Tuesday 15 March 2016

WAKAZI WA LUDETE MKOANI GEITA WAMELALAMIKIA KURUDISHWA KWA KIONGOZI WA SERIKALI YA MTAA BW.ALIPHONCE MASALAKULANGWA.


Wakazi wa mtaa wa stooni kata ya Ludete wilaya na mkoani Geita wamelalamikia suala la kutaka kurudishwa kwa kiongozi wa serikali ya mtaa Bw.Aliphonce Masalakulangwa aliekataliwa na wananchi kwa madai ya kukosa sifa ikiwa ni pamoja na kutumia madaraka vibaya katika kipindi cha uongozi wake.

Wakizungumza na storm habari wananchi hao wamedai kuwa hawamuhitaji kiongozi huyo arudi katika uongozi huo kwani hata mwanzo amewahi kukataliwa kutokana na utendaji wake kuwa mbovu.
Storm habari imemtafuta Bw.Alphonce Masalakulangwa ili kuzungumzia jambo hilo ambapo hakutaka kuzungumza  kwa madai ya kwamba hakuwa na maandalizi.

Kwa upande wake kaimu mwenyekiti wa mtaa huo Bw.Ramadhani Mapera amekiri kuwepo kwa tatizo hilo mtaani hapo huku akidai kuwa uongozi huo aliupata baada ya mwenyekiti aliyekuwepo kukataliwa na wananchi na kwamba anashangazwa na hatua ya mtendaji wa kata hiyo kutengua uamuzi huo.


Aidha storm habari ilifanya jitihada za kuwatafuta Afisa mtendaji wa kata hiyo Bi.Josephina Mgaya pamoja na diwani wake lakini jitihada hizo ziligonga mwamba kwani  hawakutaka kuzungumza wakidai kuwa na majukumu mengi.

No comments:

Post a Comment