Wednesday 2 March 2016

MKURUGENZI MKUU WA EWURA, BW.FELIX NGAMLAGOSI ATANGAZA BEI ELEKEZI YA MAFUTA NCHINI.



Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhibiti wa huduma ya nishati na maji(EWURA), Felix Ngamlagosi.

Bei ya nishati ya mafuta imeendelea kushuka baada ya mamlaka ya udhibiti wa huduma za nishati na maji Ewura kutangaza bei kikomo.


Akitangaza bei elekezi ya mafuta hayo jijini dar es salaam  itakayoanza kutumika nchini kuanzia leo tarehe 02 march  mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya udhitibiti wa nishati na  maji (EWURA) Bw.Felix Ngamlagosi amesema bei ya petroli imeshuka kwa sh. 31, dizeli sh 114 na mafuta ya taa yameshuka kwa sh, 234.

Amewataka wateja wa nishati ya mafuta kudai risiti pindi wanapopewa huduma hiyo na kwamba kuanzia sasa wananchi wanaweza kupata bei hizo kupitia simu zao za kiganjani.

Aidha ameongeza kuwa hakutakuwa na mabadiliko ya bei ya mafuta ya petroli na dizeli kwa mkoa wa tanga kwa mwezi marchi kutokana na kutopokelewa kwa mafuta mapya kupitia bandari ya tanga mwezi februari mwaka huu.

No comments:

Post a Comment