Monday 29 February 2016

HALMASHAURI YA JIJI LA TANGA HATARINI KUFUTWA.



Makamu wa raisi Mh.Samia Suluhu Hassan.


Makamu wa raisi akipokelewa mara baada ya kuwasili Tanga.

Wakati sakata la kumpata Meya wa Jiji la Dar es Salaam likiendelea kupamba moto baada ya mchakato huo kuwekewa zuio la mahakama juzi, serikali imetishia kuivunja Halmashauri ya Jiji la Tanga iwapo haitamaliza mgogoro wake wa kisiasa.

MTANGAZAJI WA STORM FM ,JOEL MADUKA AMVISHA PETE YA UCHUMBA BI.DEBORA JACKSON.


Kulia ni Joel akimtambulisha na kuelezea sifa za Mchumba wake mbele ya waumini wa Kanisa la EAGT Lumala Mpya Ilemela Mkoani Mwanza.

Mtangazaji na Mwanahahabari wa Storm Fm ya Mkoani Geita, JOEL MADUKA (Kulia) ambae ni Mkazi wa Jiji la Mwanza, leo February 28,2016 amemvisha Pete ya Uchumba na kumtambulisha rasmi Mchumba wake DeEBORA JACKSON ambae ni Mkazi wa Lumala, Manispaa ya Ilemela Mkoani Mwanza, mbele ya Viongozi wa dini, Waumini pamoja na Wanafamilia.

MAHAKAMA YA MAFISADI KUANZA KUFANYA KAZI


Mwanasheria  mkuu wa serikali, George Masaju amesema mahakama maalumu ya mafisadi inasukwa na itatekelezwa kwa muundo wa mahakama, ikiwa ni kitengo ndani ya Mahakama Kuu.

KIKWETE ASEMA ATAACHA UENYEKITI WA CCM, LAKINI HATOACHA VIKAO VYA NDANI CCM.


























Raisi mstaafu wa awamu ya nne(kushoto)Dkt.Jakaya Mrisho  Kikwete akiwa na Raisi wa awamu ya tano(kulia)Dkt.John Pombe Magufuli.

Moja kati ya hoja zinazogonga vichwa vya baadhi ya makada wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) ni 
mabadiliko ya Uenyekiti wa Chama hicho ambayo yatamuwezesha mzee wa Kutumbua Majipu, Rais John Magufuli kuanzisha operesheni hiyo ndani ya chama hicho.

Sunday 28 February 2016

DC PAUL MAKONDA AAGIZA WALIMU WA SHULE ZA SERIKALI WILAYANI KINONDONI WAPANDE DALADALA BURE.


Mkuu wa wilaya ya Kinondoni Paul Makonda.

Moja ya jambo ambalo serikali ya awamu ya tano chini ya uongozi makini wa Mheshimiwa John Pombe Magufuli imelifanya kuwa kipaumbele kikubwa kwenye mipango yake ya kimaendeleo ni suala la uboreshaji wa sekta ya elimu nchini na ndio maana serikali imeanza utekelezaji wa mpango huu kwa kufuta ada zote mashuleni.

MWANAUME AJIFANYA MWANAFUNZI MIAKA 4 MAREKANI.


Mwanamume mmoja kutoka Ukraine amekamatwa baada yake kujifanya mwanafunzi wa shule ya upili bila kugunduliwa kwa miaka minne Marekani.

USHINDI MKUBWA KWA CLINTON SOUTH CAROLINA KATIKA UCHAGUZI WA MCHUJO WA URAISI.

Hillary Clinton ameshinda kwa wingi wa kura uchaguzi wa mchujo wa urais katika jimbo la South Carolina dhidi ya mpinzani wake mkuu katika chama chao cha Democratic Bernie Sander.

LEO KATIKA HISTORIA, TAREHE 28 FEBRUARY.


Bendera ya Misri.

Miaka 93 iliyopita katika siku kama ya leo , nchi kongwe ya Misri ilipata uhuru. Misri ilikombolewa na Waislamu miaka 20 baada ya kudhihiri dini tukufu ya Kiislamu. Mwaka 969 nchi hiyo ilidhibitiwa na kutawaliwa na silsila ya Fatimiyya hadi mwaka 1172 ambapo utawala huo ulipinduliwa na Waayyubi.

WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA, KUTUA JIJINI MWANZA KESHO KUTWA.

         Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mh.Kassim Majaliwa.
                   Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Mwanza  Baraka Konisaga.

Wakazi  wa Jiji la Mwanza na vitongoji vyake wametakiwa kujitokeza kwa wingi keshokutwa ili kumpokea Waziri Mkuu Kassim Majaliwa ambaye anatarajiwa kuwasili jijini hapa akitokea jijini Dar es Salaam akielekea mkoani Simiyu.

Saturday 27 February 2016

TANZANIA NA KENYA YAZINDUA HUDUMA YA KITUO CHA PAMOJA MPAKANI


Wakizindua Kituo hicho.
Wakizindua huduma hiyo na majengo ya kisasa waziri wa Tanzania anayeshughulikia Nchi za nje, ushirikiano wa Afrika Mashariki kikanda na ushirikiano wa kimataifa Balozi Agustin Mahiga na Phyillis Kandie ambaye ni Waziri wa Kazi na Afrika Mashariki upande wa Kenya wamesema huduma hii iliyozinduliwa ni msingi muhimu katika kuelekea kwenye Ushirikiano imara wa Afrika Mashariki.

KUFUATIA KUAHIRISHWA KWA UCHAGUZI WA MEYA MARA 4 JIJINI DAR ES SALAAM, VURUGU ZAIBUKA LEO TENA.






Vurugu  kubwa zimetokea wakati wa uchaguzi wa Meya wa Jiji la Dar es Salaam mara baada ya uchaguzi huo kuhairishwa  tena kwa mara ya nne leo,huku Jeshi la Polisi likivamia ukumbi wa Karimjee na kuanza kupambana na Madiwani na wabunge wa Muunganiko wa umoja wa Vyama vinavyounda  UKAWA.

BARAZA LA MADIWANI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA LIMEPITISHA SH.BILIONI 69.6 KWA MWAKA WA FEDHA 2016 NA 2017.


Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita.

Baraza la madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Geita Mkoani hapa limepitisha sh.bilioni 69.6 katika mapendekezo na mpango wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2016 na 2017.

Friday 26 February 2016

WATU WANNE WAPOTEZA MAISHA KATIKA AJALI YA BASI LA MASHIMBA EXPRESS.


          Baadhi ya watu waliojitokeza katika eneo la tukio pamoja na abiria walionusurika.
 
                    Basi la mashimba express baada ya kugongana na gari dogo.
                          Gari dogo lililogongana na basi la mashimba express.

Watu wanne wafariki dunia katika ajali baada ya basi la Mashimba Express lililokuwa linasafiri kutoka Kahama kuelekea  jijini Mwanza kugongana na gari dogo katika eneo la njia panda kuelekea wilayani Kishapu Mkoani Shinyanga.

CUF KUANDAMANA KUPINGA UCHAGUZI WA MARUDIO VISIWANI ZANZIBAR


                  Kaimu Mwenyekiti wa Chama cha wananchi(CUF)hicho Saverina Mwijage.

Chama cha wananchi (CUF) Bukoba kimejiandaa kufanya maandamano ya amani keshokutwa, kwa ajili ya kupinga kufanyika upya uchaguzi wa Zanzibar unaotarajiwa kuwa Machi 20 mwaka huu.

Kimeiomba pia serikali ya awamu ya tano, kuchukua uamuzi wa kumtambua Maalim Seif Sharif Hamad kuwa ndiye mshindi wa uchaguzi wa urais Zanzibar na kuwa hakiko tayari kurudia uchaguzi huo tena.

Akizungumza na waandishi wa habari juu ya msimamo wa chama hicho, Kaimu Mwenyekiti wa chama hicho Saverina Mwijage, alisisitiza kuwa kamwe chama hicho hakitakuwa tayari kurudia uchaguzi huo uliotangazwa na Tume ya uchaguzi ya Zanzibar (ZEC) kuwa utafanyika Machi 20,kwa kile kinachodaiwa ni kufutwa uchaguzi wa Oktoba 25,mwaka jana.

“Tumedhamiria kuandamana ili kumfikishia ujumbe wetu Rais John Magufuli kupitia kwa Mkuu wa mkoa wa Kagera, John Mongella lengo letu hasa ni kupinga uchaguzi wa Zanzibar. Hali ya Zanzibar kwa sasa haiko shwari, watu wanatishiwa maisha yao, wanaishi kwa hofu juu ya maisha,” alisisitiza.

Mwijage ambaye pia ni Makamu Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wanawake wa CUF Taifa, alisema chama hicho kinatambua uchaguzi ulishakwisha na tume hiyo ilishatoa vyeti kwa walioshinda, kwa mantiki hiyo CUF inamtambua Maalim Seif kuwa alishinda katika uchaguzi huo.


Alisema maandamano hayo yanatarajiwa kuanzia saa 4:00 asubuhi hadi saa 9:00 alasiri na baadaye utakuwepo mkutano wa hadhara katika Uwanja wa Mashujaa Mayunga ulioko mjini Bukoba ili kuutangazia umma juu ya msimamo wa chama hicho na baada ya hapo watazunguka katika wilaya za Muleba, Missenyi na Karagwe.

AGIZO LA RAISI MAGUFULI LAANZA KUTEKELEZWA, WAZIRI MAHIGA ARUDISHA FOMU.


        Waziri wa Mambo ya Nje, Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Ushirikiano wa Kikanda na                                             Kimataifa, Dk. Augustine Mahiga.

Baada ya waziri mkuu kutaja majina ya mawaziri wanne na naibu waziri mmoja ambao hawajarudhisha fomu za Sekretariati ya maadili ya umma na kutakiwa wawe wamerejesha fomu hizo kabla ya  saa kumi na mbili jioni ijumaa ya leo mpaka sasa ni waziri mmoja aliyetii agizo hilo

SHIRIKISHO LA SOKA DUNIANI (FIFA) KUTANGAZA KIONGOZI MPYA LEO ATAEKUWA MRITHI WA SEPP BLATTER.


Blatter, 79, aliongoza shirikisho hilo tangu 1998. Aling’atuka mwaka jana kutokana na tuhuma za ufisadi zilizogubika shirikisho hilo. Kuna wagombea watano wanaotaka kumrithi.
Ambao  ni Sheikh Salman bin Ebrahim al-Khalifa, Gianni Infantino, Mwana mfalme Ali bin al-Hussein, Tokyo Sexwale na Jerome Champagne. Sheikh Salman na Gianni Infantino ndio wanaopigiwa upatu kushinda.
Upigaji kura utaanza saa 12:00 GMT (saa tisa alasiri saa za Afrika Mashariki) na Kabla ya kura kupigwa, kila mgombea atakuwa na dakika 15 za kuhutubia wajumbe,pia  kuna mataifa 209 wanachama wa FIFA lakini Kuwait na Indonesia kwa sasa hawashirikishwi, hivyo wajumbe watakaopiga kura ni 207.
Ili kutangazwa mshindi duru ya kwanza, mgombea anahitaji kupata theluthi mbili ya kura zilizopigwa. Hili lisipofanyika, wagombea wote wanapigiwa kura tena duru ya pili na atayepata kura nyingi kutangazwa mshindi.

Mshindi akikosekana duru ya pili, basi duru ya tatu hufanyika bila mgombea mwenye kura chache zaidi raundi ya pili, Fifa imesema lazima mshindi ajulikane leo Ijumaa.

SERIKALI YATOA AGIZO DHIDI YA MAWAZIRI WASIOREJESHA HATI ZA TAMKO LA MALI NA AHADI YA UADILIFU.


Waziri mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mh.Kassim Majaliwa.

Raisi  wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dk. John Pombe Magufuli amesema mawaziri ambao hawajajaza Tamko la Rasilimali na Madeni wawe wamejaza fomu hizo na kuzirejesha katika Ofisi za Sekretarieti ya Maadili ya Viongozi wa Umma Dar es Salaam ifikapo leo saa 12.00 jioni (Ijumaa, Februari 26, 2016).

WAZIRI MKUU APOKEA MCHANGO WA VIFAA VYA BILIONI 10 VYA MAHOSPITALI KUTOKA AZAM,COKE NA PEPSI.


              Waziri Mkuu Kassim Majaliwa akitazama baadhi ya vitu vilivyotolewa.



     Mkurugenzi wa IPP Reginard Mengi akislimiana na Waziri mkuu Mh.Kassim Majaliwa.

Umoja wa Wazalishaji Vinywaji laini umetoa msaada wa vifaatiba vyenye thamani ya Sh10 bilioni vilivyopokelewa na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa.

Vifaatiba vilivyopokelewa jana ni pamoja na mashine za aina mbalimbali kama utra sound, mashine za kustulia moyo, vitanda vya watoto njiti, vitanda vya kujifungulia, vitanda 80 vya kawaida na magodoro yake, ambavyo viliwekwa kwenye makontena 20.

“Haijapata kutokea msaada mkubwa kama huu,” alisema Majaliwa kwenye hafla hiyo iliyofanyika kwenye ghala la Bohari Kuu ya Dawa (MSD) iliyoko Mabibo, Ubungo jijini Dar es Salaam. 
 “Natoa wito kwa makampuni mengine binafsi kuunga mkono jitihada za Serikali.”

Msaada huo wa vifaa tiba unawalenga zaidi watoto na wajawazito, ikiwa ni jitihada za kuunga mkono juhudi za Rais John Magufuli katika kuboresha huduma za afya.

Msemaji wa umoja huo, Erastus Mtui kutoka Coca Cola Kwanza alisema msaada huo umelenga kusaidia watoto na wajawazito pamoja na wagonjwa wengine kama wa moyo.

“Tumelenga hasa vifaa vya watoto na wajawazito. Hii yote ni katika kuunga mkono jitihada za Rais Magufuli kwani anaboresha afya na kutokomeza rushwa, hii inayaokoa zaidi makampuni ya uzalishaji nchini,” alisema Mtui.

Akizungumza kwenye hafla hiyo, Majaliwa alizipongeza sekta binafsi kwa kushirikiana na Serikali kukabiliana na changamoto katika sekta ya afya.

Alisema vifaa hivyo vimekuja wakati mwafaka kwa kuwa vitawezesha vituo kutoa huduma bora za afya.
Mtakumbuka kwamba hivi karibuni Rais Magufuli alihamasisha maboresho ya Hospitali ya Taifa ya Muhimbili na hasa wodi ya wazazi, hatua hii mliyoichukua ya kutoa msaada wa vifaa hivi ni sehemu ya kumuunga mkono,” alisema Waziri Mkuu.

Alisema Serikali kupitia MSD itahakikisha vifaa hivyo vinasam bazwa kwenye vituo husika kwa umakini mkubwa, hasa maeneo yenye mahitaji makubwa.

Alisema tayari kuna orodha ya awali katika mikoa ya Dodoma, Geita, Katavi, Lindi, Kilimanjaro, Mara, Mbeya, Shinyanga na Tanga.

Naye Mkurugenzi Mkuu wa MSD, Laurean Bwanakunu alisema bohari imedhamiria kusambaza dawa na vifaa tiba vya kutosha kwenye kanda nane za nchi, lakini changamoto kubwa ni jinsi ya kuzihifadhi.

Ukubwa wa ghala hili la vifaa tiba ni mita za mraba 19,650 na hapa panatugharimu kiasi cha Sh2.5 bilioni. Na iwapo tutaendelea kuhifadhi hapa, itatulazimu kulipia Sh4 bilioni,” alisema Bwanakunu na kuongeza kuwa:

Kwa hiyo changamoto ni kupata eneo la kujenga ghala. Wizara ya Ardhi ikitupatia eneo, tunategemea kuanza ujenzi mara moja.” 

Wafanyakazi PSI wasimamisha ziara
 Wafanyakazi wa kampuni ya PSI walisimamisha msafara wa Waziri Mkuu kwa kuziba barabara wakati akiondoka, wakitaka wamuambie kero wanazokumbana nazo kazini.

Wafanyakazi hao walitoa kero zao mbalimbali ikiwa ni pamoja na kulipwa malipo kiduchu kiasi cha Sh5,750 kwa siku, huku wakinyimwa kushiriki kuchangia mfuko wa hifadhi ya jamii wa PPF.

Shida yetu kubwa ni mshahara. Tangu mwaka 2013 tunalipwa Sh5,750 mpaka leo na kwa miaka yote hiyo watu hawashiriki PPF,” alisema Amini Athuman ambaye ni mfanyakazi wa PSI.
Wote ni vibarua, hakuna aliyeajiriwa hapa. Pia kinamama wajawazito hawalipwi chochote wakienda kujifungua, mtu anafukuzwa kazi bila kosa lolote bosi akiamua.”

Akijibu malalamiko hayo, Waziri Mkuu alisema ameyapokea na kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Tano ilishajipa kazi ya kusikiliza kero za wananchi na wafanyakazi, lazima tatizo hilo litatuliwe.

Nawasihi kesho (leo) mje kazini asubuhi saa 2:00 asubuhi na Waziri ya Kazi, Jenister Mhagama atakuwa hapa kwa kuwa mmelalamika kwamba hata makato ya PPF hayakatwi. Namsihi kiongozi ayaandike vizuri malalamiko ili akija asome kwa umakini na utatuzi utapatikana kesho hiyohiyo. Nawasihi msigome kufanya kazi,” alisema. 

Thursday 25 February 2016

WAFANYABIASHARA WA MAZAO MKOANI GEITA KUTUMIA MIZANI KUNUNULIA BIDHAA NA SIYO MADUMU.

    Mbunge wa Jimbo la Bukombe Mh.Doto Biteko na Raisi wa Jamhuri ya Muungano wa            Tanzania Dkt.John Pombe Magufuli.

Kilio na Masikitiko kilimfikia Mbunge wa Jimbo la Bukombe  Mh Doto Biteko
kutoka kwa wakulima wilayani Bukombe Mkoani Geita kwamba

wafanyabiashara wa mazao wanatumia madumu makubwa maarufu kama

mozambiki kuwaibia mazao yao na kumtaka awasaidie ili kunusuru mazao

yao.

MHANDISI WA HALMASHAURI YA WILAYA YA GEITA NA MKANDARASI WAFIKISHWA MAHAKAMANI KWA TUHUMA ZA RUSHWA.




Taasisi ya kuzuia na kupamba na rushwa(Takukuru) imewafikisha mahakamani mhandisi wa halamshauri ya wilaya ya Geita na mkandarasi kwa  makosa ya rushwa.

MGODI WA GEITA GOLD MINE(GGM) WALALAMIKIWA NA BAADHI YA WAKAZI WA MKOA WA GEITA.


Mgodi wa Geita Gold Mine(GGM)

Wakazi wa mitaa ya Nyamalembo ,Compound na Katoma mkoani Geita wameulalamikia mgodi wa Geita gold mine (GGM) kutokana na kuweka bikoni katika maeneo ya makazi yao zikionyesha kuwa eneo hilo ni mali ya mgodi huo hali ambayo imesababisha wananchi hao kushindwa kuendelea na shughuli zao za maendeleo.

GARI LAPINDUKA MKOANI GEITA NA KUPELEKEA KIFO CHA MTU MMOJA NA MAJERUHI WAWILI.



Kamanda wa polisi mkoani Geita,Mponjoli Lotson

Mtu  mmoja  ambaye hajafahamika  jina lake  amefariki  dunia  baada ya gari alilokuwa amepanda kuacha  barabara na kupinduka hadi   kupelekea  kifo chake .

Aidha ajali hiyo imetokea  jana tarehe 24/02/2016 majira saa tatu na dakika 5 usiku eneo la kijiji cha Chibingo barabara ya Geita katoro kata ya mtakuja wilayani na mkoani hapa, gari  hilo lina  usajili  no t566cvv Toyota Noah mali ya Rhoda Mussa  mkazi wa Sengerema.

Gari hilo lilikuwa likitokea Geita kuelekea Chato na  lilikuwa likiendeshwa na Boniphace Alex  mwenye umri wa miaka 21 mkaazi wa muungano Chato.

Gari liliacha barabara kisha  kupinduka  na kusababisha kifo cha mtu huyo ambaye hajafahamika jina  lake na anasadikika kuwa na umri kati ya miaka 22-25  pia ilipelekea   majeruhi kwa abiria wawili  ambao walikuwa ndani ya gari hilo waliofahamika kwa majina  Mathias Pius mwenye umri wa miaka 27 ambaye ni  mkulima wa katoro  na Leornad Beatus mwenye umri wa miaka  40 ambaye ni  mkaazi wa chato.

Majeruhi wote wana majeraha sehemu mbalimbali ya miili yao  na wamelazwa hospitali ya rufaa  Geita  lakini mwili wa marehemu ambaye  hajafahamika jina una jeraha kichwani  na umehifadhiwa  chumba cha kuhifadhia maiti hosptalini hapo.
 
Aidha chanzo cha ajali hiyo ni  mwendo kasi,  mtuhumiwa Boniphace amekamatwa.

Kamanda wa polisi mkoani Geita,Mponjoli Lotson amethibitisha kutokea kwa ajali hiyo,  hivyo jeshi la polisi linatoa onyo  kwa madereva wote kuwa makini na kufuata  taratibu na kanuni  za usalama barabarani.

STEVEN WASIRA AMKUNJA SHATI MPIGA PICHA BAADA YA KESI YAKE KUPINGA USHINDI WA ESTER BULAYA KUTUPILIWA MBALI NA MAHAKAMA.




              Wasira Akimfuata mpiga picha kwa lengo la kufuta picha alizopigwa.

Mwanasiasa mkongwe nchini, Steven Wasira jana alimvamia mpiga picha aliyekuwa akichukua picha zake wakati akitoka mahakamani, lakini akashindwa kutimiza azima yake ya kufuta picha.

Wasiran ambaye ni Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika wa Serikali ya Awamu ya Nne alifanya kitendo hicho akitoka kwenye jengo la Mahakama ya Biashara ambako maombi yake ya kukata rufaa ya kupinga matokeo ya uchaguzi wa ubunge, jimbo la Bunda yalitupiliwa mbali  na Mahakama Kuu.

Katika kinyang’anyiro hicho cha ubunge, Wasira  ambaye amekuwa mbunge wa Mwibara tangu mwaka 1970 na baadaye mbunge wa Bunda hadi mwaka 2015, aliangushwa na Ester Bulaya wa Chadema katika uchaguzi wa Oktoba 25 mwaka jana. Waandishi kutoka vyombo mbalimbali vya habari akiwamo walishuhudia tukio hilo.

 “Baadaye alitaka kumgonga kwa gari lake wakati akiondoka lakini ikashindikana.”
Akisimulia tukio hilo, Jamson alisema Wasira, ambaye amefanya kazi na serikali za awamu zote tangu katikati ya miaka ya 70, alichukizwa na kitendo chake cha kumpiga picha.

“Njoo, njoo hapa wewe kijana. Nakuambia futa hizo picha kwa usalama wako.Hivi mnatafuta nini maana mnanifuatilia tangu nikiwa kule Mahakama Kuu hadi huku Mahakama ya biashara,” alisema Wasira

Jitihada za Wasira kumnasa Jamson ziliendelea hadi nje ya eneo la mahakama ambako alimfuata kwa kutumia gari aina ya Toyota Land Cruiser (namba tunazihifadhi).

Katika kumfuatilia, gari la Wasira nusura limgonge mpigapicha huyo, lakini waandishi wenzake walimnusuru kwa kumsukumia pembezoni mwa barabara.

Juhudi za kumpata Wasira kuzungumzia sababu za kutaka kumshambulia mpiga picha huyo kwa kuchukua picha za tukio hilo, hazikuzaa matunda.

NAIBU SPIKA DKT.TULIA MWANSANSU ANUSURIKA KIFO BAADA YA KUPATA AJALI JANA.


  



Naibu Spika Dk. Tulia Mwansasu, amepata ajali mkoani Mbeya alikokwenda kwa ajili ya mapumziko. Kwa mujibu wa Mkuu wa Wilaya ya Rungwe, Zainab Mbussi, Dk. Tulia alipata ajali hiyo jana wakati akitokea Mbeya mjini akielekea Kyela.

Mkuu wa wilaya alisema ajali hiyo ilitokea katika eneo la Shule ya Sekondari ya Kipoke iliyoko wilayani humo. 
Alisema maelezo ya askari wa usalama barabarani, yanaeleza kuwa chanzo cha ajali hiyo ni gari dogo lililoelezwa kuwa liliibeba familia ya mtu aliyetajwa kwa jina moja la Chacha, lililokuwa likitokea Kyela kwenda Mbeya, lilipojaribu kulipita lori na kukutana na gari la Naibu Spika.

Mbussi alisema Dk. Tulia, mdogo wake pamoja na mlinzi wake waliokuwa kwenye gari lake wako salama ingawa gari hilo limeharibika vibaya sehemu za mbele.

Aidha, alisema baadhi ya abiria waliokuwa kwenye gari la Chacha wakiwemo wanawe wawili walipata majeraha na walipelekwa katika hospitali ya Mission Igogo, Kiwira.

Awali mapema jana, Dk. Tulia, alitoa msaada wa sh. milioni tano, ili kulifanyia ukarabati bweni  la Mapinduzi, ambalo alikuwa analala wakati anasoma Shule ya Sekondari ya Wasichana Loleza, iliyopo jijini Mbeya.

 Dk. Tulia ambaye alisoma shuleni hapo kuanzia kidato cha kwanza hadi cha nne, mwaka 1991 hadi 1994, pia alitoa msaada wa magunia mawili ya mchele kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi.

Akizungumza na walimu na wanafunzi, Dk.Tulia alisema ametajiwa changamoto nyingi, zinazoikabili shule hiyo na kuwa amzichukua na kuahidi kutafuta wadau atakaoshirikiana nao ili waweze kusaidia kuzitatua.

Dk. Tulia alisema ameguswa na uchakavu wa mabweni, ambapo alipata fursa ya kuonyeshwa yakiwemo mawili aliyokuwa analala akiwa shuleni hapo, ambayo ni Kibo linaloendelea kutumika hadi sasa na lile la Mapinduzi ambalo kwa sasa halitumiki.

Kwenye bweni nililokuwa nikikaa nimepita mwenyewe. Naahidi kushughulika na lile bweni la Mapinduzi ndilo lililo kwenye hali mbaya zaidi kiasi cha kushindwa kuendelea kutumika,” alisema Dk.Tulia.

Dk.Tulia alitoa magunia mawili ya mchele, kwa ajili ya chakula kwa wanafunzi shuleni hapo na aliwachekesha wanafunzi pale aliposema katika mambo ambayo hayajabadirika shuleni hapo ni ratiba ya kula wali mara mbili kwa wiki.

“Kwa sababu mimi dada yao nimewatembelea leo, na waswahili wanao msemo ‘mgeni njoo mwenyeji apone’, basi mimi nitawaletea magunia mawili ya mchele ili angalau kwa hizi wiki wanafunzi wawe wananikumbuka,” alisema Dk.Tulia.

Naye, mbunge wa Songwe, Philip Mulugo, alimuunga mkono Dk.Tulia kwa kuchangia sh. milioni moja, kwa ajili ya kusaidia ukarabati wa bweni hilo la Mapinduzi. 


Viongozi mbalimbali wa Chama na serikali, wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya ya Mbeya, Munasa Nyerembe, walikuwepo katika ziara hiyo na Naibu Spika kutembelea shule hiyo ambayo hivi sasa inachukua wanafunzi wa kidato cha tano na sita tu.

Wednesday 24 February 2016

WALIOKWEPA KULIPA KODI ZA MAKONTENA WAANZA KUFILISIWA

Makontena bandarini
WADAIWA 16 waliokwepa kulipa kodi ya Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA), baada ya kutorosha kontena za mizigo yao kwenye Bandari Kavu (ICD) ya Azam mwishoni mwa mwaka jana, mali zao zinaanza kukamatwa leo na kufilisiwa.

WIZARA YA NISHATI NA MADINI KUDHIBITI TATIZO LA MILIPUKO LIANALOENDELEA KWA BAADHI YA KATA MKOANI GEITA.

       Naibu Waziri wa Nishati na Madini, Dkt. Medard Kalemani, (wa kwanza kushoto), akiongozwa na              Meneja Mwandamizi Miradi ya Umeme wa TANESCO  pamoja na wafuasi wengine.

Mbunge wa geita mjini Mh Costantine Kanyasu 

Wananchi wa kata ya mtakuja mtaa wa Nyamalembo,  Katoma na Kompaund,  wamefikisha malalamiko yao kwa Naibu Waziri wa nishati na madini,mh Dr.Medadi Kalemani juu ya nyumba zao kuendelea kubomoka kutokana na upasuaji wa miamba unaofanywa na kampuni ya uchimbaji wa madini ggm mkoani Geita.

BINTI WA MIAKA MITATU ABAKWA NA KUNYONGWA HADI KUPOTEZA MAISHA.



Mtoto mwenye umri wa miaka 3 na miezi 4 Mariam Deogratius mwanafunzi wa shule ya awali ya Makoko iliyopo katika Manispaa ya Mji wa Musoma mkoani Mara, amebakwa kisha kunyongwa hadi kupoteza maisha  na mtu asiyejulikana Usiku wa kuamkia leo.

Tuesday 23 February 2016

WAKAZI WA MKOA WA GEITA WATAKIWA KUCHANGAMKIA FURSA.


Naibu waziri wa ardhi ,nyumba na manendeleo ya makazi,Mh,Angelina Mabula.

Wananchi mkoani Geita wametakiwa kuchangamkia fursa katika maeneo ambayo  yameshatengwa na serikali ikiwa ni pamoja na kupanga au kununua nyumba za shirika la nyumba la taifa zilizopo  katika kata ya bomba mbili Mkoani hapa.

NECTA YASITISHA KUGAWA VYETI KWA WAHITIMU WA KIDATO CHA SITA 2015 VILIVYOGAWIWA VYATAKIWA KURUDISHWA HARAKA.

Wanafunzi wa kidato cha sita
Baraza la Taifa la Mitihani (Necta), limeagiza kusitishwa kwa ugawaji wa vyeti vya kidato cha sita kwa wanafunzi waliohitimu mwaka 2015, huku vile vilivyokwisha kugawa kwa watahiniwa hao vikitakiwa kurejeshwa kwenye chombo hicho.

FISI WAUA NA KUJERUHI WATU MKOANI TABORA.

Fisi
 Kikosi cha Kuzuia Ujangili Kanda ya Magharibi kinamsaka fisi mmoja kati ya wawili waliowashambulia Samwel Gamalaya na kusababisha kifo chake na kumjeruhi Kusekwa Ngeleja wakati wakikata kuni katika pori lililopo Kitongoji cha Isukamahela Manispaa ya Tabora.

SERIKALI KUWEZESHA UMEME VIJIJINI IFIKAPO 2025.



Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr.John Pombe Magufuli imedhamilia ifikapo mwaka 2025 vijiji vyote nchini vinafikiwa na huduma ya umeme.
Hayo yamesemwa na naibu waziri wa nishati na madini Dk.Medard Kalemani alipokuwa akizungumza na wananchi katika kijiji cha kachwamba kata ya kachwamba na ilemela  wilayani Chato mkoani Geita.

Dr.Kalemani  amesema kwamba mradi wa umeme unaotekelezwa na wakala wa nishati vijijini REA utakuwa na gharama  nafuu hivyo kila mtanzania atumie fursa hiyo kujiletea maendeleo yeye mwenyewe.

Ameongeza kuwa miaka miwili ijayo vijiji vyote vya jimbo la Chato vitakuwa tayari vimeunganishiwa umeme.
Aidha kwa upande wa madiwani wa kata ya kachwamba na ilemela  Stella Kimanunga na Thobias Ntagwanamba  wamemweleza Naibu Waziri  Kalemani changamoto zinazowakabili katika kata zao, kama mbunge mwenye dhamana ndani ya jimbo la chato.

Akijibu kero hizo Dk. Kalemani amesema zipo changamoto ambazo ameanza kuzichukulia hatua na nyingine ataziwasilisha kwa mawaziri wengine wenye dhamana ili ziweze kutatuliwa.

Naibu Waziri huyo wa nishati na madini yupo mkoani Geita kwa ziara ya siku tatu, ikiwa ni mwendelezo wa ziara yake aliyoianza mkoani Tabora, Kigoma  na sasa Geita, kukagua na kuwasha umeme katika vijiji vilivyofikiwa na nishati hiyo.

Monday 22 February 2016

JESHI LA ZIMA MOTO MKOANI GEITA LIMEENDELEA KUTOA ELIMU YA MATUMIZI YA KIFAA CHA KUZIMIA MOTO (FIRE EXTINGUISHER)


   Fire extinguisher(Vifaa vya kuzimia moto)
Kutokana na baadhi ya magari ya kusafirisha abiria kuwaka moto na kusababisha ajali jeshi la zima moto  mkoani  Geita limeendelea kutoa elimu kuhusiana na matumizi ya kifaa cha kuzimia moto (fire extinguisher) katika magari  ili kuzuia ajali za moto katika magari yao.

Sunday 21 February 2016

WACHIMBAJI MKOANI GEITA WAFUNGA BARABARA WAKIDAI MABAKI YA MAWE (MAGWANGALA).


Wachimbaji wadogo wa mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM)
Tamko lililotolewa na Makamu wa Rais Samia Suluhu Hassan kuwa wachimbaji wadogo watapewa mabaki ya mawe ya dhahabu maarufu magwangala kutoka Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM) limesababisha wakazi wa Mtaa wa Nyakabale kufurika mgodini hapo kusubiri ahadi hiyo.

Saturday 20 February 2016

SABABU KUU NNE ZA ANGUKO LA SHULE ZA VIPAJI KATIKA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE NCHINI.


              Dkt.Joyce Ndalichako, Waziri wa elimu,sayansi,teknolojia na mafunzo ya ufundi.

Anguko la shule za sekondari za Serikali zikiwamo za vipaji maalumu katika matokeo ya mtihani wa kidato cha nne, limedaiwa kusababishwa na walimu kukata tamaa, miundombinu duni na mazingira magumu ya kufundishia na kusomea.

YOWERI KAGUTTA MUSEVENI ATANGAZWA MSHINDI WA KITI CHA URAISI NCHINI UGANDA.


                    Raisi wa Uganda Mh. Yoweri Kagutta Museveni

Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika  siku ya Alhamisi ya tarehe 18 february 2016.

YANGA YAIBUKA KIDEDEA LEO BAADA YA KUIFUNGA SIMBA BAO 2-0

                    Shabiki wa yanga wakishangilia baada ya kuibuka kidedea. 

Kitendawili cha nani mbabe kati ya watani wa Jadi wa Msimbazi na Jangwani kimekamilika baada ya Simba kufungwa bao 2-0 kwa mara ya pili ndani ya miaka miwili, ndani ya uwanja wa Taifa jijini Dar es Salaam.

Friday 19 February 2016

WATOTO WANNE WA FAMILIA MOJA WENYE ULEMAVU WA VIUNGO MKOANI GEITA WANAHITAJI MSAADA.

                   
                      Watoto wa mzee Shikome Saliboko wenye ulemavu.

            Mtangazaji wa Stormfm(kati) Joel Maduka akiwa pamoja na watoto wenye ulemavu.

                      
                        Watoto wa mzee Shikome Saliboko wenye ulemavu.

Famila ya Shikome Saliboko yenye watoto wanne ambao wote ni walemavu wa viungo wanaomba msaada kwa wasamalia wema ambao wataguswa  kuwasaidia misaada mbali mbali ikiwa ni pamoja na kupatiwa elimu na mahitaji mengine.

Thursday 18 February 2016

KESI YA MAKAMANDA KOVA NA NZOWA,MVUTANO MZITO WA SHERIA WATAWALA.


Kamanda Suleiman Kova(Kushoto) na Kamanda Godfrey Nzowa(Kulia).

Mahakama ya rufani jana imeanza kusikiliza kesi ya viongozi wawili waandamizi wa polisi, Kamishna mstaafu, Suleiman Kova na Kamishna Msaidizi Mwandamizi, Godfrey Nzowa wanaogombea nyumba ya Serikali.

AMANI NA UTULIVU KUIMARISHWA ZANZIBAR.


Waziri wa mambo ya ndani mheshimiwa Charles Kitwanga.

WIZARA ya Mambo ya Ndani ya Nchi imesema imejipanga kuhakikisha inaimarisha amani na utulivu kwenye marudio ya uchaguzi Mkuu wa Zanzibar mwezi ujao na kukamilisha uchaguzi huo kwa ufanisi.