
Leo June 8, 2018 Baraza la Taifa la Elimu
ya Ufundi (NACTE) limefuta usajili wa vyuo 20 kwa kushindwa kufuata utaratibu
wa usajili wa vyuo vya ufundi na upungufu wa Rasilimali za
kufundishia
Pia Baraza limezuia vyuo 9 kudahili wanafunzi wapya kwa mwaka wa
masomo 2018/19 na vyuo 3 vimesitishwa kutoa program zisizohidhinishwa na Baraza
hilo.
Kaimu Katibu Mtendaji wa
NACTE, Dkt. Adolf Rutayuga amesema vyuo hivyo bado
vina nafasi ya kuomba usajili upya endapo watarekebisha matatizo na utaratibu
ukafuatwa.
“Matokeo ya uchunguzi
uliofanywa kuanzia July 2017 mpaka September 2017 ambao ulihusisha vyuo 458
ambapo 112 vya ualimu na vingine 7 vilivyokutwa haviendelei na shughuli za
elimu, vyuo 426 vimekidhi vigezo lakini vyuo 32 vimekutwa na mapungufu hivyo
Baraza limechukua hatua mbalimbali kwa vyuo hivyo 32,” - Dkt. Rutayunga
No comments:
Post a Comment