Tuesday 22 March 2016

WATU WAWILI WAPOTEZA MAISHA KWA KUPIGWA NA WANANCHI KATIKA KATA YA LUDETE WILAYANI NA MKOANI GEITA.

                 Kamanda  wa jeshi la polisi mkoa wa geita Mponjoli Lotson.

Watu wawili wamepoteza maisha  kwa kupigwa na wananchi katika kata ya Ludete  wilayani na mkoani  Geita kwa kile kinachosadikika kuhusika katika tukio la kujaribu kuvamia katika nyumba ya Bw.Deusi  Francis mkazi wa kijiji cha Lwamgasa Mkoani hapa.


Akithibitisha kutokea kwa tukio hilo kamanda wa polisi mkoani  Geita Bw.Mponjoli  Lotson amesema tukio hilo limetokea usiku wa kuamkia machi 21 majira ya saa kumi usiku ambapo watu hao wameuwawa kwa kupigwa  na wananchi.

Vilevile  kamanda Mponjoli amewataja waliouawa kuwa ni Paschal Charles (28) mkazi wa Bulengahasi na Pastori Magendo(30) ambaye yeye ni mkazi wa kata ya Ludete mtaa wa stooni mbali na hayo pia watu wawili wanashikiliwa  kwa ajili ya upepelelezi  zaidi kutokana na tukio hilo.

Katika hatua nyingine Jeshi la polisi mkoani Geita limetoa wito kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria  mkononi na kwamba wale wote watakaobainika kuhusika katika  tukio hilo sheria haitosita kuchukua mkondo wake ikiwa ni pamoja na kufunguliwa kesi ya mauaji.

No comments:

Post a Comment