wa Geita  wakimsikiliza meneja wa kanda wakati alipokuwa akizungumza. 





 Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga  Akizungumza na walimu wakati wa Kongamano ambalo limeandaliwa na NMB Kwenye Ukumbi wa Halmashauri ya Mji wa Geita. 






 Baadhi ya wafanyakazi wa NMB wakisikiliza maelezo ya  Mkuu wa kitengo cha Biashara Kwa Wateja Binafsi na Mauzo wa NMB Omar Mtiga  wakati akizungumza kwenye Kongamano hilo.




 Mkuu wa Mkoa wa Geita  Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga ambaye alikuwa Mgeni Rasmi akifungua Kongamano la walimu na Benki ya NMB  ambalo limefanyika kwa mala ya kwanza Mkoani Geita. 





 Baadhi ya wadau wa idara ya Elimu Mkoani Geita wakimtegea sikio Mgeni Rasmi. wakati alipokuwa akizungumza na walimu pamoja na wafanyakazi wa NMB Mkoani Geita. 



 Mkuu wa Mkoa  wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa kwenye picha ya pamoja na wafanyakazi wa NMB. 






 Mkuu wa Mkoa  wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akiwa kwenye picha ya pamoja na maafisa Elimu wa Wilaya mbali mbali zilizopo Mkoani Geita.





 Mkuu wa Mkoa wa Geita akiondoka na kuagana na Wafanyakazi wa NMB baada ya kuwa amefungua Kongamano hilo.  


Wednesday 27 September 2017

WAZIRI MKUU ATOA MAAGIZO KWA WAKUU WA MIKOA 11



Waziri mkuu Kassim Majaliwa amewataka wakuu wa mikoa 11 inayolima pamba nchini wahakikishe wanasimamia vizuri wakulima wa zao hilo ili kuongeza uzalishaji na kuwaletea tija wananchi.

AHMADIYYA KUFANYA MKUTANO MKUU WA 48 JIJINI DAR ES SALAAM



Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Sheikh Abdurahman Muhamed Ame (kushoto) akielezea juu ya Mkutano wa 48 wa Jumuiya hiyo mbele ya waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika  tarehe 30 September hadi 1 Oktoba leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya hiyo Tahir Mahmood Chandhry.


 

Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania  Tahir Mahmood Chandhry (katikati) akifafanua jambo juu ya Mkuatano Mkuu wa 48 wa Jumuiya hiyo mbele ya waandishi wa habari unaotarajiwa kufanyika  tarehe 30 September hadi 1 Oktoba,  leo jijini Dar es Salaam. Kushoto  ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya hiyo Sheikh Abdurahman Muhamed Ame, Kulia ni Katibu wa Uchapishaji wa Jumuiya hiyo, Jamil Mwanga.

 


Amir na Mbashiri Mkuu wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Tahir Mahmood Chandhry (katikati) akisoma barua iliyotumwa na Khalifatul Masihi Mkuu wa Jumuiya hiyo duniani Mirza Mansoor Ahmad mbele ya waandishi wa habari kuelekea katika Mkutano Mkuu wa 48 utakaofanyika  tarehe 30 September hadi 1 Oktoba mwaka huu, leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Katibu Mkuu Msaidizi wa Jumuiya ya Waislam ya Ahmadiyya Tanzania Sheikh Abdurahman Muhamed Ame. Kulia ni  Kulia ni Katibu wa Uchapishaji wa Jumuiya hiyo Jamil Mwanga.

Tuesday 26 September 2017

WAZIRI MWAKYEMBE AZINDUA MPANGO WA USAJILI NA UTOAJI VYETI KWA WATOTO WALIO CHINI YA UMRI MIAKA 5 MTWARA NA LINDI




Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akikata utepe katika Kitabu cha Usajili pamoja na Simu kuashiria Uzinduzi wa Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mikoa ya Lindi na Mtwara leo 26 Septemba, 2017. 


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe (aliyevaa kofia ya pama) akiwakabidhi vyeti Wazazi kwa niaba ya watoto wao wenye umri chini ya miaka mitano wakati wa Uzinduzi wa Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano leo Wilayani Tandahimba, Mkoani Mtwara 26 Septemba, 2017.


Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe akiwa katika picha ya pamoja na Wadau mbalimbali wanaosaidia Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano mara baada ya kuuzindua leo Wialayani Tandahimba, Mkoani Mtwara, 26 Septemba, 2017.

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Mhe. Dkt. Harrison Mwakyembe kwa niaba ya Waziri wa Katiba na Sheria, Mhe. Prof. John Palamagamba amezindua Mpango wa Usajili na Utoaji Vyeti kwa Watoto waliochini ya Umri Miaka Mitano kwa Mikoa ya Mtwara na Lindi.