Wednesday 16 March 2016

WANAFUNZI WA CHUO CHA GLOBAL COMMUNITY MKOANI GEITA WALALAMIKIA CHUO HICHO KUKOSA USAJILI.




Chuo cha ukunga na uuguzi cha Grobal Community kilichopo Wilaya na Mkoani  Geita kinalalamikiwa na wanafunzi wake kutokuwa na usajili.


Wakizungumza na storm habari kwa nyakati tofauti chuoni hapo,wamesema kuwa wamekuwa na wasi wasi na chuo hicho ni kutokana na mtaala wa masomo kutofautiana na vyuo vingine vya uuguzi pamoja na kutokupata ushirikiano pindi wanapokuwa katika masomo ya vitendo hususani katika hosptali na zahanati za serikali kwani wamekuwa wakiambiwa hawatambuliki.

Mmoja kati ya wanafunzi  waliohitimu katika chuo hicho mwaka jana Rosemerry Jacktone,amesema kuwa anasikitishwa  kwa kutokupatiwa cheti cha kumaliza tangu mwaka jana hali  ambayo imeendelea kuwapa wasi wasi na kuwanyima fursa za kuangalia ajira kutokana na kutokuwa na cheti cha chuo.

Aidha Mkurugenzi wa chuo hicho, Bw.Denis Joel  akizungumza na storm habari  amesema kuwa chuo chake kimesajili  wasiwasi wake anajua kuwa wale wanao kizonga chuo hicho ni baadhi  ya watu wenye chuki na maendeleo.


Kwa upande wake kaimu mganga mkuu ,Mabera Ezekiel ameeleza kuwa  kwa uhalisia uliopo katika chuo hicho ni kweli hakijasajiliwa kwani malalamiko ya wanafunzi yameshafika katika ofisi ya mganga mkuu muda mrefu na walikiomba chuo hicho kuhakikisha kuwa kinapeleka  nyaraka ambayo inatambulika kuwa chuo hicho kimesajiliwa.

No comments:

Post a Comment