Friday 18 March 2016

MWALIMU AFIKISHWA MAHAKAMANI KWA KOSA LA UBAKAJI, WILAYANI BUKOMBE MKOANI GEITA.



Jeshi la polisi wilayani Bukombe mkoani geita  limemfikisha mahamani mwalimu Jackson Jilaa  wa shule ya msingi kakoyoyo kata ya Bulega kwa kosa la kubaka na kumsababishia ujauzito mwanafunzi wake mwenye umri wa miaka 16 aliyefaulu kujiunga na kidato cha kwanza mwaka huu katika shule ya sekondari  Bulega.

Mbele ya hakimu mkazi mfawidhi mwandamizi wa mahakama ya wilayani hapo Gabriel Kulwijira, mwendesha mashitaka wa polisi  mkaguzi msaidizi  Neema Naruke ameieleza mahakama hiyo kuwa mshitakiwa bila aibu na bila kujali maadili ya utumishi alimbaka mwanafunzi wake na  kumsababishia  ujauzito.

Amesema kuwa kitendo alichokifanya Mwalimu Jackson Jilaa cha kumharibia maisha mwanafunzi wake ambae alifaulu mtihani wa darasa la 7 ni kitendo cha udhalilishaji na pia ni ukatili wa kijinsia.

Hata hivyo mshtakiwa  mwalimu Jackson amekana shitaka na hakimu mfawidhi wa mahakama ya wilaya Gabriel Kurwijila amemrudisha rumande hadi hapo kesi  itakapotajwa  tena.



No comments:

Post a Comment