Saturday 19 March 2016

RAIS MAGUFULI AFANYA UTEUZI WA WAKURUGENZI WAKUU WAPYA NSSF, TBC NA RAHCO.

Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli


Rais Magufuli amemteua Profesa Godius Kahyarara kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) ambapo uteuzi huo umefanyika kwa mujibu waSheria ya NSSF namba 28 ya Mwaka 1997, Kifungu cha 42, kinachoeleza kuwa Rais ndiye mwenye mamlaka ya kuteua Mkurugenzi Mkuu wa NSSF.

Prof. Kahyarara anachukuwa nafasi iliyoachwa wazi na Dkt. RamadhanDau, ambaye ameteuliwa kuwa Balozi.

Kwa upande mwingine Rais Magufuli amemteua Dkt. Ayub Rioba Chacha kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC) anaechukua nafasi ya Clement Mshana ambaye amestaafu hukupia Dkt. Mussa Iddi Mgwatu akiteuliwa kuwa Mkurugenzi Mkuu wa Kampuni hodhi ya rasilimali za reli Tanzania (RAHCO) anaechukua nafasi iliyoachwa wazi na Mhandisi Benhadard Tito, ambaye uteuzi wake ulitenguliwa.


No comments:

Post a Comment