Thursday 29 December 2016

MKUU WA MKOA WA GEITA AZINDUA ZOEZI LA UGAWAJI WA VITAMBULISHO MKOANI HUMO




Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga akikabidhi vitambulisho vya watumishi kwa mwakilishi kutoka wilaya ya Mbongwe Bw,Paul Cheyo wakati wa zoezi la uzinduzi wa vitambulisho vya Taifa Mkoani Geita.




Mkuu wa Mkoa wa Geita ,Meja jenerali Mstaafu Ezekiel Kyunga,akionesha kitambulisho chake baada ya kukabidhiwa.

RAIS MAGUFULI ASHIRIKI MSIBA WA MZEE MAARUFU WA CHATO ADMIRABILIS MBABE MANYAMA (82) CHATO MKOANI GEITA



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli leo tarehe 29 Desemba, 2016 ameungana na wananchi wenzake Wilayani Chato mkoani Geita kutoa pole kutokana na kifo cha Mzee Admirabilis Mbabe Manyama ambaye ni mzee maarufu wilayani hapa na Mzee James Lufunga Mchele ambaye ni jirani yake.

Friday 23 December 2016

SUMATRA YAUNDA KIKOSI KAZI KUDHIBITI UPANDISHAJI HOLELA WA NAULI KIPINDI CHA SIKUKUU ZA MWISHO WA MWAKA



Mamlaka ya Usimamizi wa Usafiri wa Majini na Nchi Kavu (SUMATRA) imeunda kikosi kazi maalum kwa ajili ya kudhibiti upandashaji holela wa  nauli kwa mabasi yaendayo mikoani wakati wa kipindi hiki cha sikukuu za mwisho wa mwaka.

Thursday 22 December 2016

SERIKALI YASIMAMISHA SHUGHULI ZA MFUKO WA UENDELEZAJI WA ZAO LA KOROSHO



Serikali imesimamisha shughuli za Mfuko wa Wakfu wa Kuendeleza Zao la Korosho ili kupisha uchunguzi wa matumizi ya fedha za mfuko huo.

Tuesday 20 December 2016

KIWANGO CHA PESA KESI ZA MAFISADI KUSHUSHWA CHINI ILI KUWABANA WENGI



Waziri wa Katiba na Sheria, Dk Harrison Mwakyembe amesema serikali inatarajia kujadili kushusha kiwango cha fedha kinachohusika katika makosa ya rushwa na uhujumu uchumi kwenye mahakama ya mafisadi ili kukomesha vitendo vya rushwa.

WAZIRI MWIGULU NCHEMBA KUFUTA TAASISI ZINAZOHAMASISHA VITENDO VYA USHOGA






































Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mwigulu Nchemba ametaka apewe taarifa kuhusu taasisi na mashirika yasiyo ya kiserikali (NGO) wanaohamasisha au kutangaza ndoa za jinsia moja nchini ili azifutie usajili mara moja.

Saturday 17 December 2016

PICHA: NAPE AFUNGUA MASHINDANO YA MICHEZO MBALIMBALI WILAYANI KARATU



Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akipiga baruti juu kuashiria ufunguzi rasmi wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu (Karatu Sports Festival).



Wanariadha wanaoshiriki mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu wakijandaa kuanza kukimbia wakati wa uzinduzi wa mashindano hayo uliofanywa na Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye Disemba 17/2016.





Waziri wa Habari Utamaduni Sanaa na Michezo Mhe. Nape Moses Nnauye akisalimkia na baadhi ya washiriki wa mashindano ya michezo mbalimbali yanayofanyika Wilayani Karatu.

Friday 16 December 2016

Thursday 15 December 2016

HUMPHREY POLEPOLE AELEZA MIKAKATI YAKE BAADA YA KUKABIDHIWA OFISI NA NAPE NNAUYE



Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Chama cha Mapinduzi (CCM) Humphrey Polepole amesema atahakikisha chama hicho kinakuwa ni cha wanyonge na kuendelea kuwa kimbilio la wasio na sauti.

DALADALA DODOMA ZAGOMA KUPINGA MANYANYASO



Zaidi ya mabasi 70 ya daladala yanayosafirisha abiria katika baadhi ya njia za manispaa ya Dodoma, yamegoma kutoa huduma kwa siku nzima ya leo kutokana na madai ya kunyanyaswa na askari wa usalama barabarani.

Wednesday 14 December 2016

NAIBU WAZIRI MAVUNDE APOKEA TUZO ALIYOSHINDA MJASIRIAMALI JENIFA SHIGOLE



Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akizungumza na vyombo vya habari kuhusu Tuzo aliyoshinda Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole katika tuzo za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.



Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akipokea cheti  alichoshinda Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole katika tuzo za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.



Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akipokea Tuzo kutoka kwa Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole aliyoshinda katika tuzo za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.



Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole Bi. Jenifer Shigole akiwaonyesha waandishi wa habari(hawapo pichani) tuzo aliyoshinda nchini Morocco na kufanikiwa kushika nafasi ya kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola moja na nusu. Kushoto ni Meneja wa Programu wa kampuni ya Malkia Investment Bw.Juma Rajabu.



Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi,Vijana na Ajira Mhe.Anthony Mavunde akipokea Tuzo kutoka kwa Mjasiriamali na Mkurugenzi wa kampuni ya Malkia Investment ltd Bi. Jenifer Shigole aliyoshinda katika tuzo za  za African entrepreneurship Awards zilizofanyika nchini Morocco na kuibuka mshindi wa kwanza katika kipengele cha masuala ya Elimu na Mazingira na kujishindia mtaji wa dola laki moja na nusu.Kulia ni Mkurugenzi Msaidizi Maendeleo ya Vijana Bi.Venerose Mtenga na wa kwanza kushoto ni Meneja wa Programu wa kampuni ya Malkia Investment Bw.Juma Rajabu.

Tuesday 13 December 2016

SERIKALI YA CHINA KUJENGA KIWANJA CHA KISASA CHALINZE



Serikali ya China imetoa ufadhili wa ujenzi wa uwanja wa Michezo kwa shule ya msingi Msoga iliyopo halmashauri ya wilaya ya Chalinze.

PICHA: KAMPUNI MBALIMBALI ZILIVYOSHIRIKI MAONYESHO YA VIWANDA JIJINI DSM



Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Dkt. Adelhelm Meru akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurgenzi Mtendaji wa Wakala wa Vyuo vya Nje ya Nchi (GEL) Bw. Abdulmalik Mollel (kulia) alipotembelea banda la Wakala hiyo katika maonesho ya Viwanda vya Tanzania jana Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Wakala wa Maendeleo ya Biashara Tanzania (TANTARDE) Bw. Edwin Rutageruka


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Dkt. Adelhelm Meru akisikiliza maelezo kutoka kwa Kaimu Meneja wa Mamlaka ya Chakula na Dawa Tanzania (TFDA) Bw. James Ndege (watatu kutoka kushoto) alipotembelea maonesho ya Viwanda vya Tanzania yaliyomalizika jana katika viwanja vya Mwl. Nyerere (sabasaba) Jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Afisa Habari na Elimu kwa Umma wa Mamlaka hiyo Bi. Roberta Ferouz.





























Baadhi ya wananchi wakipata huduma katika banda la Mfuko wa Pensheni kwa Watumishi wa Umma (PSPF) walipotembelea maonesho ya Viwanda vya Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.




Afisa Masoko wa Shirika la Kuthibiti Viwango Tanzania (TBS) Bi. Rhoda Mayugu akitoa maelezo kwa wananchi waliotembelea banda lao katika maonesho ya Viwanda vya Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Dkt. Adelhelm Meru akiangalia namna mashine ya kufyatulia matofali inavyofanya kazi alipotembelea mmoja ya banda katika maonseho ya Viwanda vya Tanzania jana Jijini Dar es Salaam.



KAHAMA OIL MILLS LIMITED YATOA AJIRA KWA WATU 600



Meneja Utawala na Uzalishaji wa Kampuni  ya Kahama Oil Mills Bw. Bryason Edward akipokea cheti cha ushiriki wa maonesho ya kwanza ya viwanda vya Tanzania kutoka kwa Katibu Mkuu waWizara ya Viwanda, Biashara na Uwezeshaji Dkt. Adelhelm Meru wakati wa hafla  ya kufunga maonesho hayo jana  jijini  Dar es Salaam.




Meneja Utawala na Uzalishaji wa Kampuni  ya Kahama Oil Mills Bw. Bryason Edward akishiriki hafla ya kufunga maonesho  ya kwanza  ya viwanda vya Tanzania yalio malizika katika viwanja vyaMwl. Nyerere (sabasaba) jana jijini Dar es Salaam.




Katibu Mkuu wa Wizara  ya Viwanda,  Biashara na Uwezeshaji Dkt. Adelhelm Meru akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja Utawala na Uzalishaji wa Kampuni ya Kahama Oil Mills Bw. Bryason Edward alipotembelea maonesho ya Viwanda vya Tanzania  jana Jijini Dar es Salaam . Kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Mamlaka ya Maendeleo  ya Biashara Tanzania (TANTARDE) Bw. Edwin  Rutageruka.

Monday 12 December 2016

SALAAM ZA LOWASSA KATIKA SIKUKUU YA MAULID



Nachukua nafasi hii kuwatakia kheri na baraka waislam wote nchini katika kuadhimisha siku hii ya kuzaliwa kwa kiongozi wao Mtume Muhammad SAW.

Waislam kama walivyo watanzania wa dini nyingine wamekuwa nguzo muhimu katika kujenga amani, upendo na utulivu nchini kwetu, na hii yote ni kutokana na mafundisho ya kiongozi wao huyo.

Ni rai yangu kwa watanzania wote wakiwemo watawala kuwa tunapo sherehekea siku hii tutimize kwa vitendo mafundisho ya bwana Mtume ambaye ni mmoja wa mitume wa mwenyezi mungu kwa kuheshimiana, kuvumiliana na kupendana.

Edward Lowassa

Waziri mkuu Mstaafu na Mjumbe wa Kamati Kuu - Chadema.

MAKAMU WA RAIS SAMIA SULUHU MGENI RASMI UZINDUZI WA MPANGO WA KUZUIA UNYAYASAJI KIJINSIA



Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan anatarajia kuwa mgeni rasmi katika  uzinduzi wa Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano (2017-22) wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto.

Thursday 8 December 2016