Thursday 31 March 2016

TAASISI NA MASHIRIKA MBALIMBALI YATAKIWA KUUNGA MKONO SEKTA YA ELIMU MKOANI GEITA.



Mkuu wa mkoa wa geita  meja Jenerali mstaafu Ezekile Kyunga, ametoa wito kwa taasisi,mashirika na watu binafisi kujitokeza katika kuunga mkono  swala la elimu  mkoani  hapa.


Wito huo  ameutoa wakati wa makabidhiano ya mabati 300 kwa ajili ya kuezekea madarasa katika wilaya ya Geita  yaliyotolewa  na mfuko wa hifadhi wa LAPF ambayo yamegharimu kiasi cha Sh.milioni saba.

Amesema kuwa  ni vyema kwa taasisi ,na mashirika ya watu kujitolea kwa moyo binafsi na wa dhati kuchangia swala la elimu ili kuweza  kuwawezesha vijana  kuwa  katika mazingira mazuri ya kusomea.

Aidha kwa upande wake meneja  masoko na mawasiliano wa mfuko huo wa penisheni, James Mlowe,ameeleza kuwa sababu za kutoa msaada huo wa mabati ni kutokana na changamoto za upungufu wa madarasa ,hivyo wao wameona  ni vyema kutoa mabati  hayo.

Afisa elimu wa wilaya  Deus Seif,amegusia swala la uhaba wa vyumba vya madarasa ambapo amesema kuwa kwa sasa jumla ya madarasa yaliyopo ni 1585 na vyumba vinavyoitajika ni 3715.

No comments:

Post a Comment