Wednesday 31 January 2018

RC GEITA MH. ROBERT LUHUMBI AWATAHADHALISHA WATENDAJI AMBAO WANATAFUNA PESA ZA MIRADI

DSC_1561
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akishiriki na wananchi wa kijiji cha Bukuru kata ya Kafita wilaya ya Nyang’hwale ujenzi wa kituo cha afya cha kijiji hapo.

DSC_1535
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikagua madarasa kwenye shule ya sekondari ya Nyachiluluma Wilayani  Nyang’hwale

DSC_1570
Baadhi ya wakina mama wa Kijiji cha Bukuru wakishiriki shughuli za ujenzi wa kituo cha afya.

DSC_1587
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na wanakijiji wa kijiji cha Bukuru wakati wa ziara ya kuhamasisha maendeleo.

DSC_1596
Zahanati ya Mwamakiliga ambayo ameizindua Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi.

DSC_1632
Mkuu wa Mkoa wa Geita mhandisi Robert Luhumbi akikagua baadhi ya vyumba vya zahanati ya Mwamakiliga.

DSC_1641
Mkuu wa mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akikata utepe wakati wa uzinduzi wa zahanati ya Mwamakiliga.

WANANCHI GEITA WAOMBA ELIMU ITOLEWE ZAIDI JUU YA MFUMO MPYA WA TEHAMA

DSC_1403
Watumishi wa mahakama Wilaya ya Geita wakiwa kwenye ufunguzi wa wiki ya sheria na hapa wakimsikiliza mkuu wa Wilaya ya Geita.Mwl Herman Kapufi.

DSC_1388
Mkuu wa wilaya ya Geita.Mwl Herman Kapufi akisisitiza wananchi kujenga desturi ya kujua sheria na kujifunza mambo mbali mbali ambayo yanahusu sheria wakati wa uzinduzi wa wiki ya sheria Wilaya humo.


DSC_1419
Mtendaji wa mahakama ya wilaya ya Geita,Bw Lothan Simkoko akimshukuru Mkuu wa wilaya kuzindua wiki ya sheria .

DSC_1430
Wanafunzi wa shule ya msingi Kalangalala wakiimba wimbo wenye maudhui ya  siku  ya sheria .


Tuesday 30 January 2018

SHIRIKA LISILO LA KISERIKALI LA AGPAHI LAWAKUTANISHA WAVIU WASHAURI MKOA WA GEITA

DSC_1660
Baadhi ya washiriki wa  Warsha hiyo  wakiwa katika  kwenye ukumbi wa hotel ya Alphendo Mjini Geita wakati wa warsha ya kuwajengea uwezo wa watu wanaishi na VVU (WAVIU).

DSC_1685
Mwezeshaji katika warsha hiyo Bi.Anastella Stephen ambaye ni mratibu wa huduma za VVU na UKIMWI ngazi ya Jamii Wilayani Chato akisisitiza   WAVIU kuacha kuingilia majukumu ambayo  si ya kwao kama kutoa dawa kwa watu ambao wanavirusi vya ukimwi.

DSC_1677
Washiriki wa warsha wakiendelea na warsha ambayo imeandaliwa na shirika lisilo la kiserikali la Ariel Glaser Pediatric AIDS Healthcare Initiative( AGPAHI)  kwa kushirikiana na Halmashauri za wilaya ya Geita Vijijini,Geita Mji ,Chato na Bukombe.(Picha na Joel Maduka.)


DSC_1795
Afisa Miradi Huduma Unganishi kwa jamii kutoka Shirika la AGPAHI, Richard Kambarangwe  akielezea umuhimu wa washiriki wa warsha hiyo kuunda vikundi ambavyo vitaweza kuwasaidia kuelimishana na pia  kufanya shughuli za ujasiliamali.

DSC_1699
Kulia ni Bw.Shilambele Mussa na Bi.Magdalena  Ngwada wakifanya maigizo ya namna ambavyo mhudumu anaweza kutoa huduma kwa  mtu mwenye maambukizi ya Virusi vya Ukimwi .

DSC_1706
MVIU mshauri  Bi.Imelda Assey kutoka CTC  ya hospitali ya wilaya ya  Chato akisisitiza  kuachana na dhana ya kuendelea kujinyanyapaa  kwa watu wanaishi na VVU.

DSC_1726
Mwezeshaji katika warsha hiyo Bi.Amida Yindi  ambaye ni Mratibu wa VVU na UKIMWI  ngazi ya jamii kwenye halmashauri ya wilaya ya Geita akitoa elimu ya namna WAVIU  wanatakiwa kuhakikisha mazingira wanafanyia kazi yanakuwa safi.

DSC_1770
Washiriki wakiwa kwenye vikundi wakijadili baadhi ya maswali.

DSC_1787


DSC_1693
Mwezeshaji  Bi.Amida Yindi akielekeza namna ambavyo MVIU mshauri anaweza kumhudumia mteja.

TAZAMA HAPA MATOKEO YA KIDATO CHA NNE 2017 YALIYOTANGAZWA NA NECTA LEO


MATOKEO



Baraza la Mitihani la Taifa (Necta) limetangaza matokeo ya kidato nne ambapo ufaulu umeongezeka kwa asilimia saba. Shule  iliyoshika namba moja inatoka Mbeya.

Jumla ya watahiniwa  385, 767 walisailiwa kufanya mtihani kidato cha nne mwaka 2017, kati yao 287,713 sawa na asilimia 77.09 ndio wamefaulu ambapo wasichana ni  143,728 sawa na asilimia 75.21 na wavulana 143,985 sawa na asilimia 79.06.

Akitangaza matokeo hayo leo Januari 30, 2018 Katibu Mtendaji wa Necta,  Dk Charles Msonde amesema mwaka 2016 watahiniwa waliofaulu walikuwa 277,283 sawa na asilimia 70.09.

Amesema matokeo ya watahiniwa 50 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya baadhi ya masomo ya mitihani hiyo, watapata fursa hiyo mwaka huu.

"Watahiniwa 77 wa shule ambao walipata matatizo ya kiafya na kushindwa kufanya mtihani watapata fursa mwaka 2018," amesema Dk Msonde.

Dkt. Msonde amesema watahiniwa 265 waliobainika kufanya udanganyifu katika mitihani  matokeo yao yamefutwa huku mtahiniwa mmoja akiandika matusi katika karatasi yake ya majibu.


Friday 26 January 2018

KATIBU WA CCM KATA YA BUHALAHALA ATUHUMIWA KUTAFUNA KIASI CHA TSH. MILIONI 20

ofisi
Ofisi za  kikundi cha wajasiliamali (KIWAGE) zilizopo mtaa wa Shilabela Mjini Geita  zikiwa zimefungwa .

ofisi%2B2
Mwenyekiti wa Mtaa wa Shilabela   Bw,Elias  Mtoni akielezea suala la vikundi ambavyo vimeonekana kuwa na dhana ya utapeli juu ya fedha za wajalisiamali .

BUGOMOLA
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Mji wa Geita,Leornad Kiganga Bugomola akizungumza juu ya uwepo wa taarifa za kiongozi ambaye analalamikiwa kutokomea na fedha za wajasiliamali.

Thursday 25 January 2018

SHIRIKA LA JSI LAENDELEA KUTOA MSAADA WA KUPAMBANA NA WATOTO WAISHIO KWENYE MAZINGIRA MAGUMU GEITA


DSC_1245
Mkurugenzi wa JSI kanda ya ziwa Dr Amos Haki Nsheha akimkabidhi Baiskeli Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita,Elisha Lupuga kwaajili ya kuwapatiwa  wasimamizi wanaotoa huduma kwa watoto wanaoishi kwenye mazingira hatarishi.

DSC_1210
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Geita,Elisha Lupuga akijaribia kuendesha baiskeli ambayo imetolewa na shirika lisilo la kiserikali la JSI.
DSC_1241
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita,Ali Kidwaka akikabidhiwa Baiskeli na Mkurugenzi wa JSI kanda ya ziwa Dr Amos Haki Nsheha 

DSC_1221
Mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita,Ali Kidwaka  Akisoma taarifa ya shukurani kwa shirika hilo.

MILA POTOFU NA UMBALI IMEELEZWA NI SABABU WAJAWAZITO KUJIFUNGULIA NYUMBANI

DSC_0823
Mganga Mfawidhi wa Kituo cha afya cha Uyovu Wilayani Bukombe,Dk Steven  Kazuzu akisoma taarifa mbele ya Mkuu wa Mkoa wa Geita,wakati alipofika kushiriki ujenzi wa jengo la upasuaji.

DSC_0699
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisaini kwenye kitabu cha wageni ofisi ya Mkuu wa wilaya ya Bukombe wakati alipowasili 

DSC_0731
Mkuu wa Wilaya ya Bukombe,Josephat Maganga akisisitiza wananchi kuendelea kushiriki kwenye shughuli za maendeleo ambazo zinafanywa na serikali ya awamu ya Tano.

DSC_0769
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akiweka sawa mawe kwenye msingi wa shule ya Sekondari ya Ushirombo wakati alipofika kushiriki na wananchi shughuli za maendeleo.

DSC_0782
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akizungumza na wananchi pamoja na wakina mama ambao wananufaika na mfuko wa TASAF wilaya ya Bukombe.


DSC_0813
Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Bukombe,Safari Mayala akizungumza na wananchi wa uyovu juu ya maendeleo.

DSC_0835
Mkuu wa Mkoa wa Geita,Mhandisi Robert Luhumbi akisisitiza ushiriki wa wananchi kwenye sekta ya maendeleo kwenye maeneo ambayo wanaishi.

Wednesday 24 January 2018

RAIS MAGUFULI AOMBOLEZA KIFO CHA JAJI MSTAAFU WA MAHAKAMA YA RUFANI TANZANIA


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli amemtumia salamu za rambirambi Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof. Ibrahim Hamis Juma kufuatia kifo cha Jaji Mstaafu wa Mahakama ya Rufani Tanzania Mhe. Robert Kisanga kilichotokea jana tarehe 23 Januari, 2018 katika hospitali ya Regency Jijini Dar es Salaam.

Katika salamu hizo Mhe. Rais Magufuli amesema Jaji Mstaafu Robert Kisanga atakumbukwa kwa mchango wake mkubwa alioutoa kwa Taifa wakati wote wa utumishi wake uliojaa umakini, uchapakazi, uzalendo na ushirikiano na wengine, mambo ambayo yalimwezesha kupata mafanikio makubwa.

“Sote tunafahamu kazi nzuri alizofanya akiwa katika majukumu mbalimbali ya kitaifa, mchango wake katika kuijenga taaluma ya uanasheria baada ya uhuru na uanzishaji wa Mahakama ya Rufani baada ya kuvunjika kwa Jumuiya ya Afrika Mashariki mwaka 1977, kwa hakika mchango wake hautasahaulika.

“Nakuomba Mhe. Jaji Mkuu Prof. Ibrahim Hamis Juma unifikishie salamu zangu za pole kwa familia ya Marehemu Jaji Mstaafu Kisanga, Majaji na wanasheria wote, ndugu, jamaa na marafiki wote walioguswa na msiba huu” amesema Mhe. Rais Magufuli.

Mhe. Rais Magufuli amewaombea wafiwa wote wawe na moyo wa subira, uvumilivu na ustahimilivu katika kipindi hiki kigumu cha majonzi na amemuombea Marehemu Jaji Mstaafu Kisanga apumzishwe mahali pema peponi, Amina.

Gerson Msigwa
Mkurugenzi wa Mawasiliano ya Rais, IKULU
Dar es Salaam
24 Januari, 2018

AIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI ATEKETEZA ZANA ZA UVUVI HARAMU WILAYANI CHATO

DSC_0899-1-768x513
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega  akiteketeza nyavu haramu  zilizounganishwa 21710 zenye macho madogo,makokolo ya Sangara 695,Timba 690,makokoro ya dagaa 90 wilayani Chato.

DSC_0882-1-768x513
Naibu waziri wa Mifungo na Uvuvi Mhe.Abdallah Ulega akizungumza na wananchi wa Mwembeni pamoja na watumishi na viongozi kuacha kuendelea na tabia ya kushirikiana na wavuvi haramu.
  
DSC_1136-768x513
Naibu Waziri wa Mifugo na Uvuvi Mhe.Abdalla  Ulega akizungumza na Wafanyakazi wa Hifadhi ya Lubondo juu ya kuacha kushirikiana na wavivu haramu kwani wamekuwa wakiwaruhusu kuingia kwenye hifadhi na kuwafichia zana zao wanapomaliza kuvua.