Tuesday 1 March 2016

WANANCHI WA MKOA WA GEITA WALISHUKURU SHIRIKA LA UMEME (TANZANIA) TANESCO.

Shirika la umeme Tanzania(TANESCO)

Wananchi wilaya na mkoa wa Geita wamelishukuru  shirika la umeme nchini (TANESCO) kwa kuwasilisha maombi ya kushusha bei ya umeme kwa asilimia 1.1 katika mamlaka ya udhibiti wa nishati na maji (EWURA) pamoja na kuondoa kabisa gharama za maombi ya awali ya  wateja wapya na gharama za huduma kwa wateja wa majumbani.


Storm habari imezungumza na wananchi hao ambao wamedai kuwa kufanya hivyo kutawasaidia kupunguza bajeti ya matumizi ya umeme hasa kwa wajasiriamali wadogo na wananchi wenye kipato cha chini kutokana na kulipa kiasi kikubwa cha malipo na umeme huo kutofika mwishoni  mwa  mwezi mwingine.

Naye meneja wa Tanesco mkoa wa GeitaBbw.Joachim Ruweta amesema kuwa amelifurahia tamko hilo ambalo litakuwa lina unafuu kwa wateja wake na kwamba wamelipokea uzito mkubwa na tayari limeshapelekwa kwenye taasisi husika kwa ajili ya kupunguza gharama hizo.

No comments:

Post a Comment