Monday 30 January 2017

WALIMU SHULE YA MSINGI ISABILO WAGOMA KUFANYA KAZI



Walimu  wa shule ya msingi Isabilo wilaya na Mkoa wa Geita wamegoma kufanya kazi tangu Januari 25 mwaka huu  kutokana  na kile kinachodaiwa kuwa  ni kukosa  morali ya kazi baada ya   wanakijiji kuvamia na kuwapiga walimu wawili kwa tuhuma za  kuwaadhibu watoto   wao.

WAHANGA 15 WALIOFUKIWA NA MGODI WA RZ WARUHUSIWA KUTOKA HOSPITALINI LEO



Mchungaji wa Kanisa  FPCT Geita Mathias Gundula  ,Akimshukuru Mungu juu ya yale ambayo ameyateda kwa vijana ambao wameokolewa kutoka mgodini.



Mkuu wa Mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu,Ezekiel Kyunga akiwasalimia wachimbaji ambao walikuwa wamefukiwa na kifusi kwenye Mgodi wa RZ,katika Hosptali ya Rufaa ya Geita.

Wahanga  15  wakiwemo watanzania 14 na Raia mmoja wa kichina  walionusurika na  kifo baada ya kuokolewa kutoka chini ya ardhi kwenye  mgodi wa dhahabu wa RZ Union ulioko  kijiji cha Mawe-meru  kata ya Nyarugusu mkoani Geita baada ya kukaa siku 3 bila chakula wala huduma wameruhusiwa kutoka hospital ya mkoa wa geita walikopelekwa kupata matibabu.

BALOZI OMBENI SEFUE ATEULIWA JOPO LA WATU MASHUHURI AFRIKA



Mwanadiplomasia mahiri wa Tanzania aliyepata pia kuwa Katibu Kiongozi-Ikulu, Balozi Ombeni Sefue ameteuliwa kuwa Mtanzania wa kwanza kuingia katika Jopo la Watu Mashuhuri katika Mpango wa Afrika Kujitathmini Kiutawala Bora (APRM).

Friday 27 January 2017

KICHANGA CHATUPWA CHOONI MKOANI GEITA



Matukio ya watoto kutupwa yanaendelea kuchukua sura mpya baaada ya tukio jingine kutokea leo katika mtaa wa Msalala road Geita mjini ambapo mtu asiyejulikana ametupa kichanga katika shimo la choo jirani na Mbeho Guest house.

SERIKALI YA KIJIJI CHA LWAMGASA HATIANI KUSHITAKIWA MAHAKAMANI




Mkuu wa wilaya ya Geita,Mwl Herman Kapufi akitoa maagizo wakati wa mkutano wa kusoma mapato na matumizi uliofanyika kwenye kijiji cha Lwamgasa.


Mtendaji wa kijiji cha Lwamgasa ,Samwel Shosha akisamo taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji.


Mkuu wa wilaya pamoja na Diwani wa Kata ya Lwamgasa wakifatilia kwa makini taarifa ya mapato na matumizi ya kijiji

Thursday 26 January 2017

MA RC, DC WAAGIZWA KUHAKIKISHA WANACHUKUA HATUA DHIDI YA TATIZO LA WATOTO WAISHIO KATIKA MAZINGIRA HATARISHI



Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) George Simbachawene akizindua kitabu cha Mwongozo wa Taifa wa Utekelezaji wa Sera za Huduma kwa watoto waliokatika mazingira hatarishi kwa Serikali za Mitaa leo jijini Dar es Salaam. Wanaoshuhudia tukio kutoka kushoto ni Kaimu Mkurugenzi wa Shirika la Misaada na Maendeleo la Marekani (USAID)  nchini Tanzania Tim Donnay, Katibu Tawala wa Mkoa wa Dar es Salaam Theresia Mmbando, Naibu Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa – TAMISEMI Dkt. Zainab Chaula na Msaidizi wa Waziri wa Nchi TAMISEMI

RAIS MAGUFULI KUWA MGENI RASMI SIKU YA SHERIA NCHINI



Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.


Jaji Kiongozi wa Mahakam Kuu Tanzania Jaji Ferdinandi Wambali (kushoto) akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.


Msajili Mkuu wa Mahakama ya Tanzania, Katrina Revocati akiongea na wanahabari (hawapo pichani) kuhusu Kilele cha Maadhimisho ya Siku ya Sheria nchini kitakachofanyika hivi karibuni katika viwanja vya Mahakama vilivyopo jijini Dar es Salaam.

WATU 14 WAMEFUKIWA NA UDONGO KWENYE MGODI




Watu  kumi na nne (14) mmoja akiwa  ni  Raia  wa China  wamefukiwa na udongo usiku  wa kuamkia leo majira  ya saa saba usiku wakiwa wanaendelea na majukumu  yao  ya uchimbaji kwenye  kampuni  ya  RZ  iliyopo kijiji cha Nyarugusu wilayani na mkoa wa Geita.

WATU WAWILI WAFARIKI DUNIA KWA KUKOSA HEWA NDANI YA KISIMA



Watu wawili wamefariki Dunia papo hapo katika mamlaka ya mji mdogo  wa Katoro Wilayani na Mkoani Geita baada ya kukosa hewa katika shimo la kisima  ambalo waliingia kwa lengo la kupasua mwamba  uliokuwa  umetanda  katika kisima hicho.

SAKATA LA MAJERUHI WALIOPIGWA NA MCHINA MKOANI GEITA LACHUKUA SURA MPYA




Baadhi ya wafanyakazi wakizungumzia hali ilivyokuwa juu ya kuwepo kwa taarifa ya kupigwa kwa wenzao mgodini hapo.

Wednesday 25 January 2017

PICHA:WAZIRI MWAKYEMBE AKUTANA NA KUFANYA MAZUNGUMZO NA BALOZI WA NORWAY LEO



Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe (katikati) akimsikiliza mmoja wa wataalam walioambatana na Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad (watatu kulia) walipomtembelea ofisini kwake leo jijini Dar Es Salaam.



Katibu Mkuu Wizara ya Katiba na Sheria Prof. sifuni Mchome (wapili kulia) akifafanua jambo wakati wa kikao na Balozi wa Norway na ujumbe wake (hawapo pichani) walipotembelea Wizara hiyo leo ili kujadili namna wataalam hao wanavyoweza kusaidia kiteknolojia katika kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wananchi.



Waziri wa Katiba na Sheria Dkt. Harrison Mwakyembe akiagana na  Balozi wa Norway nchini Tanzania Mhe. Hanne Marie Kaarstad na ujumbe wake baada ya kumaliza kikaol eo jijini Dar es salaam.

TMAA YAJIDHATITI KUKUSANYA MAPATO SEKTA YA MADINI



Kaimu Mkuu wa Kitengo  Cha  Habari toka Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Mhandisi Yisambi Shiwa akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mafanikio ya wakala huo katika kipindi cha Julai-Desemba 2016 ikiwemo kufanikiwa kukusanya Bilioni 79.26 zilizolipwa Serikalini na Kampuni za Madini kama kodi ya mapato. Kushoto ni Meneja Utafiti  na Mipango wa Wakala huo Bw. Julius Moshi na Kulia ni Kaimu Mkurugenzi Uzalishaji na Biashara ya Madini Migodi Mikubwa, ya Kati na Midogo Mhandisi Baraka Manyama.



Meneja  Utafiti na Mipango wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) Bw. Julius Moshi akitoa ufafanuzi kuhusu hatua zinazochukuliwa na wakala huo katika kuhakikisha kuwa Serikali inakusanya mapato yote yanayotokana na Madini.



Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza akizungumza na waandishi wa habari leo Jijini Dar es salaam kuhusu mikakati ya wakala huo kusimamia vyema sekta ya madini ili iweze kulinufaisha Taifa. Kulia ni Meneja Utafiti na MipangowaWakala waUkaguzi waMadini Tanzania (TMAA) Bw. Julius Moshi.


Baadhi ya waandishi wa Habari wakifuatilia mkutano wa Wakala wa Ukaguzi wa Madini Tanzania (TMAA) leo Jijini Dar es salaam.


Kaimu  Mkurugenzi Uzalishaji na Biashara ya madini migodi mikubwa,ya kati na midogo Mhandisi Baraka Manyama akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kupatikana kwa malipo  ya mrabaha kutokana na shughuli za uchenjuaji wa marudio kwa kutumia teknolojia ya VAT LEACHING. Kulia ni Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza na kushoto ni Meneja Utafiti  na Mipango Bw. Julius Moshi.


 Kaimu Mkurugenzi wa ukaguzi wa hesabu za Kodi  na fedha za Migodi Bw. Venance Bahati akieleza kwa waandishi wa Habari kuhusu mikakati ya wakala huo kukagua migodi yote na kuhakikisha kuwa Kodi zote zinalipwa Serikalini kwa kuzingatia sheria na kanuni zinazosimamia sekta ya madini , kulia ni Meneja wa uthamini wa Madini Bw.George Kaseza na  kushoto ni Meneja Utafiti na Mipango Bw. Julius Moshi.

PICHA: RAIS MAGUFULI: JENGENI KITUO CHA DALADALA NA KUPAKI MAGARI MADOGO KIMARA MWISHO



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwasili katika kituo cha mabasi yaendayo haraka Kariakoo Gerezani alipoenda kuzindua Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam leo.Kulia ni Makamu wa Rais wa Benki ya Diunia kwa Ukanda wa Afrika  Maktahar Diop











Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akihutubia mamia ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.




Waziri wa Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa akifafanua jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais _TAMISEMI George Boniphace Simbachawene akizungumza jambo wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.


Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.

Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda akizungumza wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.


Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Joseph Nyamhanga aakimtambulisha Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Balozi Augustine Mahiga(aliyesimama) wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwaongoza viongozi na wananchi wa Dar es Salaam kuimba wimbo wa taifa wakati wa hafla ya uzinduzi Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam leo. Kutoka kulia ni Mbunge wa Ilala Mussa Zungu, Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Dar es Salaam Ramadhan Madabida,Waziri wa OR – TAMISEMI George Simbachawene, Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop, Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa, Waziri wa Mambo ya Nje Balozi Augustine Mahiga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Paul Makonda.


Baadhi ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam wakifuatilia hotuba mbalimbali za viongozi wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akitazama jiwe la msingi mara baada ya kuzindua rasmi Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kulia kwa Rais ni Waziri wa Nchi OR – TAMISEMI George Simbachawene na Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Profesa Makame Mbarawa.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli (wa pili kulia), akiwa na Katibu Mkuu wa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhandisi Mussa Iyombe (katikati) na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop wakimwagilia maji mti uliopandwa kama kumbukumbu za uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akipeana mkono na Makamu wa Rais wa Benki ya Dunia Kanda ya Afrika Makthar Diop wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka Dar es Salaam, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akieenda kumtumza msaani wa muziki Mrisho Mpoto na Banana Zoro   wakati wa hafla ya uzinduzi wa  Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka jijini Dar es Salaam leo. Uzinduzi huo umefanyika katika kituo cha mabasi yaendayo haraka cha Gerezani Kariakoo amba Mpoto na Banana waklitumbuiza wimbo wao unaohamasisha wananchi kufanya kazi hali iliyomvutia Rais Magufuli.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiwa katika picha na baadhi ya viongozi wa kiserikali na siasa wakati wa hafla ya uzinduzi wa Miundombinu na Huduma za mabasi yaendayo haraka, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.Aliyemshikana naye mkono ni Meya wa Jiji la Dar es Salaam Isaya Mwita.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Joseph Magufuli akiendesha Basi la Mwendokasi mara baada ya kuzindua Miundombinu na Huduma za Mabasi yaendayo Haraka, awamu ya kwanza leo jijini Dar es Salaam.









SERIKALI YASITISHA KUPOKEA WAKIMBIZI WA NCHI ZA MAZIWA MAKUU



Serikali imetangaza kusimamisha kupokea wakimbizi kutoka nchi za Maziwa Makuu kwa makundi, kutokana na kutokuwepo kwa sababu za kiusalama, zinazowafanya wakimbizi hao kukimbia nchi zao na kuomba hifadhi ya ukimbizi nchini.

RAIS MAGUFULI AZINDUA MRADI WA MABASI YA MWENDO KASI LEO JIJINI DAR



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Dkt John Pombe Joseph  Magufuli, amezindua Awamu ya Kwanza ya Miundombinu na Utoaji wa Huduma ya Mabasi Yaendayo Haraka (Bus Rapid Transit - BRT) katika Kituo Kikuu cha Mabasi kilichopo Kariakoo eneo la Gerezani jijini Dar es salam.

Monday 23 January 2017

RAIS WA UTURUKI AWASILI NCHINI KWA ZIARA YA KIKAZI



Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa   na Rais wa Uturuki, Mheshimiwa Recep Tayyip Erdogan  aliyefuatana na  mkewe, Mheshimiwa Emine Erdogan (kulia) wakifuhia ngoma kwenye uwanja wa ndege wa Julius Kambarage jijini Dar es salaam baada ya Rais huyo  kuwasili kwa ziara rasmi nchini Januari 22, 2017. Mheshimiwa Majaliwa alimpokea Rais huyo kwa niaba ya Rais John Magufuli. (Picha na Ofisi ya Waziri Mkuu). 



Rais wa Uturuki Mheshimiwa Recep Erdogan amewasili nchini jana jioni (Jumapili, Januari 22, 2017) kwa ziara ya kikazi ya siku mbili na kupokelewa katika Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere  na Waziri Mkuu Kassim Majaliwa na niaba ya Mheshimiwa Rais. Dkt. John Magufuli.

Rais huyo ameambatana na mkewe Mama Emine Erdogan pamoja na Mawaziri watatu ambao ni Waziri wa Mambo ya Nje Mheshimiwa Mevlüt ÇavuÅŸoÄŸlu, Waziri wa Uchumi Mheshimiwa Nihat  Zeybekekci na Waziri wa Nishati na Maliasili Mheshimiwa Berat Albayrak


Pia Rais huyo ameambatana na wafanyabiashara wapatao 85 wa nchi hiyo.

UCHAGUZI MDOGO WA UDIWANI NKOME WAMALIZIKA KWA USALAMA


Baadhi ya wananchi wakisikiliza kwa makini maelekezo ya kupiga kura kutoka kwa msimamizi 


Askari polisi wakiimarisha ulinzi katika kituo cha kupigia kura

WATANZANIA WAHIMIZWA KUZINGATIA USAWA WA KIJINSIA KATIKA SEKTA YA KILIMO



Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam. Kulia ni Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda.


Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono akiwaonyesha waandishi wa habari (hawapo pichani) kitabu kinachotumika kutoa elimu juu ya usawa wa kijinsia katika sekta ya kilimo, sheria za kimila leo jijini Dar es Salaam. Kutoka kushoto ni Mhadhiri wa Shule Kuunya Uandishi wa Habari na Mawasiliano kwa Umma (SJMC) Bw. Dotto Kuhenga, Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele.


Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda akifafanua jambo kwa waandishi wa habari wakati wa mkutano wao na waandishi hao(hawapo pichani) kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam.Kutoka kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono na Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele.


Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (Sehemu ya Uandishi wa Habari na Mawasiliano ya umma –SJMC) Bw, Dotto Kuhenga akionyesha waandishi wa habari kitabu cha mwongozo wa waandishi wa habari  katika utekelezaji wa mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono na Mtafiti kutoka Taasisi ya Taaluma ya Maendeleo UDSM Profesa Bertha Omari Koda (kulia).


Mtaalamu Mwelekezi wa masuala ya Jinsia,Utawala Bora na Maendeleo kutoka LAND O’ LAKES Bibi. Margreth Henjewele akitoa ufafanuzi kuhusu mradi wa uhamasishaji usawa wa kijinsia katika kilimo, uhakika wa chakula na lishe leo jijini Dar es Salaam. Kushoto ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Kimataifa la Maendeleo LAND O’ LAKES Dkt. Rose Kingamkono.