Wednesday 23 March 2016

MWANAFUNZI WA DARASA LA NNE SHULE YA MSINGI KALEMANI MKOANI GEITA AFANYIWA VITENDO VYA UBAKAJI KWA ZAIDI YA MIEZI MIWILI.


Mwanafunzi wa darasa la nne katika shule ya msingi kilimani iliyopo mji mdogo wa Katoro wilayani Geita mwenye umri wa miaka 11 amekuwa akifanyiwa kitendo cha ubakaji kwa zaidi ya miezi miwili na mwanaume mmoja aliyejulikana kwa jina moja la Joseph.

Amekuwa akirubuniwa na Joseph kwa madai ya kumuahidi kumuoa na kumhudumia huku akimlaghai kwa kumpa kiasi cha shilingi 1000 hali iliyosababisha mwanafunzi huyo kuacha kuhudhuria masomo
Mwanafunzi huyo ambaye amekuwa hafiki shule na alipoulizwa na baba yake mzazi alidai kuwa shule hawafundishwi na ndipo baba yake aliamua kufatilia kwa karibu na kugundua mtoto wake hahudhurii masomo.
Mmoja wa walimu wa shule ya msingi kalemani ajulikanaye kwa jina la Jumanne Misungwi alibainisha kupigiwa simu na baba mzazi na kulalamikiwa kutofundishwa kwa mtoto huyo na ndipo alimuomba mzazi huyo afike shuleni ili kutatua tatizo hilo sambamba na kupata ukweli.
Katika hatua nyingine mmoja wa walimu wakike ilibidi amchukue mwanafunzi huyo na kukaa nae chini ili ajue kipi kimemsibu hadi kutohudhuria masomo.

Aidha jeshi la polisi mkoani Geita limedhibitisha kutokea kwa tukio hilo na kwamba linamshikilia mtuhumiwa kwa uchunguzi zaidi na mara baada ya upelelezi kukamilika atafikishwa mahakamani kujibu shitaka hilo.

No comments:

Post a Comment