Wednesday 16 March 2016

MIRADI YA BIL.1.7 INAYOTOLEWA NA MGODI WA GEITA(GGM)KULETA CHACHU YA MAENDELEO.


  Vijana wakiwa kwenye mafunzo ya uchomeleaji.

Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) umekuwa ukichangia kwa kiasi kikubwa katika utoaji wa fursa za kiuchumi kwa wananchi wanaozunguka Mgodi huo, ambapo kwa sasa inatekeleza miradi mipya mitatu ambayo ni uchomeleaji,kilimo na ushonaji.

Kwa leo utaona picha mbalimbali za mafunzo ya uchomeleaji wanayopewa baadhi ya vijana ambapo watakapofuzu mafunzo watakuwa na jukumu la kuwafundisha vijana wenzao ikiwa  ni njia ya kuweza kuwainua wakazi wa Geita  kuona fursa za kiuchumi.
Mafunzo hayo yanatolewa bure na hapo juu ni picha mbalimbali za vijana wakipata mafunzo ya uchomeleaji.

Huu ni mradi wa kwanza tumeuona kwani pia kuna  miradi mingine yenye tija inayofadhiliwa na Mgodi wa GGM wakishirikiana na Serikali.

No comments:

Post a Comment