Saturday 12 March 2016

SERIKALI MKOANI GEITA INAENDELEA NA JITIHADA ZA KUKABILIANA NA UPUNGUFU WA MADAWATI NA MAJENGO YA KUSOMEA.


Mkuu wa mkoa wa Geita,Bi.Fatuma Mwasa.

Serikali mkoani Geita  inaendelea na jitihada za kukabiliana na upungufu wa madawati na majengo ya kusomea mkoani hapo.

Akizungumza na storm habari katika hafra  iliyoandaliwa na kamati kuu ya ccm mkoani hapa ya kuzipongeza wilaya zilizofanya vizuri katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana katika ukumbi wa ‘lenny hotel’ mkuu wa mkoa wa Geita,Bi.Fatuma Mwassa amesema kuwa amezunguka takribani wilaya zote na kujionea namna na jinsi ambavyo wanafunzi wamekuwa wakipata shida.

Aidha katibu wa CCM mkoani hapa, London Muba,ametoa shukurani  kwa wilaya zote namna na jinsi ambavyo ziliweza kushiriki katika zoezi la uchaguzi mkuu na hivyo kutokana na zoezi kwenda vizuri chama cha mapinduzi kimeamua kutoa hati kwa kila wilaya.

Kwa upande wake mwenyekiti wa wafanyabiashara mkoani hapa  Agnas Inyasi amemwomba Raisi John Pombe  Magufuli kuona umuhimu wa kuwateulia maeneo ya uchimbaji vijana ambao wapo mkoani hapa  ili waweze kufanya kazi na kupata fedha za kujikimu.


Kamati  ya chama cha mapinduzi CCM  mkoani hapa imetoa gari  aina ya noah ikiwa ni zawadi  kwa wilaya ya mbongwe kutokana na kufanya  vizuri  katika uchaguzi mkuu wa mwaka jana.

No comments:

Post a Comment