Friday 31 March 2017

PICHA: TANZANIA,ETHIOPIA ZAKUBALIANA KUENDELEZA USHIRIKIANO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiwa na Mgeni wake Waziri Mkuu wa Ethiopia  Mhe. Hailemariam Dessalegn ikulu leo Jijini Dar es Salaam


Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dkt. Suzan Kolimba na Waziri wa Mambo ya Nje wa Ethiopia Dkt. Workneh Gabeyehu wakisaini mkataba unaolenga ushirikiano katika kupambana na uhamiaji haramu, masuala ya biashara na mapambano na ugonjwa wa malaria Ikulu Jijini Dar es salaam.


Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe na Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Ethiopia Dkt. Hirut Teketel wakisaini mkataba wa makubaliano yanayotoa fursa za uwekezaji pamoja na mafunzo kwa wadau wa sekta ya utalii Ikulu Jijini Dar es salaam.


Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Maghembe na Waziri wa Utamaduni na Utalii wa Ethiopia Dkt. Hirut Teketel wakibadilishana mikataba wa makubaliano yanayotoa fursa za uwekezaji pamoja na mafunzo kwa wadau wa sekta ya utalii Ikulu Jijini Dar es salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na waandishi wa habari na kuwaeleza masuala ambayo wamekubaliana kushirikiana na Serikali ya Ethiopia Ikiwemo sekta ya Nishati, Usafiri wa Anga, Sekta ya Utalii, Sekta ya Elimu pamoja na Sekta ya Maji kulia ni  Waziri Mkuu wa Ethiopia  Mhe. Hailemariam Dessalegn ikulu leo Jijini Dar es Salaam.


Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn akiongea na waandishi wa habari katika hafla ya utiliaji saini mikataba ya ushirikiano baina ya Tanzania na Ethiopia ambao amemuahidi kuendelea kushirikiana katika sekta mbalimbali za maendeleo, Kulia ni Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ikulu leo Jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimpongeza Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akimueleza jambo Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe. Hailemariam Dessalegn mara baada ya kumaliza kuongea na waandishi wa habari Ikulu Jijini Dar es Salaam.





TANZANIA KUPATA MEGAWATI 400 ZA UMEME KUTOKA ETHIOPIA



Tanzania inategemea kupata Megawati 400 za umeme kutoka Ethiopia ikiwa ni moja ya makubaliano yaliyofikiwa baada ya ziara ya kikazi ya siku mbili ya Waziri Mkuu wa Ethiopia Mhe.Haile Mariam Desalegn.  

WANANCHI WAJITOLEA KUISAIDIA SERIKALI KUTENGENEZA BARABARA YA MTAA WA NYANTOROTORO A MJINI GEITA.

Wananchi wa mtaa wa Nyantorontoro "A"Kata ya Nyankumbu wakikwa kwenye shughuli ya kujitolea ya utengenezaji wa Barabara.


Shule ya Msingi ambayo wananchi wamejitolea kutengeneza Barabara ya kufika shuleni Hapo.

Mwenyekiti wa Mtaa wa Nyantorontoro Gerevas Kayelelo kulia akifokeana na moja kati ya wananchi ambaye hakutaka eneo lake kuondolewa mihogo ambayo alikuwa amepanda.


                              Elias Totoe mkazi wa nyantorotoro akizungumza namna ambavyo wameweza kufikia uwamuzi wa kutoa maeneo yao kwaajili ya maendeleo ya mitaa.

Lecta Maningu mkazi nyantorotoro akieleza juu ya tatizo la maji ambavyo limekuwa ni changamoto katika kata hiyo.

Wananchi wakionesha vitendea kazi

 Gerevas Kayelelo m/kiti mtaa wa Nyantorotoro A,akifafanua juu ya uwamuzi wa wananchi kujitokeza kwenye shughuli ya utengenezaji wa barabara.





Barabara ni moja  Kati ya huduma  muhimu za kijamii zinazohitajika  ili kurahisha na kuchochea kasi ya maendeleo lakini maeneo yaliyo mengi hapa nchini  yamekuwa yakikabiliwa na changamoto ya miundombinu hiyo ambayo inarahisisha kasi ya maaendeleo.

MKUU WA WILAYA YA GEITA.,MWAL HERMAN KAPUFI AMEONGOZA MAMIA KUUAGA MWILI WA ALIYEKUWA MWANDISHI WA CHANNEL TEN MKOANI GEITA VALENCE ROBERT.

Jeneza lililobeba mwili wa marehemu Valence Robart Mulamula ukiwa nje ya nyumba yao kwaajili ya heshima ya mwisho kabla ya kwenda kuzikwa kwenye makazi yake ya milele.
Baba wa Marehemu wa katika kati akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ambaye alifika kutoa pole na kushiriki mazishi.
Mkuu wa wilaya ya Geita akitoa pole kwa mama wa Marehemu Valence Robart.

Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi (katikati)akibadirishana mawazo na Mwenyekiti wa halmashauri ua mji wa Geita pamoja na mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita.
Mwili wa Marehemu Valence Robart ukitolewa Nje.
Mkuu wa wilaya ya Geita Mwl Herman Kapufi ,akitoa heshima za mwisho kwenye mwili wa marehemu Valence Robart.
Mwenyekiti wa halmashauri ya Mji  Lernad Kiganga Bugomola akitoa heshima za mwisho na kuuaga mwili wa mwanahabari Valence Robart.
Mwakilishi wa wafanyabiashara Mkoani Geita,Saimon akiaga mwili.
Mwandishi wa ITV Mkoani Geita,Rose Mweko akitoaga mwili wa marehemu Valence Robart.


Marehemu Valence Robert alianza kusumbuliwa na maradhi mwaka jana mwishoni na katika juhudi za kutafuta matibabu alipelekwa jijini mwanza ambapo  alipatiwa matibabu na kurudia hali yake ya awali na kuendelea na Majukumu yake ya kazi lakini Mwanzoni mwa mwaka huu mwezi wa pili hali yake ya afya ilibadirika na kupelekea kuzidiwa mwezi wa tatu hali ambayo ilimrazimu kurudi Nyumbani kwaajili ya matibabu.