Thursday 17 March 2016

WANANCHI MKOANI GEITA WATAKIWA KUJITOKEZA KUPIMA MAGOJWA YA KIFUA KIKUU NA VIRUSI VYA UKIMWI.

Wananchi  mkoani Geita wametakiwa kujitokeza kwa wingi kupima magojwa ya kifua kikuu pamoja na virusi vya ukimwi ili waweze kutambua  afya zao.


Hayo yamesema na mratibu wa mradi wa Challenge TB  mkoani Geita Bw. Patriki Magassa  kutoka katika shirika la KNCV lenye makao makuu yake jijini Dar es salaam, kwa kushirikiana na wizara ya afya mandeleo ya jamii jinsia,wazee na watoto  kupitia mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma nchini,huku akidai lengo la mradi huo ni kuibua wagonjwa wengi wasiokuwa na mazoea  ya kupima pindi wanapokuwa na dalili za magonjwa hayo.

Ameongeza kuwa baadhi ya wagonjwa wanapogundulika kuwa na magonjwa hayo wamekuwa wakigoma kutumia dawa na wengine kutoroka  hali ambayo imekuwa ni changamoto kwa watoa huduma.


Aidha Magasa amewaomba wanachi wa mkoa wa Geita kutumia nafasi hiyo kwani mpango huo utazunguka katika maeneo yote na kwamba mkoani hapa umeanza na vijiji vya Nyakabale na Mgusu.

No comments:

Post a Comment