Wednesday 28 February 2018

BARAZA LA MADIWANI GEITA LAPITISHA BILIONI 77.6 MWAKA WA FEDHA 2018/2019

Makamu mwenyekiti wa halmashauri ya wilaya ya Geita,Khadja Said akiwakilisha Bajeti ya mwaka 2018/19.

MHE BITEKO NA MHE MAVUNDE WATINGA MKOANI SHINYANGA KWA ZIARA YA KIKAZI


Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kushoto) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde (Kulia) wakifatilia taarifa ya Mkoa wa Shinyanga mara baada ya kuwasili Mkoani humo kwa ziara ya kikazi, Leo 27 Februari 2018.


Katibu wa Chama Cha Mapinduzi Mkoa wa Shinyanga Bi Haula Kachwamba akizungumza jambo mara baada ya Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko (Kulia) na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde (Kushoto) kuzuru katika ofisi za chama wakiwa katika ziara ya kikazi, Leo 27 Februari 2018. 


Naibu Waziri wa wizara ya Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akisisitiza jambo mara baada ya kuwasili Mkoani Shinyanga kwa ziara ya kikazi akiwa sambamba na Naibu Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Kazi Vijana na Ajira Mh Anthony Mavunde, Leo 27 Februari 2018. 

Tuesday 27 February 2018

NAIBU WAZIRI NYONGO ASISITIZA UTULIVU NA AMANI KWA WACHIMBAJI WADOGO

Naibu Waziri wa nishati na madini,Stanslaus Nyongo  akizungumza na wachimbaji wadogo wa Kijiji cha Nyakafulu wilayani Mbongwe wakati alipokuwa kwenye ziara yake ya kikazi Mkoani Geita.
Naibu Waziri wa nishati na madini,Stanslaus Nyongo akiwa kwenye shimo ambalo linatumika kuingilia ndani kwaajili ya kuchimba.


Naibu Waziri wa nishati na madini,Stanslaus Nyongo  akizunguka na kukagua baadhi ya  maeneo ya mgodi wa Nyakafulu.

Rais wa shirikisho la  wachimbaji wadogo wa madini nchini  Bw John Bina akizungumza na wachimbaji wadogo wa Nyakafulu wilayani Mbongwe.

Bw,Iddy Mrisho ambaye ni mchimbaji akielezea masikitiko yake na namna ambavyo wamekuwa wakinyanyasika kutoka kwa viongozi wa vikundi.

Baadhi ya wachimbaji wadogo wakimsikiliza  Naibu waziri wa madini,Staslaus Nyongo.

Wachimbaji wadogo wakiwa wamebeba mabango ambayo yanamalalamiko.


Naibu waziri  wa madini Stanslaus Nyongo amewata wachimbaji wadogo wa mgodi wa Nyakafulu na Bingwa  kudumisha amani na utulivu katika shughuli zao  ikiwemo  kujenga desturi ya kufanya usafi wa mazingira ili kuepukana na magojwa ya mlipuko na  iwapo hawatazingatia hayo migodi  hiyo itafungwa.

Monday 26 February 2018

WAZIRI MKUU ATOA AGIZO KWA TAKUKURU JUU YA MKURUGENZI WA HALMASHAURI YA MASASI


Waziri mkuu Kassim Majaliwa amemuagiza kamanda wa TAKUKURU mkoa wa Mtwara Bw. Stephen Mafipa  kumtafuta popote alipo na kumkamata aliyekuwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mji wa Masasi Bw. Fortunatus  Kagoro  kwa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha.

WANANCHI WAMLILIA NAIBU WAZIRI NYONGO WALALAMIKA KUCHELEWESHEWA FIDIA

Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo  akizungumza na wananchi wa kijiji cha Ziwani  kata ya Nyarugusu Wilayani Geita ambao walipatwa na majanga ya kutilikiwa kwa maji yenye sumu kutoka kwenye Bwawa la mgodi wa Nyarugusu mine.

Msemaji Mkuu wa wahanga hao akizungumza mbele ya Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo ambapo alielezea namna ambavyo kwasasa wameendelea kuishi maisha ya shida hali ambayo imepelekea wakaandamana na kufunga barabara na kuhamua kulala hapo kwa takribani siku tano wakidai walipwe fidia zao.

Mzee Slvanus Matanywa akilia mbele ya  Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo kutokana na kucheleweshewa fidia zao kwa muda mrefu.

Wananchi wakimsikiliza Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo wakati alipokuwa akitia maelekezo.

Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo,akizungumza na moja kati ya wakina mama ambao wanamadai ya kulipwa Fidia.

 Wananchi wakifungua njia ya barabara ya kutoka mgodini baada ya kuagizwa na Naibu waziri Staslaus Nyongo.

Katibu wa chama cha mapinduzi Wilaya ya Geita,Julius Peter (Kulia )akizungumza na Naibu waziri wa madini wakati alipofika na kuzungumza na wananchi.

Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo,akikagua na kuangalia Bwawa ambalo limesababisha athari kwenye mazao ya wananchi.

Naibu waziri wa madini Staslaus Nyongo Akizungumza na mmoja wa wamiliki wa mgodi huo Bw ,Alex Kindersley.
Naibu Waziri wa madini Stanslaus Nyongo amewataka wamiliki wa mgodi wa Nyarugusu Mine  Company kuwalipa  fidia haraka  iwezekanavyo  wananchi 133 ambao wapo kwenye kijiji cha Ziwani kata ya Nyarugusu Wilayani Geita kutokana na kuharibiwa mazao yao na sumu ambayo ilitoka kwenye  Bwawa la maji yenye sumu.

Friday 23 February 2018

UBOVU WA BARABARA WAKWAMISHA MAENDELEO

Barabara ya mtaa wa Nshinde Kata ya Nyankumbu Wilayani Geita ikiwa imeharibika kutokana na mvua ambazo zinaendelea Kunyesha.

Mwananchi akishindwa kupita na usafiri  kwenye Barabara ambayo imeharibika kwa kiasi kikubwa.

Mwenyekiti wa mtaa wa Shinde Bw,Makoye Mirambo akizungumza juu ya uharibifu huo unavyowaathiri wananchi wake.

WANAWAKE WANAOISHI MAENEO YA SHUGHULI ZA UCHIMBAJI KUNUFAIKA KATIKA HILI





Wanawake wapato elfu 70 wanaoishi katika maeneo yenye shughuli za uchimbaji wa dhahabu mkoani Geita wanalengwa kujengewa uwezo wa kiuchumi pamoja na kupatiwa huduma bora za afya.

MAKAMU WA RAIS AITAKA SIMIYU KUENDELEZA MPANGO WA EQUIP-TANZANIA




Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan akiongea na wadau wa Elimu Mkoani Simiyu, leo wakati wa Kongamano kubwa la Elimu ya Juu lililoandaliwa na Chuo Kikuu Huria Tanzania kwa kushirikiana na Ofisi ya Mkuu wa Mkoa huo.





Mkuu wa Mkoa wa Simiyu Mhe. Anthony Mtaka akimuelezea Makamu wa Rais (hayupo pichani)  namna utekelezaji wa mpango wa EQUIP-Tanzania unavyofanyika mkoani humo katika kongamano la Elimu ya Juu lililofanyika leo, mkoani humo.





Mkuu wa DFID-Tanzania Bibi Elizabeth Arthy akizungumza mbele ya Makamu wa Rais juu ya mchango wa Serikali ya Uingereza katika kuboresha elimu nchini Tanzania katika kongamano la Elimu ya Juu lililofanyika leo, mkoani Simiyu.

"NI BORA TUKAWIE LAKINI TUFIKE" MHE BITEKO

Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua kinu cha kuchakata dhahabu mara baada ya kutembelea mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018. 
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua baadhi ya mitambo ya uchenjuaji madini katika mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akikagua njia ya kwenda kwenye mgodi wa chini mara baada ya kutembelea mgodi wa uchimbaji dhahabu wa Shanta Gold Mine uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza akiwa katika ziara ya kikazi Mkoani Songwe, Leo 22 Februari 2018.
Naibu Waziri wa Madini Mhe Doto Mashaka Biteko akizungumza na wafanyakazi wa mgodi wa Shanta uliopo katika Kijiji na Kata ya Saza Wilayani SongweLeo 22 Februari 2018

UJENZI WA HOSPITALI YA RUFAA YA MKOA WA GEITA WAFIKIA ASILIMIA 35

Kaimu Mganga mfawidhi Mkoa wa Geita,Dkt Joseph Odero akizungumza na Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji wa Geita wakati walipofika kwaajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa Hospital ya Rufaa ya mkoa wa Geita. 

Michoro ya ramani ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Geita.

Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu akizungumza na  Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Glads Jefta  wakati alipofika kwaajili ya kuona maendeleo ya ujenzi wa Hospitali hiyo.

Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Glads Jefta  akielezea maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa.

Kaimu Meneja wa Wakala wa majengo mkoani Geita Mhandisi Glads Jefta  akionesha michoro ya ramani ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa.


Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu pamoja na mwenyekiti wa halmashauri ya mji,Leornad Bugomola  wakikagua maendeleo ya ujenzi wa hospitali ya Rufaa.

Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji wa Geita.Leornad Kiganga Bugomola akikagua ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita.

Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali Teule ya mkoa wa Geita Bw ,Simon Rweyemamu,akizungumza na waandishi wa habari juu ya hatua iliyopo kwa sasa ya ujenzi wa hospitali ya rufaa ya mkoa wa Geita.
Kaimu Mganga mfawidhi Mkoa wa Geita,Dkt Joseph Odero  akizunguma juu ya changamoto ambazo zipo kwa sasa kutokana na hospitali iliyopo kuwa ndogo.





Hospitali ya rufaa Mkoani Geita inayojengwa Mtaa wa Magogo kata ya Bombambili mjini Geita inatarajiwa kuhudumia wagonjwa zaidi ya elfu moja wa nje na zaidi ya 480 watakaokuwa wakilazwa.

Thursday 22 February 2018

MAKAMU WA RAIS AWAHIMIZA WANANCHI KUCHANGIA UJENZI WA MIUNDOMBINU YA ELIMU

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika katika uwanja wa Nguzo nane Mjini Maswa, wakati wa ziara yake wilayani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akimwagilia mti wa mwembe alioupanda mara baada ya kufungua Jengo la Upasuaji la Hospitali ya Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA SULUHU HASSAN OPERATING THEATER” wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu.
Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki, Mhe.Stanslaus Nyogo ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini akitoa maelezo kwa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan wakati alipokuwa akikagua Jengo la Upasuaji la Hospitali ya Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA SULUHU HASSAN OPERATING THEATER” mara baada ya kulifungua wilayani humo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akikagua Hospitali ya Wilaya ya Maswa mara baada ya kufungua Jengo la Upasuaji la Hospitali ya Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA SULUHU HASSAN OPERATING THEATER” wakati wa ziara yake Mkoani Simiyu, (kulia mwenye miwani) Mkuu wa Wilaya ya Maswa, Dkt.Seif Shekalaghe akimuongoza.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan(katikati) akia katika picha ya pamoja na viongozi wa Chama na Serikali wa Wilaya ya maswa na Mkoa wa Simiyu mara baada ya kufungua Jengo la Upasuaji la Hospitali ya Wilaya ya Maswa ambalo limepewa jina lake “SAMIA SULUHU HASSAN OPERATING THEATER” wakati wa ziara yake wilayani Maswa.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan akiagana na wananchi wa Wilaya ya Maswa mara baada ya mkutano wa Hadhara uliofanyika Uwanja wa Nguzo Nane mjini Maswa.
Mbunge wa Jimbo la Maswa Mashariki ambaye pia ni Naibu Waziri wa Madini , Mhe.Stanslaus Nyogo, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika katika uwanja wa Nguzo nane Mjini Maswa, wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan wilayani humo

Mbunge wa Jimbo la Maswa Magharibi, Mhe.Mashimba Ndaki, akizungumza na wananchi wa Wilaya ya Maswa kwenye mkutano wa Hadhara uliofanyika katika uwanja wa Nguzo nane Mjini Maswa, wakati wa ziara ya Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Samia Suluhu Hassan wilayani humo.