Friday 11 March 2016

WAHUKUMIWA MIAKA 4 JELA KWA KOSA LA WIZI WA PIKIPIKI WILAYANI BUKOMBE, MKOANI GEITA.


Mahakama ya wilaya ya Bukombe mkoani Geita imewahukumu  watu wanne kwenda kutumikia kifungo cha  miaka minne jela kila mmoja kwa kosa la wizi wa pikipiki aina ya sanilg.



Waliohukumiwa kifungo jela ni Marco Emanuel Teso mkazi wa Katoro na wenzake watatu ambao ni Elisha John naye ni mkazi wa Katoro na wengine ni Paskal Hamis mkazi wa Katente na Nelson Mandela mkazi wa Kapera mjini  Ushirombo.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi wa mahakama hiyo Gabriel Kurwijila mwendesha mashtaka wa polisi Elias Mgobera aliiambia mahakama hiyo kuwa washitakiwa hao walitenda kosa hilo  julai 6 mwaka jana majira ya saa nane usiku huko mtaa wa Kapera Masakuroni  ambako walifanya njama na kuiba pikipiki aina ya sanilg yenye usajiri namba t192 adl mali ya Andrew Jackson yenye thamani ya sh. milioni moja laki saba na tisini 1,790,000 .


Baada ya mahakama kuridhika na ushahidi uliotolewa mahakamani hapo na upande wa mashitaka na wao kukiri kuwa walifanya njama hakimu Gabriel Kurwijira amewahukumu wote wanne kwenda kutumikia kifungo jela miaka minne kila mmoja na baada ya kumaliza kifungo watawajibika kulipa kila mmoja sh.laki nne arobaini na saba na miatano  (447,500)  ili kulipa pikipiki , chini ya kifungu 258 na 265 kanuni ya adhabu sura namba 16 ili iwe fundisho kwa wengine kutokana na matukio ya wizi wa pikipiki kukithiri wilayani Bukombe.

No comments:

Post a Comment