Tuesday 8 March 2016

WAKULIMA 70 WA ZAO LA PAMBA MKOANI GEITA WAKUMBANA NA CHANGAMOTO.


Wakulima zao la pamba wapatao 70 waliolima na kupanda pamba eneo linalokadiliwa ekari 250 wilayani Mbogwe mkoani Geita wamepata changamoto ya kupata viuatilifu vya zao hilo kutokana na taarifa zao kutokuwepo ofisi za vijiji vyao  na  idara  ya  kilimo.


Hali hiyo imejitokeza kutokana na wakulima hao kupata mbegu za pamba kutoka vyanzo vingine tofauti na huduma ya ugawaji ya  pembejeo za pamba iliyokuwa inatolewa na umoja wa makampuni ya kuchambua pamba umwapa.

Wakulima hao wameiomba serikali kupitia idara ya kilimo  na bodi ya pamba iwasaidie ili kuwashawishi UMWAPA wawaingize kwenye orodha ya daftari la kilimo cha mkataba ili wapatiwe huduma hiyo muhimu.

Steven Shilemba kaimu afisa kilimo wilayani Mbogwe amethibitisha kuwepo kwa wakulima hao 70 ambao wamepata changamoto ya kutopata  viuatirifu  kwa wakati.

Wakulima hao wamepata mbegu za pamba kwa kununua sehemu zingine na wengine kutumia mbegu iliyokuwa imebaki msimu uliopita  kutokana na tatizo la mbegu zilizoanza  kusambazwa na UMWAPA  kuwa na uotaji hafifu.

Aidha shilemba amewataka wakulima hao wavute subira kwani serikali  kupitia idara yake ya kilimo na bodi ya pamba wanaendelea kupata idadi halisi ya wakulima wenye uhitaji huo ili UMWAPA wawape viuatilifu hivyo.

Afisa huyo amethibitisha tayari wakulima waliokosa wameanza kupelekewa viuatilifu ili kudhibiti wadudu  wa  zao la pamba.

Shilemba amesema, kuwa kwa msimu huu wa kilimo wilaya ya mbogwe ina wakulima waliolima pamba wapatao elfu nane miatano na  3 ambao wamelima jumla ya hekta zinazokadiriwa kufikia elfu 12, au ekari elfu 30, sawa asilimia 64 ya utekelezaji wa kulima hekta elfu 18, 819.  

Makampuni yanayounda UMWAPA ni 1.Kahama oil mills ltd (kom) ,2.Nida textile co ltd ,3.Fresho investment co ltd ,4.Kahama cotton company ltd (kccl) ,5.S.m holdings na 6.Birchand co ltd.



No comments:

Post a Comment