Tuesday 31 May 2016

WANANCHI WA MKOA WA GEITA BADO HAWAELEWI MIRADI MBALIMBALI INAYOANZISHWA NA MGODI WA DHAHABU WA GEITA(GGM)


Mkuu  wa mkoa wa Geita Meja Jenerali Mstaafu Ezekiel Elias Kyunga   amesema kuwa  miradi mbalimbali inayoanzishwa na Mgodi wa Dhahabu wa Geita (GGM), bado haieleweki kwa Wananchi hali ambayo inasababisha kuwepo kwa malalamiko mengi.

SERIKALI KUANZISHA BENKI YA MAENDELEO YA VIWANDA NCHINI.



Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimia na Waziri wa Nishati na Madini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitembelea baadhi ya mabanda ya bidhaa zinazotoka viwandani wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.

Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji, Mhe. Charles Mwijage akiongea na wadau wa sekta ya Viwanda wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 na kuwataka kuunganisha nguvu katika uanzishaji na uendelezaji wa viwanda nchini ili kuongeza upatikanaji wa bidhaa nchini hali itakayopelekea kukuza uchumi wa nchi na kuongeza ajira kwa watanzania.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akizindua nembo ya shirikisho la viwanda nchini wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam kulia ni Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwekezaji Mh. Charles Mwijage, wa kwanza kulia ni Mkurugenzi Mtendaji wa Shirikisho la Viwanda Tanzania (CTI) Leodger Tenga na wa pili ni Mwenyekiti wa Shirikisho la Wamiliki wa Viwanda nchini Tanzania (CTI)Dr.Samuel Nyantahe.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akiongea na wadau wa sekta ya viwanda nchini(hawapo pichani) na kuwaahidi kuwaunga mkono katika harakati za kuendeleza sekta ya viwanda ikiwamo kuanzisha banki ya maendeleo ya viwanda nchini itakayosaidia kutoa mikopo yenye riba nafuu kwa wale wenye nia ya kuanzisha viwanda.


Wadau wa Sekta ya Viwanda nchini wakimsilkiliza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli wakati wa hafla ya utoaji tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akitoa tuzo kwa washindi wa tuzo za Rais kwa wazalishaji Bora wa Viwandani kwa mwaka 2015 leo Jijini Dar es Salaam.


Monday 30 May 2016

WABUNGE 7 WA UPINZANI WASIMAMISHWA KUHUDHURIA BUNGENI

Akisoma maamuzi hayo ya Bunge Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Haki, Kinga, Maadili na Madaraka ya Bunge, George Mkuchika amesema Januari 27.01.2016 wabunge hao walikiuka sheria na taratibu za kuongoza bunge kwa walishinikiza kiti cha spika kijadili hoja ambayo ilikwisha tolewa uamuzi na kiti hicho.

WANANCHI MKOANI GEITA WALALAMIKIA KUTOZWA PESA ZA KUANDIKISHWA KATIKA DAFTARI LA MAKAZI

Wakazi  wa mtaa  wa  Uwanja  kata ya Nyankumbu mkoani Geita wamelalamikia suala la kutozwa pesa kwa ajili ya kuandikishwa katika daftari linalowatambulisha kuwa ni wakazi wa eneo hilo pindi wanapohamia katika mtaa  huo.

PICHA:JAJI MKUU WA TANZANIA MOHAMED CHANDE OTHMAN KATIKA ZIARA YAKE MKOANI GEITA

5

3

6

2

4


SERIKALI YAPIGA MARUFUKU POMBE YA VIROBA YA KWENYE MIFUKO YA PLASTIKI

Mifuko ya plastiki inayofungasha pombe maarufu kama ‘viroba’ imepigwa marufuku na Serikali kuanzia mwakani.

Saturday 28 May 2016

KUELEKEA FAINALI YA UEFA, FAHAMU MAMBO 14 MUHIMU KATI YA SIMEONE NA ZIDANE

 

 
Kesho Mei 28 katika dimba la San Siro, kutakuwa na pambano kali la fainali ya UEFA pale Real Madrid watakapokuwa wakichuana na mahasimu wao wakubwa Atletico Madrid. Hii imekuwa ni fursa adhimu sana kwa makocha wa timu zote mbili yaani Zinedine Zidane na Diego Simeone kuoneshana umwamba kutokana na wote kuwa na historia ya kuvichezea vilabu hivyo.

REKODI YA SERENGETI INDIA YAWAPAGAWISHA WAKENYA.

  Kikosi cha timu ya soka ya Serengeti Boys.


Serengeti Boys imecheza mfululizo michezo 7 ya kimataifa bila kufungwa dhidi ya Misri (2), India, Kore, Malaysia, na Marekani (USA).

ULIMWENGU NAYE KUIKOSA STARS DHIDI YA HARAMBEE KESHO

Mchezaji Thomas Ulimwengu
Mchezo wa kirafiki wa kimataifa kati ya wenyeji Kenya na Tanzania, Taifa Stars utapigwa kesho katika Uwanja wa Moi Kasarani mjini Nairobi, Kenya kuanzia Saa 10:00 jioni.

Thursday 26 May 2016

TAIFA STARS KUCHEZA NA HARAMBEE BILA SAMATTA

MSHAMBULIAJI wa kimataifa wa Tanzania, Mbwana Ally Samatta(pichani kushoto) hataweza kusafiri na Taifa Stars kwenda Nairobi, Kenya kucheza na wenyeji Harambee Stars mchezo wa
kirafiki wa kimataifa.

KRC Genk imemuombea Samatta kutorejea nchini kwa ajili ya mchezo huo kwa sababu inamuhitaji katika mechi ya mchujo wa mwisho wa kuwania tiketi ya kucheza michuano ya Europa League.
Na kwa ombi hilo la timu hiyo ya Ubelgiji, Samatta hatakuwemo kwenye msafara wa unaoondoka kesho saa 12.00 Alfajiri chini ya makocha wake, Charles Boniface Mkwasa na Hemed Morocco.
Mchezo huo ni maandalizi ya kujiandaa kucheza Misri Juni 4, 2016 katika mchezo wa kuwania kufuzu kucheza fainali za Kombe la Mataifa ya Afrika (AFCON-2017) wakati Kenya pia itakuwa na mchezo dhidi ya Congo.

Wednesday 25 May 2016

RAIS MAGUFULI AMTEUA WAZIRI MKUU MSTAAFU MIZENGO PINDA KUWA MKUU WA CHUO KIKUU HURIA (OUT)


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli amemteua Waziri Mkuu Mstaafu Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda kuwa Mkuu wa Chuo Kikuu Huria cha Tanzania (OUT).

Mheshimiwa Mizengo Peter Pinda anachukua nafasi iliyoachwa wazi na Balozi Dkt. Asha-Rose Mtengeti Migiro ambaye ameteuliwa kuwa Balozi wa Tanzania nchini Uingereza.

Taarifa iliyotolewa leo tarehe 25 Mei, 2016 na Katibu Mkuu Kiongozi Balozi John Kijazi imeeleza kuwa uteuzi wa Mheshimiwa Pinda unaanza mara moja.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam
25 Mei, 2016

SERIKALI YAWEZESHA VIKUNDI 1,200 VYA WAKULIMA KUPATA MASOKO

Serikali imefanikiwa kuwezesha vikundi 1200 vya wakulima wadogo wadogo nchini ili kupata masoko ya uhakika ya mazao yao wanayozalisha.

USAJILI WA WAFANYAKAZI WA UMWAGILIAJI DAWA ZA UKOKO WAINGIA DOSARI MKOANI GEITA


Wananchi  mkoani  Geita wamelalamikia kuwepo kwa tabia ya kuchukuliwa watu  wa  mikoa  ya  nje  katika zoezi la usajili wa wafanyakazi wa umwagiliaji dawa za viuatilifu vya mbua.

HUYU NDIYE NYOTA ALIYEAPA KUFIA MSIMBAZI LICHA YA KUTAKIWA JANGWANI


Beki wa kushoto wa Simba, Mohamed Hussein Tshabalala, amesikia kwamba Yanga wanaitaka saini yake kwa udi na uvumba na alichowaambia ni kwamba wasahau mpango huo.

SERENGETI BOYS YAITUNGUA MALAYSIA 3-0 NA KUSHIKA NAFASI YA TATU.

boys
Serengeti Boys wameibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Malaysia katika mchezo wa kumtafuta mshindi wa tatu katika michuano ya vijana ya AIFF ya nchini India.

TANESCO YAWATAKA WATEJA WAKE KUZINGATIA SHERIA NA KANUNI ZA MATUMIZI YA UMEME



Meneja wa Afya na Usalama Mahali pa Kazi Kutoka Shirika la Umeme Tanzania (TANESCO) Mhandisi Majige Mabula akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) ambapo aliwataka wateja wa shirika hilo kuzingatia sheria na kanuni za matumizi ya umeme ili kuepuka ajali zinazoweza kusababishwa na hitilafu za umeme.Kulia ni Afisa Uhusiano wa Shirika hilo Bw. Yasini Silayo.

HII NDIO REKODI YA YANGA NA AZAM KUANZIA 2008-2016

Image result for yanga azam

BUNGE LATOLEA UFAFANUZI MADAI YA KITWANGA KUJIBU SWALI BUNGENI HUKU AKIWA AMELEWA


Bunge limekanusha taarifa inayosambazwa katika mitandao ya kijamii na watu wanaodaiwa kuwa ni madiwani wa Halmashauri ya Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Tuesday 24 May 2016

SERIKALI IMEDHAMIRIA KUIFANYA TANZANIA KUWA NCHI YENYE UCHUMI WA KATI KWA KUBORESHA MAZINGIRA YA BIASHARA



Katibu Mkuu Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Uratibu,Bunge,kazi,Ajira na watu wenye ulemavu Dkt. Hamis Mwinyimvua(Kushoto) akizungumza wakati wa akifungua mkutano wa wadau wa biashara nchini uliolenga kujadili namna ya kuboresha mazingira ya biashara katikati ni Mkurugenzi Mtendaji  wa Taasisi ya Sekta Binafsi Tanzania Godfrey Simbeye na kulia ni Katibu Mtendaji wa Baraza la Taifa la Biashara(TNBC) Raymond Mbilinyi.

CHUO CHA ELIMU YA BIASHARA(CBE) CHAWATAKA WANANCHI KUPUUZA TAARIFA ZA UPOTOSHAJI ZINAZOTOLEWA NA VYOMBO VYA HABARI


Mkuu wa Chuo cha Elimu ya Biashara (CBE) Prof. Emmanuel Mjema akiwaonesha waandishi wa habari (hawapo pichani) ripoti ya Mdhibiti na mkaguzi mkuu wa hesabu za serikali (CAG) inayoonesha kuwa chuo hicho kimepata ziada ya bilioni 1.2 kati ya mwaka huu na kufanya chuo kujiendesha kwa faida tofauti na baadhi taarifa za upotoshaji zilizotolewa na baadhi ya vyombo vya habari.

YANGA KUKUTANA USO KWA USO NA TP MAZEMBE KOMBE LA SHIRIKISHO AFRIKA

IMG_201605145_043419
Droo ya kupanga makundi mawili ya timu zitakazo cheza katika kuwania nafasi ya kufuzu hatua ya nusu fainali ya kombe la shirikisho Afrika imetoka ambapo timu ya Tanzania bara klabu ya Yanga ipo Group A itapambana na timu za TP Mazembe (Congo DR), MO Bejaia (Ageria) na Medeama (Ghana).

VITA YA AZAM FC NA YANGA SC KOMBE LA SHIRIKISHO KUJULIKANA KESHO


Mchezo huo utapigwa kesho kuanzia saa 10:30 jioni  kwenye Uwanja wa Taifa, jijini Dar es Salaam huku waamuzi wasaidizi watakuwa Ferdinand Chancha wa Mwanza (line 1) na upande wa pili ni Soud Lila wa Dar es Salaam (line 2) na mwamuzi wa akiba ni Frank Komba wa Dar es Salaam pia na Kamishna wa mchezo huo atakuwa Juma Mgunda wa Tanga.

Monday 23 May 2016

MANCHESTER UNITED YAMFUTA KAZI LOUIS VAN GAAL

Mkufunzi wa kilabu ya Manchester United Louis van Gaal amefutwa kazi kama mkufunzi wa klabu ya Manchester United ,huku aliyekuwa mkufunzi wa Chelsea Jose Mourinho akitarajiwa kuchukua mahala pake.Raia huyo wa Uholanzi anaondoka baada ya kukamilisha miaka miwili ya kandarasi yake kati ya mitatu.Kitengo cha habari za michezo cha BBC Sport kiliripoti siku ya Jumamosi kwamba ushindi wa United wa kombe la FA dhidi ya Crystal palace utakuwa mechi yake ya mwisho akiwa mkufunzi.Uteuzi wa Mourinho unatarajiwa kuthibitishwa baada ya raia huyo wa Ureno mwenye umri wa miaka 53 kukutana na maafisa wakuu wa United siku ya Jumanne.

JUMA ABDUL NDIYO MWANASOKA BORA WA MWEZI APRIL

Beki wa kulia wa timu ya soka ya Young African ya Dar es Salaam, Juma Abdul ameteuliwa kuwa mchezaji bora wa mwezi Aprili, 2016 baada ya kura zake kuwashinda Donald Ngoma ambaye pia anakipiga Young Africans na Hassan Dilunga wa JKT Ruvu ya Pwani.

SPIKA ASEMA BAADHI YA WABUNGE HUVUTA BANGI NA UNGA, ASEMA VIFAA MAALUM VITAFUNGWA ILI KUWABAINI


Kama unashangaa kusikia kwamba aliyekuwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Charles Kitwanga, ametimuliwa kwa kuingia bungeni akiwa amelewa.
Bila shaka utachoka zaidi ukisikia kuna wabunge kadhaa huingia kwenye ukumbi wa Bunge wakiwa wametumia vilevi vikali zaidi vikiwamo bangi, viroba na dawa za kulevya.

Sunday 22 May 2016

FAHAMU FAIDA ZA KULA TUNDA LA PAPAI KIAFAYA

PAPAI IMAGE 1
Asili ya mpapai ni Amerika ya Kati, ambapo kuanzia matunda, majani na utomvu wa mmea huu hutumiwa kama dawa maeneo mbalimbali duniani. Vile vile, matunda na utomvu wake yamekuwa yakitumika kutengeneza pombe na mvinyo katika baadhi ya nchi, huku wengine wakitumia mpapai kama dawa kwa mifugo na binadamu.

MGODI WA DHAHABU WA GEITA NA TACAIDS WAZINDUA KAMPENI INAYOLENGA KUPIGA VITA MAAMBUKIZI YA VIRUSI VYA UKIMWI























Mgodi wa Dhahabu wa Geita(GGM) kwa kushirikiana na TACAIDS walizindua rasmi kampeni inayolenga kupiga vita maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.

Saturday 21 May 2016

MAREKANI YATOA SALUTI KWA WAPIGANAJI WA TANZANIA, YAMTUNUKU NISHANI YA ULIPUAJI WA MIZINGA MEJA JENERALI JAMES MWAKIBOLWA

Mnadhimu Mkuu wa Jeshi la Marekani linaloshughulikia masuala ya kijeshi barani Afrika, Meja Jenerali Darrly Williams, amemtunuku mkuu wa majeshi ya vikosi vya nchi kavu Tanzania Meja Jenerali James Mwakibolwa nishani ya ulipuaji bora wa mizinga nchini.

MTOTO AMUUA MAMA YAKE NA KISHA KUMTUNDIKA DARINI

Mkazi wa Kitongoji cha Kapembo, Kijiji cha King’wangoko wilayani Kaliua, Mkoa wa Tabora, ametiwa mbaroni  akituhumiwa kumuua, mama yake mzazi , Kiziko Lukambwe kwa kumnyonga kisha kumtundika ndani ya nyumba waliyokuwa wakiishi.

MAONI YA ZITTO KABWE BAADA YA RAIS MAGUFULI KUMFUTA KAZI CHARLES KITWANGA

Habari kubwa iliyoteka vyombo mbalimbali vya habari jana usiku ni habari ya Rais Magufuli Kumfuta kazi Waziri wa Mambo ya Ndani ya nchi, Charles Kitwanga

UFAFANUZI WA WAZIRI MKUU KASSIM MAJALIWA KUHUSU KUTENGULIWA KWA KITWANGA

Waziri  Mkuu Kassim Majaliwa amesema uamuzi wa Rais Dk. John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani, Bw. Charles Kitwanga umefuata kanuni za utumishi wa umma ambao unakataza mtumishi kulewa akiwa kazini.

TAREHE 20 MWEZI MAY RAISI MAGUFULI ALITENGUA UTEUZI WA WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI


Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli ametengua uteuzi wa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Mheshimiwa Charles Kitwanga kuanzia leo tarehe 20 Mei, 2016.

Rais Magufuli ametengua uteuzi huo kufuatia kitendo cha Mheshimiwa Charles Kitwanga kuingia bungeni na kujibu swali linaloihusu wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi akiwa amelewa.

Gerson Msigwa
Kaimu Mkurugenzi wa Mawasiliano, IKULU
Dar es salaam

20 Mei, 2016

NI MIAKA 20 SASA TANGU KUTOKEA KWA AJALI YA MELI YA MV BUKOBA.









Mei 21,1996 katika ziwa Victoria, meli ya MV Bukoba ilipata ajali na zaidi ya watu 800 kupoteza maisha. Meli hiyo ilizama ikiwa imebakiza kilomita 30 kutia nanga kwenye bandari ya Jiji la Mwanza ikitokea mkoani Kagera.

TANZIA: ALIYEKUWA MKURUGENZI WA JIJI LA DAR ES SALAAM, WILLSON KABWE AFARIKI DUNIA

Aliyekuwa Mkurugenzi wa Jiji la Dar es Salaam, Wilson Kabwe ambaye April 19 mwaka huu alisimamishwa kazi na Rais Magufuli amefariki dunia usiku wa kuamkia leo.

Friday 20 May 2016

JUMLA YA WADAIWA 21,721 WAJITOKEZA HESLB KUREJESHA MIKOPO



Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Robert Kibona akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utekelezaji wa agizo la siku 60 kwa wadaiwa wa Bodi hiyo na waajiri, ambapo takribani asilimia 72 ya wadaiwa wote wameshawasilisha taarifa zao. Kulia ni Meneja Habari, Elimu na Mawasiliano wa Bodi hiyo.


Mkurugenzi Msaidizi Habari, Elimu na Mawasiliano kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Cosmas Mwaisobwa (kushoto) akieleza kwa  waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu utaratibu wa urejeshaji wa mikopo kwa wadaiwa ambao mikopo yao imeshaiva. Kulia ni Mkurugenzi wa Urejeshaji Mikopo kutoka Bodi ya Mikopo ya Elimu ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu (HESLB) Bw. Robert Kibona

JESHI LA POLISI JIJINI DAR ES SALAAM LAFANIKIWA KUMKAMATA TAPELI WA MADINI


Kamanda wa Polisi kanda maaalum ya Dar es Salaam Kamishna Simon Sirro akionesha waandishi wa habari mzani unaodaiwa kutumiwa na tapeli wa madini kupima madini bandia na kuwatapeli wananchi wakati wa kutoa taarifa ya kukamatwa kwa tapeli huyo Jijini Dar es salaam Mei 20 2016.

WIZARA YA NISHATI YATENGEWA TRIL.1.22/- KATIKA BAJETI YA MWAKA WA FEDHA 2016/17

Wizara ya Nishati na Madini imetengewa Sh trilioni 1.22 katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/17 huku fedha za miradi ya maendeleo zikiwa ni asilimia 94 ya fedha hizo.