Tuesday 1 March 2016

MBUNGE WA KWIMBA SHANIFU MANSOOR AIPATIA JOKOFU HOSPITALI YA WILAYA YA KWIMBA MKOANI MWANZA.



Mbunge wa jimbo la Kwimba mh.Shanifu Mansoor.

Mkuu wa wilaya ya Kwimba Bi. Pili Moshi .

Hospitali ya wilaya ya Kwimba  mkoani Mwanza imepewa msaada wa jokofu la kutunzia damu salama na mbunge wa jimbo jilo Bw, Shanifu Mansoor kwa  ajili ya kuweza kuwasaidia wananchi wanaohitaji damu.

Akikabidhi jokofu hilo kwa uongozi wa hospitali hiyo Bw.Mansoor amesema amefanya hivyo katika kutekeleza ahadi zake kwa wananchi na kuomba uongozi wa wilaya hiyo kuandika barua kwa bohari ya dawa  MSD wafungue duka la dawa Kwimba.
Aidha ametoa wito kwa uongozi wa hospitali hiyo kuweka dirisha la wazee ili kutoa huduma bure kwao.

Mkuu wa wilaya ya Kwimba Bi. Pili Moshi amewaomba watumishi wa hospitali hiyo kuitunza vizuri jokofu  hiyo ili iweze kusaidia kutunza damu salama kwa ajili ya huduma kwa wananchi wote.

Kwa upande wake kaimu mganga mkuu wa hospitali hiyo Bw. Michael Ngoso amesema jokofu  hiyo imeondoa changamoto ya muda mrefu iliyokuwepo hospitalini hapo.

No comments:

Post a Comment