Monday 14 March 2016

WANANCHI WA MKOA WA GEITA WAMPONGEZA RAISI MAGUFULI.


Wananchi  mkoani Geita wamempongeza Rais wa jamhuri ya muungano  wa Tanzania Mh. John Pombe Magufuli kwa uteuzi wa wakuu  wa mikoa ambao alitangaza siku ya jana  marchi 13.


Wakizungumza na storm habari baadhi ya wakazi wa mkoani hapa wamesema kuwa uteuzi wa Raisi umeangalia swala la uadilifu na kutazama wale ambao anaamini watakwenda na kasi yake ya kuhakikisha wanafanya kazi kwa bidii ili kuweza kuleta maendeleo katika maeneo ambayo wamepangiwa kufanyia kazi.

Aidha wamemwomba mkuu mpya wa mkoani hapa  Meja Jenerali mstaafu Ezekiel Elias Kyunga kuhakikisha kuwa anatatua changamoto za ajira  kwa vijana na kuwa anatenda kazi kwa kufuata usawa na haki kwa wananchi waliopo mkoani hapa.


Wakuu wa mikoa wapya ambao wameteuliwa na Rais wanatarajia kuapishwa kesho marchi 15 kuanzia majira ya saa 3:30 asubuhi ikulu jijini Dar es salaam.

No comments:

Post a Comment