Thursday 17 March 2016

SERIKALI IMEJIPANGA KUHAKIKISHA KUWA INATATUA TATIZO LA MBEGU ZA PAMBA NCHINI.


Waziri wa kilimo mifugo na uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba.


 Mwenyekiti wa chama cha mapinduzi  (CCM) mkoani Geita na mbunge wa Geita vijijini Mh.Joseph Msukuma.  

Serikali kupitia wizara ya kilimo mifugo na uvuvi imejipanga kuhakikisha kuwa inatatua tatizo la mbegu za pamba kwa kuhakikisha  inarudisha upatikanaji wa mbengu ambao ulikuwa umezoeleka kwa muda mrefu na kuachana na mfumo uliopo kwa hivi sasa.


Hayo yamesemwa na waziri wa kilimo mifugo na uvuvi, Mh.Mwigulu Nchemba wakati alipokuwa akizungumza na wananchi wa Katoro katika viwanja vya mnada wa ngombe.
Amesema kuwa wizara kwa sasa inaangalia utaratibu wa kurejesha upatikanaji wa mbengu ambao ulikuwa umezoeleka kwa hapo zamani ambao ulikuwa ukisababisha zao la pamba kufanya vizuri katika nchi.

Aidha kwa upande wake mwenyekiti wa chama cha mapinduzi  (CCM) mkoani hapa na mbunge wa geita vijijini Mh.Joseph Msukuma  amemtaka waziri wa kilimo kuhakikisha kuwa anashughulika na umwapa ambao ni wasambazaji wa mbegu za pamba kwa kuhakikisha kuwa wanaondolewa kwani mbengu ambazo wamekuwa wakizisambaza nyingi zimeonekana kuwa na shida katika kilimo cha pamba.

waziri mkuu Mh.Kassim Majaliwa  ameongezea kuwa ni vyema kwa bodi ya pamba kuhakikisha kuwa inatathimini zao la pamba na jinsi ambavyo limekuwa likishuka  thamani kila wakati na sababu zinazopelekea zao hilo kuwa na changamoto nyingi kwa wakulima.

Waziri mkuu amemaliza ziara yake  mkoani Geita kwa kutembelea baadhi ya maeneo na kuzungumza na wananchi mkoani hapa ikiwa ni pamoja na kuwasimamisha viongozi ambao wamekosa maadili katika kazi.

No comments:

Post a Comment