YOWERI KAGUTTA MUSEVENI ATANGAZWA MSHINDI WA KITI CHA URAISI NCHINI UGANDA.

Raisi wa Uganda Mh. Yoweri Kagutta Museveni
Tume ya Uchaguzi nchini Uganda imemtangaza Rais Yoweri Museveni kuwa mshindi wa uchaguzi wa urais uliofanyika siku ya Alhamisi ya tarehe 18 february 2016.
Rais Museveni amepata kura 5,617,503 sawa na asilimia 60.75 ya kura zilizohesabiwa kwa mujibu wa mwenyekiti wa tume ya uchaguzi nchini Uganda, Dkt Badru Kiggundu.
Mpinzani wake mkuu Dkt Kizza Besigye amepata kura 3,270,290 ambazo ni sawa na 35.37%.
Awali, waangalizi kutoka Umoja wa Ulaya na Jumuiya ya Madola walikosoa uchaguzi huo kwa kudai kuwa una kasoro nyingi.
Aidha walishutumu kukamatwa kwa mgombea wa upinzani Dkt Besigye na kuzimwa kwa mitandao ya kijamii.
No comments:
Post a Comment