Friday 11 March 2016

WANANCHI WA KATA YA MGUSU MKOANI GEITA WAMEIOMBA SERIKALI KUFUNGUA MGODI ULIOFUNGWA BAADA YA KUTOKEA VIFO VYA WACHIMBAJI 5.


 Naibu waziri wa Nishati na Madini Dkt.Medard Kalemani akizungumza na baadhi ya wananchi waliofika eneo la tukio.

Mkuu wa mkoa wa Geita Bi. Fatuma Mwasa akizungumza na wananchi waliohudhuria eneo la tukio.


  Mkuu wa mkoa wa Geita  Bi.Fatuma Mwasa


 Baadhi ya wananchi waliohudhuria eneo la tukio.


Wananchi wa kata ya mgusu iliyopo  mkoani Geita wameiomba  Serikali kuwafungulia mgodi uliofungwa baada ya kutokea vifo vya wachimbaji 5 na wengine kujeruhiwa  ili kuendeleza shughuli za uchimbaji ambao unawaendeshea maisha.


Hayo wameyasema wakati  walipokuwa wakizukungumza na mkuu wa mkoa wa Geita  Fatuma Mwasa kwenye mkutano uliofanyika katika maeneo ya machimbo hayo na kueleza jisi wanavyoathirika kwa kufungwa kwa mgodi huo.

Kaimu Afisa madini wa mkoani hapa  Bw.Fabian Lukas Mshai amewaomba wananchi kuzingatia  kanuni za uchimbaji ili kuepuka kukumbwa na maafa mengine.

Aidha mkuu wa mkoa Geita   Bi.Mwasa amewapa pole wananchi hao na kuwataka kumpa ushirikiano na kumuunga mkono ili kutokomeza vifo katika  mgodi  huo.


Marchi 9 majira ya saa tisa alasiri watu  watano walifariki  na wengine kujeruhiwa baada ya kuangukiwa na kifusi wakati walipokuwa  kwenye shughuli za uchimbaji.


No comments:

Post a Comment