![]() |
Baadhi ya wananchi wa Kijiji cha Nyakagwe wakivuka Mto kwa kuvua viatu kutokana na kukosekana kwa daraja kwenye eneo hilo. |
![]() |
Mwananchi akivusha usafiri kwenye eneo la Mto
ambao unapita kijijini Hapo.
![]() |
Mkuu wa wilaya ya Geita, Mwl Herman Kapufi
akiwa na baadhi ya wajumbe wa chama cha mapinduzi (CCM)wakitazama namna ambavyo
tatizo hilo lilivyo.
![]() |
Mkuu wa wilaya ya Geita, Mwl Herman Kapufi
akizungumza juu ya mikakati ya kuwasaidia wananchi na tatizo la kukosekana kwa
Daraja .
|
Wananchi wa Kijiji cha
Nyakagwe kata ya Butobera Wilayani Geita wameiomba serikali kuwatengenezea
daraja la kuvukia kwenye mto unaopita kijijini hapo kutokana na sasa hivi
kujikuta wakipata shida pindi maji yanapojaa kwenye eneo hilo.
Baadhi ya wanakijiji
ambao wamezungumza na mtandao huu wameelezea kuwa wamekuwa wakipata shida kubwa
pindi mvua zinaponyesha na kusababisha wanafunzi kushindwa kwenda
masomoni pindi mto huo unapojaa maji.
“Pindi mvua zinaponyesha mwandishi
watoto wetu wanashindwa kwenda masomoni kwani hali inakuwa ni mbaya na maji
yana jaa sana kwenye haya maeneo ya juu hivyo tunajikuta tunashindwa namna ya
kufanya tunabaki kuwashauri wanafunzi kutokwenda kwenye masomo lakini tunaamini
kama serikali itasikia kilio chetu ikatusaidia juu ya hili tutakuwa
tumenufaika” Alisema Mzee John Mabisa.
Hata hivyo diwani wa
Kata hiyo,Bw Hemed Swalehe amesema jitihada ambazo amezifanya kwa
sasa ni kuwasiliana na wakala wa barabara vijijini na mijini (TARURA) Hili
waweze kufika na kujionea tatizo hilo waone namna ambavyo wanaweza kuwasaidia
wananchi hao ambao wamekuwa wakiteseka kwa muda mrefu.
Mkuu wa wilaya ya
Geita,Mwl Herman Kapufi amefika kwenye eneo hilo na kujionea tatizo na kuahaidi
kuwasiliana na meneja wa TARURA ili aweze kuja na kuona namna ya kutatua tatizo
hilo.
“Niseme tu kwamba
nitahakikisha Meneja wa TARURA wa Mkoa anakuja na kuona namna ambavyo wanaweza
kusaidia ujenzi wa daraja hili ambalo limekuwa ni tatizo la Muda mrefu kwa
wananchi wa vijiji hivi viwili kwa maana Butobela na Nyakagwe” Alisema DC Kapufi.
No comments:
Post a Comment