Monday 7 March 2016

KUELEKEA SIKU YA WANAWAKE DUNIANI ITAYOADHIMISHWA MARCH 08 2016.











Kampuni ya Trumark hapa Tanzania inaandaa Tamasha la Pamoja Tunafanikisha kusherekea Siku ya Wanawake duniani Machi 8, mwaka huu. katika Ukumbi wa King Solomoni, eneo la Namanga jijini Dar es salam. Siku hii muhimu itawakutanisha wanaume na wanawake wataungana kusherekea mafanikio ya wanawake.


Mkurugenzi wa Kampuni ya Trumark Bi Agnes Mgongo alisema kwa kutambua changamoto nyingi zinazomkabili mwanamke, katika kuadhimisha siku hiyo Trumark imekuwa ikiandaa shughuli za maadhimisho kwa kuwaalika wadau mbalimbali kutoka nyanja tofauti ili kujadiliana namna ya kuzikabili na kuzifanya kuwa fursa na pia kuwapongeza wanawake ambao wameonyesha njia kwa kujikwamua kiuchumi, kijamii na kiafya huku kauli mbiu ikiwa "50-50 MPAKA KUFIKIA 2030"

Trumark imekua ikiadhimisha siku ya wanawake kwa takribani miaka mitano sasa na tumekuwa na mafanikio makubwa kwani washiriki wengi wamekuwa na mrejesho chanya, nakuongeza mtandao katika shuguli zao mbalimbali.

Aliongeza Bi Agnes alisema hii inakuja ikiwa ni mwaka wa kwanza baada ya umoja wa Mataifa (United Nation) kuja na malengo mapya 17 ya maendeleo endelevu (SDGS) baada ya kuisha muda kwa malengo nane ya millennia yaliyowekwa na umoja huo mwaka 1990. Katika malengo haya mapya lengo namba 5 linataka kuleta usawa wa kijinsia na kuwawezesha wanawake na wasichana kila mahali.

Katika kuelekea maadhimisho ya siku ya mwanamke duniani, mwanamke wenyewe anayo fursa kubwa ya kujitathimi na kujitambua anahitaji nini katika maisha yake Alisisitiza kweli nguvu za pamoja zinahitajika ili kumwezesha mwanamke kutoka mahali aliko sasa, lakini hilo litafanikiwa zaidi ikiwa mwanamke naye atachukua hatua ya kujitoa kitanzini kwa kushirikiana na mwanaume.

Hivyo ni swala la jamii nzima kushiriki harakati hizi za kuleta usawa wa kijinsia. Alisema maadhimisho yataambatana na burudani kutoka kwa wasanii wa bendi ya mapacha watatu pamoja na chakula cha usiku katika kusheherekea mafanikio ya wanawake.

Agnes alifafanua kuwa wageni waalikwa watapata fursa ya kuhamasishw a maswala ya afya ikiwemo faida ya mazoezi ili kujenga afya bora na kuepukana magonjwa yale yasiyo ambukizwa lakini ni hatari kama kisukari, shinikizo la damu na uzito uliozidi (obesity).

Pia aliongeza katika siku hiyo kutakuwa na fursa kwa wafanyabiashara wanawake kujitangaza kwa kufanya maonyesho ya bidhaaa zao mbalimbali (exhibition) ili kujitangaza na kujiongezea wateja.

Aliwakaribisha wahisani na wadau mbalimbali wanaojihusisha na maswala mbalimbali ya Wanawake kujitokeza na kushiriki pamoja katika siku hii muhimu kwa jamii yetu. Pamoja wanaume na wananake Tunafanikisha mafanikio ya wanawake.

No comments:

Post a Comment