Friday 8 June 2018

HOFU, KUTOJIAMINI ZAPELEKEA UPOTEVU WA HAKI KWA WANAWAKE GEITA


Baadhi ya wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa mwanamke wakiwa kwenye kikao cha pamoja kilichokuwa kimelenga kujadili sera na sheria ya ukatili dhidi ya Mwanamke kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa la Anglikana Mjini Geita.


Wadau wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mwanasheria wa shirika lisilo la kiserikali la Woman promotion center.


Mwanasheria wa shirika lisilo la kiserikali la Woman Promotion Center ,Bi, Walta Caros akizungumza na waandishi wa habari juu ya sheria ya vitendo vya kikatili kwa mwanamke.

VYUO 20 VYAFUTIWA USAJILI NA BARAZA LA TAIFA LA ELIMU YA UFUNDI (NACTE)




Leo June 8, 2018 Baraza la Taifa la Elimu ya Ufundi (NACTE) limefuta usajili wa vyuo 20 kwa kushindwa kufuata utaratibu wa usajili wa vyuo vya ufundi na upungufu wa Rasilimali za kufundishia

MFUMUKO WA BEI NCHINI WAENDELEA KUPUNGUA TOKA 3.8% HADI 3.6%


Mkurugenzi wa Sensa ya Watu na Takwimu za Jamii kutoka Ofisi ya Taifa ya Takwimu (NBS), Ephraim Kwesigabo akifafanua jambo alipokuwa akizungumza na waandishi wa habari(hawapo pichani) kuhusu mfumko wa bei wa Taifa leo Jijini Dar es Salaam, Mfumuko wa bei umeshuka toka asilimia 3.8 mwezi Aprili hadi kufikia 3.6 Mei. Kushoto ni Meneja wa Ajira na Bei toka NBS, Ruth Minja. 

Thursday 7 June 2018

PM MAJALIWA - TUNA KAZI KUBWA YA KUELIMISHA JAMII KUHUSU FISTULA


Makamu wa Rais, Samia Suluhu Hassan amesema bado kuna kazi kubwa kuhakikisha jamii inafikishiwa ujumbe kuhusu tatizo la fistula na athari zake kwa afya ya mama na uchumi kwa ujumla.
Mama Samia amesema hayo leo Alhamisi Juni 7, alipozungumza katika Viwanja vya Hospitali ya CCBRT ambako alifanya ziara kujionea huduma mbalimbali zinazotolewa hospitalini hapo.

MKUU WA MAJESHI AHAMASISHA VIJANA KUJIUNGA NA JKT


Mkuu wa Majeshi ya Ulinzi  Jenerali Venance Mabeyo amewahamasisha vijana kujiunga na Jeshi la Kujenga Taifa ili waweze kupata stadi za ufundi na hatimaye wajiajiri badala ya kutegemea kuajiriwa na Serikali.

Tuesday 5 June 2018

MAKAMU WA RAIS ASHIRIKI KATIKA UZINDUZI WA UKUTA JIJINI DSM


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akisisitiza jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Katibu Mkuu Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, Mhandisi Joseph Malongo akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Mwakilishi Mkazi wa Shirika la Maendeleo la Umoja wa Mataifa, Alvaro Rodriguez akizungumza na wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano na Mazingira, January Makamba, akifafanua jambo kwa wananchi (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Baadhi ya waandishi wa habari wakiendelea na majukumu yao wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akikagua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam mara baada ya kuuzindua mapema hii leo, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Sehemu ya kupumzika iliyojengwa katika ukuta wa ufukwe wa bahari ya Hindi uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Msanii Beka Fleva akitoa burudani kwa wananchi wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Baadhi ya wananchi wakimsikiliza Makamu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan,(hayupo pichani) wakati wa sherehe za uzinduzi wa ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi.


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, akiwapungia wananchi mara baada ya kuzindua ukuta wa ufukwe wa bahari uliojengwa kando ya barabara ya Barack Obama jijini Dar es Salaam, ukuta huo umejengwa kwa ufadhili wa mfuko wa Dunia wa kuhimili mabadiliko ya tabianchi. Picha na Eliphace Marwa 

KINARA WA UTEKAJI AUWAWA MKOANI GEITA



Mtu mmoja anayejulikana kwa majina ya Panda Kinasa mwenye miaka 36 anayetuhumiwa kuwa kinara wa utekaji  watu ameuwawa kwa kupigwa na risasi makalioni wakati akijaribu kuwatoroka polisi baada ya kuwapeleka kwenye mashimo alikokuwa ametupa miili ya watu wawili wilayani Bukombe Mkoani Geita.

Monday 4 June 2018

RAIS MAGUFULI AZINDUA AWAMU YA PILI YA PROGRAMU YA KUENDELEZA KILIMO NCHINI



 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akikata utepe kuashiria kuzindua rasmi Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018. Anayemshikia kitabu hicho ya Programu ni Waziri wa Kilimo Dkt. Charles Tizeba.

  
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Rais Mstaafu wa Awamu ya Pili Alhaji Ali Hassa Mwinyi nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kuizindua katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi  Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji Mhe. Mahamoud Hassan Mgimwa nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kuizindua katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.  


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Makamu Mkuu wa Chuo Kikuu cha Kilimo cha Sokoine (SUA) Profesa Raphael Tihela Chibunda nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kukabidhiwa  katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.  


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimkabidhi Mwenyekiti wa Taasisi za Sekta Binafsi (TPSF) Dkt. Reginald mengi  nakala ya kitabu cha  Awamu ya Pili ya Programu ya Kuendeleza Kilimo (ASDP ll) baada ya kukabidhiwa  katika ukumbi wa mikutano wa Mwalimu Julis Nyerere jijini Dar es salaam leo Juni 4, 2018.  

RAIS MAGUFULI AWAAPISHA MAJAJI WATATU LEO IKULU JIJINI DAR ES SALAAM


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Ferdinand Wambali kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko kuwa Jaji wa Mahakama ya Rufani, Ikulu jijini Dar es Salaam.


 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimuapisha Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi  kuwa Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu ya Tanzania.

 
Majaji watatu walioapishwa wakila Kiapo cha Maadili Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kulia ni Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Ferdinand Wambali akifatiwa na Jaji Mwanaisha Athuman pamoja na Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi  

 
Majaji pamoja na watendaji wa Mahakama Kuu pamoja na Mahakama ya Rufani wakifatilia tukio la uapisho wa Majaji watatu Ikulu jijini Dar es Salaam.

  
Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Ferdinand Wambali akizungumza mara baada ya kuapishwa na Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli Ikulu jijini Dar es Salaam.

 
Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa katika picha ya pamoja na Majaji watatu aliowaapisha Ikulu jijini Dar es Salaam. Wa kwanza kushoto ni Jaji Kiongozi wa Mahakama Kuu Jaji Dkt. Eliezer Mbuki Feleshi, Jaji wa Mahakama ya Rufani Jaji Ferdinand Wambali pamoja na Jaji Jaji Mwanaisha Athuman Kwariko mara baada ya tukio la uapisho Ikulu jijini Dar es Salaam. 

WANANCHI WA NYAKAGWE WAIOMBA SERIKALI KUWATENGENEZEA DARAJA


Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nyakagwe wakivuka Mto kwa kuvua viatu kutokana na kukosekana kwa daraja kwenye eneo hilo.


Mwananchi akivusha usafiri kwenye eneo la Mto ambao unapita kijijini Hapo.


Mkuu wa wilaya ya Geita, Mwl Herman Kapufi akiwa na baadhi ya wajumbe wa chama cha mapinduzi (CCM)wakitazama namna ambavyo tatizo hilo lilivyo.

Mkuu wa wilaya ya Geita, Mwl Herman Kapufi akizungumza juu ya mikakati ya kuwasaidia wananchi na tatizo la kukosekana kwa Daraja .

Friday 1 June 2018

PM MAJALIWA ATEMBELEA KIWANDA CHANGUO CHA URAFIKI NA KUKUTA MADUDUDU

 

Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akizungumza na wafanyakazi na viongozi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam baada ya kukagua kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kushoto ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Charles Mwijage na kulia ni Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam na Mkuu wa Mkoa wa Pwani, Mhandisi, Evarest Ndikilo.


Baadhi ya wafanyakazi wa kiwanda cha nguo cha Urafiki wakimshangilia Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa wakati  alipozungumza nao kiwandani hapo, Juni1, 2018.


 
Waziri Mkuu ,Kassim Majaliwa  akipata maelezo kutoka kwa Kaimu Mhandisi Mkuu wa kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam, Khamis Mazugo (kushoto)  kuhusu mitambo ya kiwanda hicho iliyokoma kufanya kazi wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana.




Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipita katika eneo zilipong'olewa mashine za kiwanda cha nguo cha Urafiki cha jijini Dar es salaam wakati alipotembelea kiwanda hicho Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana

 
Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa akipata maelezo kutoka kwa Naibu Meneja Mkuu wa kiwanda cha nguo cha Urafiki, Shadrack Nkelebe kuhusu mashine za kutengeneza  nyuzi za pamba wakati alipokitembelea kiwanda hicho, Juni 1, 2018. Kiwanda hicho kimesimamisha uzalishaji tangu Desemba mwaka jana. 

WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI AZINDUA WIKI YA MAZIWA NCHINI,AAHIDI KUINUA SEKTA HIYO


Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina(wa pili kulia) akikata utepe kuzindua Wiki ya Maziwa kitaifa kwenye uwanja maonesho ya Kilimo na Mifugo Nanenane Njiro,kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na viongozi wa Baraza la Kilimo nchini na Bodi ya Maziwa.


Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina akitoa hotuba yake kwenye uzinduzi wa Wiki ya Maziwa kitaifa kwenye uwanja maonesho ya Kilimo na Mifugo Nanenane Njiro jijini Arusha. 


Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina akiwapa wanafunzi wa Shule ya Msingi Baraa ya jijini Arusha baada ya kuzindua Wiki ya Maziwa kitaifa kwenye uwanja maonesho ya Kilimo na Mifugo Nanenane Njiro,kulia kwake ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo. 


Meneja wa kampuni ya Milkcom maafuru Dar Fresh,Tunnu Mssika akimpa maelezo Waziri wa Mifugo na Uvuvi wakati akikagua mabanda ya waoneshaji bidhaa mbalimbali zinazotokana na mifugo. 


Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina(katikati) akipewa maelezo na Mjasiriamali wa kampuni ya Mpilika Leather kutoka Dodoma,Anna Malongo ,kushoto ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo . 


Wananchi waliohudhuria maadhimisho ya Wiki ya Maziwa kitaifa mkoa wa Arusha wakifatilia kwa makini hotuba za viongozi. 



Waziri wa Mifugo na Uvuvi,Luhaga Mpina(kushoto) akizungumza jambo na Mwenyekiti wa Baraza la Wakulima nchini(ACT),Dk Sinare Sinare(kulia)kwenye uwanja maonesho ya Kilimo na Mifugo Nanenane Njiro,wa pili kulia ni Mkuu wa mkoa wa Arusha,Mrisho Gambo na Kaimu Mwenyekiti wa Bodi ya Maziwa,Lucas Malunde.