Tuesday 15 March 2016

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUWASILI KESHO MKOANI GEITA KWA ZIARA YA SIKU MBILI KIKAZI.



Waziri mkuu wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Mh.Kassimu Majaliwa kesho marchi 16 anatarajia kuanza ziara ya kikazi ambayo ni ya siku mbili mkoani Geita.


Akizungumzia  kwa niaba ya mkuu wa mkoa juu ya ziara hiyo mkuu wa wilaya ya Geita Mh. Manzie Manguchie amesema kuwa ziara ya waziri mkuu mkoani hapa itaanza kesho kwa kuanzia wilayani Chato na kisha siku itakayofuatia atamalizia katika wilaya ya Geita.

Aidha Mh.Manguchie ameongeza kuwa waziri mkuu katika ziara yake atakutana na wananchi ikiwa ni pamoja na kufanya mikutano ya hadhara na kutembelea katika maeneo tofauti na kujionea kazi ambazo zinafanyika katika maeneo ya wilaya ya Chato na Geita.

Mkuu  wa wilaya amewataka wananchi mkoani hapa kujitokeza kwa wingi kumsikiliza waziri mkuu  katika maeneo ambayo atafanya mikutano ya hadhara.

No comments:

Post a Comment