Saturday 19 March 2016

WANANCHI WALILALAMIKIA JESHI LA POLISI MKOA WA GEITA.

 Kamanda mkuu wa jeshi la polisi mkoa wa geita Mponjoli Mwabulambo


Wananchi mkoani Geita wameiomba serikali kudhibiti vitendo vya rushwa  nchini  ambavyo vinapelekea  kukosa haki zao  za  msingi wanapohitaji kuzipata.


Wakizungumza na Storm habari baadhi ya wananchi hao ambao wamelishutumu jeshi  la  polisi kwa kuendelea kujihusisha na vitendo hivyo ambavyo vimeonekana kuwabana zaidi wananchi wenye kipato cha chini na kushindwa kupata haki zao.

Aidha kamanda wa polisi mkoa wa GeitaMponjoli  Lotson amekiri kuwepo kwa tuhuma hizo huku akiwataka wananchi kuonyesha ushirikiano hasa kwa vielelezo ili wanaojihusisha na  vitendo  hivyo wachukuliwe  hatua  za kisheria.

Kwa upande wake mkuu wa taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa (TAKUKURU) Bw.Thobias Ndaro ametoa wito kwa wananchi kutoa taarifa katika ngazi husika pindi yatokeapo matukio hayo hali itakayosaidia kuondoa tatizo hilo mkoani hapa.


No comments:

Post a Comment