Saturday 12 March 2016

TAKUKURU, WILAYANI BUKOMBE IMEMTAKA MKUU WA WILAYA YA BUKOMBE AMAN MWENEGOHA KUFIKA MAHAKAMANI MACHI 14.


Taasisi  ya kuzuia na kupambana na rushwa(TAKUKURU) wilayani Bukombe imemtaka mkuu wa wilaya ya  bukombe mkoani Geita, Mh.aman Mwenegoha  kufika mahakamani  siku ya jumatatu machi 14,kwa  ajili ya kutoa ushahidi juu ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi umoja.

Mwenegoha amepewa wito huo wa mahakama ya wilaya wa kufika ili akatoe ushahidi dhidi ya mwalimu mkuu wa shule ya msingi umoja  iliyoko kata ya Katente mjini Ushirombo James  Nying’ati aliyekamatwa akipokea rushwa kutoka kwa mzazi Marco Elias ili ampatie nafasi mtoto  wake arudie darasa la saba.

Akizungumza na storm habari mkuu wa wilaya ya Bukombe, amesema kuwa amepata barua ya mahakama na yupo tayari kwa ajili ya kwenda kutoa ushahidi juu ya kile ambacho aliweza kukiona kwa mwalimu huyo.

Kamanda  wa takukuru wilaya ya Bukombe, Chuzera Shija amethibitisha kuwa  ni kweli mahakama imempelekea mkuu wa wilaya hati ya wito(samansi) ili afike mahakama ya wilaya akatoe ushahidi ikiwa ni  kwa  mujibu  wa taratibu,sheria na kanuni ili mahakama iweze kupata ushahidi  wa kujiridhisha na kisha itoe hukumu ya haki.


Hivi karibuni mwezi februari TAKUKURU  iliweka mtego na kuweza kumkamata mwalimu huyo mkuu wa shule ya msingi umoja James Nying’ati aliyeomba rushwa toka kwa mzazi ili ampatie msaada wa mwanaye kurudia darasa la saba.Shija ameionya jamii  iache kabisa tabia za kutoa, kuomba  ama kupokea rushwa ya aina yoyote.

No comments:

Post a Comment