Thursday 24 March 2016

WANANCHI MKOANI GEITA WAMEIOMBA SERIKALI KUTOA ELIMU ZAIDI KUHUSIANA NA UGONJWA WA KIFUA KIKUU

Wananchi  mkoani Geita wameiomba serikali  kutoa elimu zaidi kuhusiana na ugonjwa wa kifua kikuu ikiwa ni pamoja na watu kuhudhuria vituo vya afya kupima  ugonjwa huo.


Wakizungumza na storm habari wabnanchi hao wamebainisha kuwa ili kuepukana na ugonjwa wa kifua kikuu ni muhimu kuzingatia kanuni za afya.

Aidha kwa upande wake meneja wa mpango wa taifa wa kudhibiti kifua kikuu na ukoma, Dr Beatrice Mutayoba amebainisha dalili kuu za ugonjwa wa kifua kikuu kuwa ni maambukizi yanayosababishwa kwa njia ya hewa. 

Hayo yanakuja ikiwa leo ni siku ya maadhimisho ya ugonjwa wa kifua kikuu duniani ikiwa na kauli mbiu “tuungane kutokomeza kifua kikuu.


No comments:

Post a Comment