
Mtoto wenye umri wa miaka 11
anaetambulika kwa jina la Emmanuel Metusela
mkazi wa mji mdogo wa Katoro wilayani na mkoani Geita ameshikiliwa na jeshi
la jadi (sungusungu) kwa kukutwa na noti bandia shilingi elfu kumi.
Tukio hilo limetokea jana mtaa wa stooni katika mamlaka ya mji mdogo wa katoro ambapo
mtoto huyo amekamatwa na noti bandia pindi alipo kuwa akijaribu kwenda kununua
vocha katika duka lililopo mtaani hapo.
Akizungumza mtoto huyo amesema kuwa
hela hiyo alipewa na mtu ambae hamfahamu akamchukulie vocha dukani pasipo kujua
kama ni noti bandia ndipo alipo kamatwa na mwenye duka na kuambiwa kuwa noti
hiyo ni bandia.
Kwa upande wake Bw.Moses Nganikie
mmiliki wa duka ambalo tukio hilo limetokea amesema kuwa kijana huyo alikuja
mara ya kwanza akiwa na noti ya elfu kumi akanunua vocha ya elfu moja kisha
akaondoka baada ya kijana yule kuondoka
ndipo alipo chukua noti ile ya shilingi elfu kumi kwa lengo la kuchukua
sigara kwa jirani yake ndipo walipo gundua kuwa noti ile ni bandia baada ya
muda mfupi mtoto yule akarudi tena na noti nyingine ndipo walipo shituka na
kumkamata.
Aidha kamanda mkuu wa jeshi la jadi (sungusungu) wa
mtaa huo Bw. Marchades Gervas alithibitishwa
kukamatwa kwa mtoto huyo ambapo uchunguzi zaidi unaendelea kubaini kiini
cha tukio hilo.
No comments:
Post a Comment