Tuesday 22 March 2016

TAREHE 22 MARCH DUNIANI KOTE WATU HUADHIMISHA SIKU YA MAJI.






Leo ni siku ya maji duniani inayoadhimishwa kila siku ya tarehe 22 mwezi wa tatu kila mwaka duniani, Katika siku ya leo kauli mbiu ikiwa ni KUPUNGUZA IDADI YA VIFO VITOKANAVYO NA UPUNGUFU WA MAJI MWILINI KWA KUHAKIKISHA MATUMIZI YA MAJI SAFI NA SALAMA.



Shirika la afya duniani(WHO) limetoa ripoti kuwa katika kila dakika mbili mtoto mmoja hukabiliwa na athari ya kufariki dunia kutokana na kunywa maji machafu pia katika hatua nyingine asilimia 10 ya watu duniani hawapati maji safi ya kunywa na kwa msingi huo  wanakabiliwa na hatari ya maradhi ya tumbo na kufariki dunia.


Wakatib huo huo pia shirika la watoto duniani(UNICEF) limetahadharisha kutokuwepo maendeleo ya kutoshakatika suala la kudhibiti maji taka inapelekea maisha ya watoto yakabiliwe moja kwa moja na hatari kubwa na kupoteza maisha.

No comments:

Post a Comment