Friday 8 June 2018

HOFU, KUTOJIAMINI ZAPELEKEA UPOTEVU WA HAKI KWA WANAWAKE GEITA


Baadhi ya wadau wa kupinga ukatili wa kijinsia kwa mwanamke wakiwa kwenye kikao cha pamoja kilichokuwa kimelenga kujadili sera na sheria ya ukatili dhidi ya Mwanamke kilichofanyika kwenye ukumbi wa mikutano wa kanisa la Anglikana Mjini Geita.


Wadau wakisikiliza maelekezo kutoka kwa mwanasheria wa shirika lisilo la kiserikali la Woman promotion center.


Mwanasheria wa shirika lisilo la kiserikali la Woman Promotion Center ,Bi, Walta Caros akizungumza na waandishi wa habari juu ya sheria ya vitendo vya kikatili kwa mwanamke.

Hofu na kutojiamini ni miongoni mwa sababu za wanawake wengi wanaofanyiwa ukatili kushindwa kutoa taarifa na kujikuta wakipoteza haki zao ikiwemo kudhurumia baadhi ya mirathi pindi waume zao wanapofariki.


Hayo yamebainishwa katika kikao cha Shirika lisilo la kiserikali la Woman Promotion Centre na maafisa ustawi wa jamii, watendaji wa mitaa na kata pamoja na Madiwani wa halmashauri za mkoa wa Geita ili kujadili mapungufu ya sera na sheria za nchi zinazohusu masuala ya kijinsia na haki za wanawake.

Afisa maendeleo ya jamii wa Halmashauri ya mji wa Geita Bi Mariam John amesema wanawake wengi wanahofia pale wanapoambiwa kesi zipelekwe mahakamani hali inayosababisha wengi wao kuendelea kunyanyasika .

“Tatizo kubwa ambalo limeendelea kuwakuta wanawake wengi ni kuendelea kuwa wasili kwa maana ya kutokutoa taarifa ambazo zitasaidia kufikishwa kwenye ngazi za kisheria na hata tunapotaka kufikisha kwenye ngazi hizo wengine wamekuwa wakiogopa” Alisema Mariam.

Mwanasheria wa Shirika hilo Bi Walta Carlos amesema kuna umuhimu wa kuwepo kwa sheria au sera itakayozungumzia ukatili kwa wanawake kwa kuwa kumeendelea kuwepo kesi nyingi za ukatili.

“Nadhini ni wakati umefika kwa serikali kuona umuhimu wa kuwepo kwa sera au sheria ambayo itasimamia na kuzungumzia kwa marefu na mapana suala la wanawake na wasichana ambao wameendelea kufanyiwa ukatili hii ni kutokana na sheria iliyopo kwa sasa kuwa na mapungufu mengi” Alisema Mwanasheria Walta.

No comments:

Post a Comment