Friday 18 March 2016

WAZIRI WA KILIMO,MIFUGO NA UVUVI AWATAKA WATANZANIA KUDUMISHA DEMOKRASIA NCHINI.

Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba.

Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba amewataka  watanzania kutambua kuwa hakuna chama cha siasa ambacho kinaweza kuthaminishwa na maisha ya mwanadamu  na kwamba wananchi hawana sababu ya kuendelea kupigana na kutoana uhai kwa sababu ya ushabiki wa vyama.


Hayo  ameyasema   katika mkutano   wa hadhara uliyofanyika katika viwanja vya Mnadani katika mji mdogo wa Katoro wilayani na mkoani Geita.

Amesema  kuwa hivi karibuni kumekuwepo na matukio ya mauaji yayohusishwa na mambo ya siasa mkoani hapa na Tunduma ambapo raia walipoteza  maisha kwa sababu   ya  tofauti   za kisiasa.

Aidha  ametaka wafasi wa vyama kutambua kuwa wale wote   ambao wamekuwa wakipigana  ni vyema wakajua kuwa hakuna hata mmoja  ambae   anaingia bungeni kwani wabunge wa vyama pinzani na vyama tawala   wamekuwa   ni kitu kimoja  pindi wanapokuwa bungeni  na nje ya bunge.

Ameongeza kuwa wananchi wanapaswa kutambua kuwa mfumo wa vyama vingi nchini haukuletwa kwa lengo la kuondoa amani ya nchi bali ni kudumisha demokrasia.



No comments:

Post a Comment