Monday 28 March 2016

RAISI MAGUFULI AWATAKA WATANZANIA KUBORESHA USHIRIKIANO ZAIDI.


Rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania  Dkt.John Pombe Magufuli amewasihi watanzania kuendelea kuwa wamoja na kushirikiana kuijenga nchi yao badala ya kubaguana.

Ametoa wito huo katika kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (KKKT) usharika wa Azania front jijini Dar es salaam, aliposali ibada ya pasaka pamoja na waumini wa  kanisa  hilo.

Amesema mwenyezi mungu alimtoa mwanae wapekee yesu kristo kuja kuikomboa dunia bila kuwabagua wanadamu, vivyo hivyo nasi binadamu wanapaswa kutobaguana, iwe kwa dini, makabila, mitazamo ya kisiasa na hata rangi  zetu.

Aidha  Rais Magufuli amewakumbusha watanzania kufanya kazi kama ambavyo vitabu vitakatifu vinasisitiza umuhimu wa kufanya kazi, na amebainisha kuwa tanzania yenye neema inawezekana endapo kila mtu atazingatia kufanya  kazi.

Katika hatua nyingine pia amewaomba watanzania kuendelea kuliombea taifa lao na pia kumuombea yeye ili afanikiwe kutekeleza jukumu kubwa na zito la kuiongoza   nchi pamoja na kuongoza maombi ya kumuombea Raisi Magufuli na mkewe mama Janeth Magufuli waliohudhuria ibada hiyo, Askofu mkuu wa KKKT Dayosisi ya mashariki na pwani Dkt.Alex Malasusa amempongeza Raisi magufuli kwa tabia yake ya kupenda kuhudhuria ibada na kuwasihi viongozi wengine kupenda ibada.


Askofu Malasusa ameuelezea ufufuo wa yesu kristo kuwa jambo la kuleta matumaini,na hivyo amepongeza mwelekeo wa nchi kwa sasa huku akisema kanisa linaona matumaini  kwa taifa.

No comments:

Post a Comment