Tuesday 1 March 2016

WANANCHI MKOANI GEITA WALALAMIKIA MAGARI YA TAKA KUSHINDWA KUBEBA TAKA.


Uchafu ukiwa umerundikana bila kubebwa

Wananchi  wa  kata  ya Kalangala  mtaa wa Misheni wilaya na  mkoani Geita wamelalamikia magari  ya kubeba taka kushindwa kubeba taka hizo kwa wakati hali inayoweza kuwasababishia kupata magonjwa  ya  milipuko ukiwemo    kipindupindu.

Wakizungumza na storm habari  wananchi hao wamesema kuwa  magari hayo yamekuwa hayasimami mahali husika kwa muda na na wakati  mwingine huacha taka hizo.

Naye mwenyekiti wa mtaa huo bw. Juma Kajala amelalamikia swala hilo kutokutekelezwa huku akidai magari hayo hayatekelezi majukumu yao  kama     wanavyokuwa wanazungumza kwenye vikao  vyao.

“Magari yamekuwa hayasimami mahali usika lakini pia yamekuwa hayakai mda mrefu nap engine kushindwa kufika katika baadhi ya meneo jambo amblo linasabisha uchafu kuendelea kubaki katika maeneo ya makazi ya watu”.alisema

Afisa mtendaji wa kata hiyo Samsoni  Lukas  Muhondwa  amedai kuwepo kwa kero hiyo katika kata yake huku  akiwalalamikia madereva hao kushindwa kutekeleza zoezi hilo kwa wakati

Afisa usafishaji wa mazingira wa halmashauri ya mji wa Geita Pankrasi  Shwekelela  ametoa wito kwa jamii kutoa  ushirikiano kwa  magari hayo huku akidai mpango huo wa kupuliza filimbi ni mpya japo kuna changamoto wanazokutana  nazo madereva   hao.

“Jambo hilo limekuwa likikubwa na changamoto kwani mpango huu bado ni mpya hivyo watu wengi bado hawajaufahamu vizuri ndio maana matatizo kama hayo yanajitokeza”,alisema


No comments:

Post a Comment