Tuesday 30 May 2017

DC GEITA HERMAN KAPUFI - “MAHAKAMA NI MUHIMILI ULIO HURU”



Mkuu wa Wilaya ya Geita Mwl. Herman Kapufi amewataka wanasheria kuwasaidia wananchi kujua elimu ya sheria kutokana na wengi wao kushindwa kujua sheria hali ambayo inasababisha wengi kukosa haki zao za msingi pindi wanapofuatilia haki zao.

PICHA: YALIYOJIRI KIKAO CHA 37, MKUTANO WA 7 BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 30, 2017



Mwenyekiti wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.



Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji Mhe. Mhandisi Isack Kamwelwe akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017



Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza jambo na Mbunge wa Kaliua(CUF) Mhe.Magdalena Sakaya katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.


Waziri wa Elimu,Sayansi na Teknolojia Prof. Joyce Ndalichako akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Utumishi na Utawala Bora Mhe.Angelina Kairuki akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.


Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe.Khamis Kigwangalla akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.


Naibu Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki Dk.Susan Kolimba akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.


Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.


Waziri wa Fedha na Mipango Dk.Philip Mpango akisoma Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Fedha na Mipango kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.  


Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Faida Bakara akiuliza swali katika kikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.


Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mhe.Amina Mollel akiuliza swali katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017.


Waziri wa Habari,Utamaduni ,Sanaa na Michezo Dk.Harrison Mwakyembe akizungumza jambo na Naibu wake Mhe.Anastazia Wambura katika kikao cha 37 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017


Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera, Bunge,Ajira,Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama akijadili jambo na Mbunge wa Iringa Mjini(CHADEMA) Mhe.Peter Msigwa katika kikao cha 37 cha Mkutanowa Saba wa Bunge la 11 leoMjini Dodoma Mei 30, 2017. 


Mwanasheria Mkuu wa Serikali Mhe.GeorgeMasaju akifafanua jambo katika kikao cha 35 cha Mkutano wa Saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 30, 2017.Kushoto kwake ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Ajira,Kazi,Vijana na Watu wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama na Kulia ni Naibu Waziri wa Nishati na Madini Dk.Medard Kalemani.




PICHA: SPIKA WA BUNGE ATEMBELEWA NA MCHUNGAJI LUSEKELO LEO MJINI DODOMA



Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kushoto)akimsikiliza Mbunge wa Viti Maalum, Mheshimiwa Anna Lupembe (aliesimama)akizungumza jambo pale ugeni kutoka kanisa la Maombezi (GRC)ukiongozwa na Mchungaji, Anthony Lusekelo (wa pili kulia)ulipomtembelea leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akipiga picha ya pamoja na ugeni kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) ukiongozwa na Mchungaji Anthony Lusekelo (wa tatu kulia) baada ya kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (katikati) akizungumza jambo wakati alipotembelewa na ugeni kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) ulioongozwa na Mchungaji Anthony Lusekelo (wa pili kulia) katika kikao kilichofanyika leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.


Spika wa Bunge, Mheshimiwa Job Ndugai (wa pili kulia) akimsikiliza Mchungaji Anthony Lusekelo (kulia) kutoka Kanisa la Maombezi (GRC) pale alipomtembelea leo katika ukumbi wa Spika Mjini Dodoma.


SERIKALI KUIFANYIA MABADILIKO SHERIA YA NDOA NA MIRATHI



Serikali kupitia Wizara ya Afya,Maendeleo yaJamii,Jinsia,Wazee na Watoto imesema kuwa imewasilisha mapendekezo ya maboresho ya Sheria ya Ndoa na Sheria ya Mirathi Wizara ya Katiba na Sheria pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kwa hatua zaidi.

Thursday 25 May 2017

WANNE WAFUKIWA NA KIFUSI NA KUFARIKI MKOANI GEITA



 Wachimbaji wadogo wanne wamekufa baada ya kufukiwa na kifusi katika machimbo madogo ya nyamalimbe yaliyopo wilayani Geita mkoani hapa.

NHIF YAZINDUA MPANGO WA MADAKTARI BINGWA MKOANI GEITA



Kaimu Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba akielezea malengo ya kuwepo kwa madkatari Bingwa kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Geita wakati wa hafra fupi ya uzinduzi ambayo imefanyika kwenye Hospitali ya Rufaa ya Mkoa huo. 



Kaimu Mkurugenzi wa tiba na ushauri wa kiufundi NHIF Makao makuu ,Dr Aifena Mramba akimkabidhi Katibu Tawala wa Mkoa wa Geita Celestine Gesimba Shuka mia moja ambazo wametoa kama msaada kwa hosptali hiyo.




Meneja wa NHIF Mkoani Geita Mathias Sweya Akitoa utambulisho mbele ya mgeni Rasmi wakati wa Hafra fupi ya uzinduzi wa Mpango wa Madaktari Bingwa.

Mfuko wa Taifa wa Bima ya afya (NHIF)  umezindua mpango wa madaktari  Bingwa  Mkoani Geita  lengo likiwa ni kushirikiana na serikali kupunguza changamoto za upatikanaji wa huduma za kibingwa na kusogeza huduma karibu na wananchi pamoja na wanachama wa mfuko huo.

PICHA: YALIYOJIRI KATIKA KIKAO CHA 34, MKUTANO WA SABA BUNGE LA 11 MJINI DODOMA LEO MAY 25, 2017



Mwenyekiti wa Bunge Mwenyekiti   wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Najma Giga akiongoza kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Waziri wa Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenista Mhagama  akiomba Bunge kutengua Kanuni zake na kuruhusu Bunge kuhairisha shughuli zake saa kumi na mbili jioni ili kuruhusu wabunge ambao ni waumini wa dini ya Kiislaamu kutimiza matakwa ya mfungo mtukufu wa Ramadhani unaotarajiwa kuanza Jumamosi.



Naibu Waziri wa Nchi  Ofisi ya Waziri Mkuu Vijana,Ajira na Kazi Mhe. Anthony Mavunde akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Mhe. William Ole Nasha Naibu Waziri wa Kilimo Mifugo na Uvuvi akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Waziri wa Ujenzi,Uchukuzi na Mawasiliano  Mhe. Prof Makame Mbarawa na Naibu wake Mhe.Edwin Ngonyani wakijadiliana jambo katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Waziri wa Ardhi,Nyumba na Maendeleo ya Makazi Mhe.William Lukuvi akiwasilisha  Makadirio ya Maapto na Matumizi ya Bajeti ya Wizara yake kwa mwaka wa Fedha 2017/2018 katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi Mhe. Mwigulu Nchemba akizungumza jambo na Mhe. Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Mpango katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji  Mhe. Charles Mwijage akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Waziri wa Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa  Mhe. Dkt Hussein Mwinyi akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Mbunge wa Viti Maalum (CCM) Mbeya  Mhe. Mary Mwanjelwa akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Mbunge Bukoba Vijijini Mhe. Jasson Rwekiza akiuliza swali katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Mbunge wa Mbulu Vijijini Mhe. Flatei Massay akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.


Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi  Mhe. Mwigulu Nchemba akijadiliana jambo na Mbunge wa Arusha Mjini  Mhe. Godbless Lema Mbunge wa Arusha Mjini katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Waziri wa Viwanda Biashara na Uwekezaji Mhe. Charles Mwijage akijadiliana jambo na Naibu Waziri wa Nishati na Madini Mhe. Dkt Medard Kalemani katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Mbunge wa Hanang Dkt Mary Nagu akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



 Mbunge wa Ileje Mhe.Janeth Zebedayo Mbene akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.



Timu ya Mpira ya Mbao FC kutoka Mwanza wakifuatilia mijadala mbalimbali Bungeni, Mbao Fc wapo Mjini Dodoma kwa ajili ya maandalizi ya Mchezo wa fainali za FA kati yao na Simba Fc zitakazofanyika katika Uwanja wa Jamhuri Mjini Dodoma Jumamosi ya May 27, 2017.



Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Dar Young African “Yanga” kwa msimu 2016/2017 wakifuatilia mijadala mbalimbali Bungeni Mjini Dodoma.


Mabingwa wa Ligi kuu Tanzania Bara Dar Young African “Yanga” kwa msimu 2016/2017 wakifurahia na mawaziri na wabunge mara baada ya kulileta kombe la Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania Bara Bungeni Mjini Dodoma.


 Mbunge wa Mtwara Vijijini Mhe. Hawa Ghasia akiuliza swali katika kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.


Waziri wa Fedha na Mipango Mhe. Dk. Philip Mpango akijibu maswali mbalimbali ya wabunge katika  kikao cha thelasini na nne cha Mkutano wa saba wa Bunge la 11 leo Mjini Dodoma Mei 25, 2017.  





MAHENGE AVAA KIATU CHA ALPHONCE MAWAZO GEITA

Mwenyekiti aliyechaguliwa wa chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA,Fabian Mahenge Akiomba kura kwa wajumbe wakati wa mkutano wa maamuzi ya uchaguzi wa ndani ya chama hicho.

Mgombea wa uenyekiti Bw,Charles Makanje akiomba kuchaguliwa wakati wa uchaguzi wa mwenyekiti ngazi ya Mkoa ndani ya chama cha CHADEMA.


Miongoni mwa wasimamizi wa uchaguzi huo,ambaye ni Afisa wa kanda wa chama Mayala Marthin Akionesha karatasi ya uchaguzi mbele ya wajumbe.

Uchaguzi ukiendelea moja kati ya wajumbe akidumbukiza kikaratasi kwenye chombo cha uchaguzi.

Uchaguzi ukiendelea moja kati ya wajumbe akidumbukiza kikaratasi kwenye chombo cha uchaguzi.

Wajumbe wakifuatilia uchaguzi huo.

Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Katibu wa kanda ya ziwa wa  chama hicho,Bi Rehema James Mkoha akitangaza matokeo ya uchaguzi huo.
Msimamizi wa uchaguzi ambaye ni Katibu wa kanda ya ziwa wa  chama hicho,Bi Rehema James Mkoha,akimkabidhi  hati ya ushindi  Fabian Mahenge ambaye ndio mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya Mkoa.



Mwenyekiti wa CHADEMA Mkoa wa Geita ,Fabian Mahenge akiwashukuru wajumbe kwa kumpigia kura na kumpa nafasi ya kuwaongoza ndani ya chama hicho.



Chama cha demokrasia na maendeleo (Chadema) Mkoani Geita kimefanya uchaguzi wa ngazi ya mwenyekiti kwaajili ya kuziba nafasi ya  aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho,Mkoani humo Alphonce Mawazo aliyeuwawa  mwezi wa kumi na moja  mwaka 2015 huko kwenye Kijiji cha Ludete Halmashauri ya mji mdogo wa katoro.

Uchaguzi huo ulianza majira ya saa Sita na kumalizika saa kumi na moja jioni na msimamizi akiwa ni Katibu wa kanda ya ziwa wa  chama hicho,Bi Rehema James Mkoha ambaye aliwatangaza wagombea wa kiti hicho kuwa ni Fabian Mahenge na Charles Makanje.

Hata hivyo pamoja na kuwepo kwa figisu figisu kwa baadhi ya wajumbe kuonekana kutoa rushwa Msimamizi wa uchaguzi aliwaonya wenye tabia za namna hiyo kuachana nazo mala moja kwani uchaguzi huo unazingatia misingi ya haki kama ilivyo ndani ya katiba ya chama hicho.

Bi,Mkoha akiwa kama msimamizi wa uchaguzi huo alimtangaza Fabian Mahenge kuwa ni msindi wa kiti hicho kwa kura 35 sawa ni asilimia 61.4 huku mgombea Mwingine Bw,Charles Makanje akipata kura 22 sawa na asilimia 61.4.

Hivyo kutokana na matokeo hayo Msimamizi wa uchaguzi huo alimtangaza Bw ,Fabian Mahenge kuwa  mrisi wa nafasi ya aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho ngazi ya Mkoa Alphonce Mawazo aliyeuwawa tarehe 14 mwezi wa 11 mwaka 2015 na kuzikwa tarehe 30 mwezi wa 11 mwaka 2015.

Kwa upande wake mwenyekiti ambaye amechaguliwa Bw,Fabiani Mahenge  amewahidi wanachama  kuwatumikia  kwa kujitoa pamoja na kuwa na mshikamono huku akikemea swala la matabaka ndani ya chama na kuwataka wanachama kuwa wamoja katika kutetea masirahi ya chama hicho.

Uchaguzi huo ulikuwa na  idadi ya ya wapiga kura waliojisajiri 59 ,idadi ya kura ambazo zimepigwa ni 57 halali 57 na ambao hawakupiga kabisa ni 2.