Saturday 26 March 2016

SERIKALI MKOANI GEITA YAJIPANGA KUKABILIANA NA WATUMISHI HEWA

Mkuu wa mkoa wa Geita meja jenerali mstaafu Ezekiel Kyunga
Serikali mkoani Geita, imejipanga vya kutosha kuhakikisha  kuwa inakabiliana na  watumishi hewa,ambapo ni agizo la raisi mh Jonh Magufuli la kuzitaka kila halmashauri nchini kushughulikia  tatizo  la watumishi  hewa.


Akizungumza na waandishi wa habari,ofisini kwake mkuu wa mkoa wa Geita,meja generali mstaafu Ezekile Kyunga,amesema kuwa uhakiki wa watumishi unaendelea na kwamba wanafanya kikao cha kupitia kila ripoti iliyoandaliwa na kila wilaya wakiwa na wakurugenzi wa halmshauri  ili kuweza kujiridhisha  juu  ya ripoti zao.


Aidha mkuu wa mkoa katika kuhakikisha kuwa ulinzi na usalama wa mkoa unaimarishwa wamekwisha kuanza kuchukua hatua za awali kwa kuagiza kila wilaya,vijiji,vitongoji,kata na mitaa,  mabalozi  wa nyumba 10  wanatumika kikamilifu kwa kuhakikisha wanawafatilia wageni wote wanaoingia katika maeneo wanayoyaongoza.


Aidha mh,Kyunga ameagiza pia kwa kila mtu na kwa kila shirika kuhakikisha kuwa wanapeleka silaha katika vituo vya polisi vilivyopo karibu kwa ajili ya kuhakiki kwani mwisho wa zoezi hilo ni mwezi juni  lengo ni kujua matumizi  bora  ya  silaha.


No comments:

Post a Comment