Wednesday 30 March 2016

SERIKALI MKOANI MWANZA KUBORESHA VIFAA VYA ULINZI NA USALAMA.


Serikali Mkoani Mwanza inatakiwa kuboresha vifaa vya  ulinzi na usalama katika visiwa vilivyo ndani ya ziwa Victoria ili kuweza kuinua huduma za uokozi na usalama wa raia mali zao visiwani humo.


Akikabidhi Ofisi ya Mkoa kwa mkuu wa mkoa wa Mwanza Mpya John Mongera Mkuu wa mkoa wa zamani Magessa Mulongo amesema kuwa mkoa uko salama lakini kuna uhaba wa vifaa vya ulinzi na usalama hasa vya majini.

Bw. Mulongo amesema kuwa kuna uhitaji wa Boti za mwendo kasi kwa ajili ya vikosi vya usalama ili kuweza kufika maeneo ya matukio kwa haraka katika visiwa vilivyo ndani ya ziwa Victoria ikiwemo ukerewe na Ilugwa, hali itakayo saidia kudhibiti uhalifu mkoani humo.

Aidha Mkuu wa mkoa mpya Bw.John Mongera akipokea taarifa ya makabidhiano ya  mkoa ameshukuru na kuahidi kuendeleza mazuri yaliyofanywa na mtangulizi wake ikiwa ni pamoja na kudumisha amani na salama wa mkoa huo.


Makabidhiano hayo yamefanyika baada ya Rais wa jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Dr John Pombe magufuli kufanya uteuzi mpya wa wakuu wa mikoa, huku Mulongo amehamishiwa mkoa wa Mara na nafasi yake kuchukuiwa na  Mongera akitokea Mkoa wa Kagera.

No comments:

Post a Comment